Ndoa ni kitu fulani delicate sana itategemea kabla na baada ya ndoa ulijenga falsafa gani ya kuendesha family yako, yaani ni participatory or non participatory katika upande wa financial, kwani lakini umsome mwenza wako kwa upande wa financial management na ndipo unaweza ukatengeneza utaratibu wa kuendesha familia yako, kuna familia nyingine mwanamume ndiye mtumiaji mbaya wa hela na mwanamke akawa tight nad vice versa.
Kuna siku tulikuwa tunabishana kuhusu kumshirikisha mwenza wako katika mambo yako, jamaa akadai mke wako jaribu kumshiriki baadhi ya mambo na sio yote hasa yale yanayohusu kuweka kifuani kwa muda wote au kipindi fulani kwani mkigombea ambacho kwenye ndoa ni jambo la kawaida atachulia lile jambo ni rungu la kukufanya unyamaze,Kkuna jamaa alimwambia mke wake je unaweza kuvumilia na kutunza siri zangu na ubaya wangu wote kama mme wako, mke alijibu ndiyo,jamaa alikuwa na ugomvi na jamaa x baada ya kugundua alikuwa anamfukuzia mke wake na alipomuuliza mke wake alimjibu jamaa x ananisumbua sana na ananikera sana huku njiani kwani angejua mimi nimetokea kumchukia kwa kitendo cha kunisumbua akijua mimi ni mke wa mtu, jamaa akasema sawa mke wangu lakini angalia maisha haya magumu na magonjwa,Siku moja jamaa alichelewa kurudi nyumbani alipofika akamwambie mke wake, jamaa x nimekutana naye nikampiga hadi kumuua na nimemzika karibu na mgomba kule nje, kwa muda huo jamaa x alisafiri hivyo yule mwanamke akaamini kuwa ni kweli amaemuua, jamaa alijua siku ambayo yule jamaa x alikuwa anarudi, usiku akamchokozke wake na ukatokea ugomvi mkubwa na jamaa alimpiga makofi kadhaa, mke wakemuuaji mkubwa wewe na ndo maana unataka kuniua hata mimi, hivyo sikubali, wakalala mzungu wa nne,asubuhi jamaa akaanzia tena mjadala ule ulipelekea mgomvi kwani alijua yule jamaa x ndo siku ambayo alikuwa anarudi, yule mke wake alienda polisi kushitaki kuwa jamaa ni muuaji kwani alitaka kumuua na tayari amemuua jamaa x na amemzika palepale nyumbani kwake,polisi walichuukua 110 na yule mama, walipofika walimkuta yule jamaa anakunywa chai, walimkata na kumfunga pingu kwa sababu jamaa hakuwa msumbufu hakupigwa, yule mama aliulizwa amemzika wapi wapi alionesha wakaamua kumwambia afukue, walikute kuna mfuko (kiroba) kimefunga na kina damu damu watu wote waliamini kuwa jamaa kamuua jamaa x, walipoungua ndani walikuta mzoga wa mbuzi ambaye jamaa alikuwa na mbuzi, ghafla mbuzi yule alikufa na bwana mifugo alimwamuru amuzike kwani alikuwa mgonjwa. Na bahati nzuri kwa yule jamaa mara jamaa x ndo anarudi na kushangaa kwa jirani kuna watu wengi ikibidi asogee, jamaa alipoulizwa akaeleza kama hapo juu makubaliano yake na mke wake, Je unajifunza nini katika masuala uwazi na mawasiliano katika ndoa? kwani jamaa alisema sio kila kitu unapaswa kumshirikisha mke wako kwani mke wake na jamaa x walikuwa bado wapenzi.