Ndoa inapokuwa ni ya ndugu na wazazi………………

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,354
Matatizo ya ndugu au wazazi kuingilia ndoa ni suala linalotajwa sana katika kuvunjika kwa ndoa nyingi. Wengi wetu tunajua kwamba kwa mila na desturi zetu(ambazo ni potofu hata hivyo) ndoa inakuwa ni ya ndugu na wazazi pia, siyo wanandoa peke yao.
Lakini kwa bahati mbaya sana, katika ndoa nyingi, ndugu wa wanaume ndio ambao huingilia ndoa kwa kuwasakama wake katika ndoa hizo. Kwa mila na desturi hizo hizo, wanaume wengi hujikuta wakiwaunga mkono wazazi au ndugu zao dhidi ya wake zao.
 
SaraM

Senior Member
Sep 8, 2011
162
109
mwanaume ukiwa dhaifu hata jirani au hata hosegirl anaweza kuingilia ndoa yako.....

ukiwa strong hata nani hathubutu....trust me...
Kweli kabisa mkuu maana kuna wanaume wamewaachia mama zao waongoze nyumba zao mpaka huruma
ninapenda mwanaume mwenye msimamo kwa kweli, kuna dada angu mumewe alikuwa anaambiwa na dada
ake eti kilaukifika nyumbani tu unaenda kukaa chumbani na mkeo, na sie tunataka kuongea na wewe
yule shemeji alimjibu kama unamwona anafaidi kuongea na mimi njoo na wewe tuongee, ilikua kesi kubwa
lakini meseji ilifika wakakoma, sasa dada anaishi kwa amani
 
caven dish

Senior Member
Sep 12, 2011
124
86
Kwa kweli umeugusa mtima wangu. Sijui nikupe nini kwa kuitengeneza siku yangu leo!!!!!!
 
Kaizer

Platinum Member
Sep 16, 2008
25,287
17,741
Kweli kabisa mkuu maana kuna wanaume wamewaachia mama zao waongoze nyumba zao mpaka huruma
ninapenda mwanaume mwenye msimamo kwa kweli, kuna dada angu mumewe alikuwa anaambiwa na dada
ake eti kilaukifika nyumbani tu unaenda kukaa chumbani na mkeo, na sie tunataka kuongea na wewe
yule shemeji alimjibu kama unamwona anafaidi kuongea na mimi njoo na wewe tuongee, ilikua kesi kubwa
lakini meseji ilifika wakakoma, sasa dada anaishi kwa amani

hapo tu ndo patamu

Inakera sana vitu vya namna hiyo
thanks God hayo kwen baadhi ya ndoa hayapo.
 
daughter

JF-Expert Member
Jun 22, 2009
1,275
739
Chanzo cha ili tatizo ni udhaifu wa mwanaume kama The Boss alivyosema. Dawa ni wewe mume ufahamu na kukubali kuwa you are no longer accountable to your mom and sisters but to yo ur wife.Ila kuna mijanaume inakera kwa kweli kila mtakacho kipanga ndani lazima mama aambiwe and in worst cases mama ndio anafanya maamuzi.
 
The Priest

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
1,030
256
Umenikumbusha film moja inaitwa Our Family wedding,baada ya wazazi na ndugu kuingilia sana mahusiano yao pamoja na harusi,mwisho wa siku jamaa akaweka msimamo na mtu wake kuwa "Their Wedding,Our Marriage" ukigundua hilo hawakupi tabu!
 
BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,760
572
kawaida ndoa haikosi misuko suko ila kuna misuko suko mingine hupeda wenyewe wanandoa kwa kutoa mambo ya ndani
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,609
7,813
Matatizo ya ndugu au wazazi kuingilia ndoa ni suala linalotajwa sana katika kuvunjika kwa ndoa nyingi. Wengi wetu tunajua kwamba kwa mila na desturi zetu(ambazo ni potofu hata hivyo) ndoa inakuwa ni ya ndugu na wazazi pia, siyo wanandoa peke yao.
Lakini kwa bahati mbaya sana, katika ndoa nyingi, ndugu wa wanaume ndio ambao huingilia ndoa kwa kuwasakama wake katika ndoa hizo. Kwa mila na desturi hizo hizo, wanaume wengi hujikuta wakiwaunga mkono wazazi au ndugu zao dhidi ya wake zao.

Mtambuzi,

Hapo kenye red pananipa tabu kidogo.

Ni potofu kwa vigezo vipi? Je vigezo hivyo ni universal? Nani anayesema/aliyesema potofu? Iliyonyooka inatakiwa kuwaje kuwaje?
 
Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,956
3,297
Baadhi yetu sisi wanaume ndo tunayakaribisha haya na tunasahau kuwa:
  • Ndoa inajengwa na watu wawili tu.
  • Ndoa haina m/kiti wala kamati kuu, hivyo vinaishia siku ya harusi yako tu na baada ya hapo kila kitu kinabaki kwenu wawili tu.
 
HekimaMoyoni

Member
Dec 9, 2010
55
17
I stand to be correct....

Ukiona ndoa inaingiliwa na ndugu, Mama/Baba mkwe, mawifi na mashemeji. Tatizo mara nyingi ni udhaifu wa Mwanamme.
Mume anashindwa kutenganisha kati ya ndugu/wazazi na Mke, na majukumu gani anapaswa kufanya kwa ndugu au Mke.

Sikatai kwamba kuna baadhi ya wanawake wakorofi ktk ndoa...
 
Shantel

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
2,018
1,108
Tatizo utakuda dume zima na lina mke , kutwa oooh my dad, my mom, haipiti dk unategemea huyu atakuwa na maamuzi yake kweli, mwanaume unatakiwa usimame kidete, hakuna kuweka mwanya wa mkeo kunyanyasika, au kuwaruhusu wazazi wako waongoze nyumba
 
mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,777
4,625
Umenikumbusha film moja inaitwa Our Family wedding,baada ya wazazi na ndugu kuingilia sana mahusiano yao pamoja na harusi,mwisho wa siku jamaa akaweka msimamo na mtu wake kuwa "Their Wedding,Our Marriage" ukigundua hilo hawakupi tabu!
dah hapo kwenye red nimeipenda hyo mkuu
 
nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,312
8,346
Kama umeoa afu bado wazazi wana wa finance unategemea nini lazima wawe na sauti; he who pays the piper...

Kuna kijana namjua ni mtoto wa kiume pekee wa familia tajiri. Baba yake alifariki muda sana. Mama yake ana maela ya urithi kama hana akili nzuri. Huyo kijana amemuoa rafiki wa dada yangu. Wanaishi kwenye nyumba ya urithi; bonge la house kwa kuwa baba yake aliacha several houses tena zote ziko strategic areas.

Sasa mama mkwe wa huyo dada ana sauti mwanzo mwisho. Yani kuna moja ni kali jamaa alikuwa anatoka ulaya; mama kaenda kumpokea wakakutana na wife airport; mama akaamuru kijana aende moja kwa moja nyumbani kwake wameandaa dinner ataenda kwa mkewe kesho yake.

Haya mambo ya sijuho mtoto anapokea, sijuhi nini, mama anawaamulia mpaka wajukuu wavae nini.

Wamama kama hawa wanakuwa wamewalea watoto wao wa kiume kuwatii saana na huwezi kubadili hilo ni kukubali matokeo.

Na ukirogwa ukatamka sijuhi chagua moja mimi au mama yako, utazimia maanake possibility ya mama kuwa chaguo ni 99%

Watu kama hao wanaoa tu kutimiza wajibu but they feel that they have everything being with their family (mom and sisters)
 
Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,354
Mtambuzi,

Hapo kenye red pananipa tabu kidogo.

Ni potofu kwa vigezo vipi? Je vigezo hivyo ni universal? Nani anayesema/aliyesema potofu? Iliyonyooka inatakiwa kuwaje kuwaje?

Ndoa kuwa ni ya wazazi au ndugu ni mila potofu..........ni mila ambayo haina mashiko, zaidi ya kuingilia uhuru wa wengine........
 
mdeesingano

Member
Aug 12, 2008
65
19
Ha ha ha.... Hizi comment naziona kama zote ni:

TATIZO LA MARAFIKI NA JAMII KUINGILIA NDOA ZA WATU....
Ukifuatilia hii post na hizi comment unakuta ndoa yako hivi sasa imeingiliwa na makundi manne: NDUGU, WAZAZI, JAMII na MARAFIKI!

Said Mdee
Administrator
JigambeAds
Ya kiTz kwa waTz
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
45,222
95,816
Kama umeoa afu bado wazazi wana wa finance unategemea nini lazima wawe na sauti; he who pays the piper...

Kuna kijana namjua ni mtoto wa kiume pekee wa familia tajiri. Baba yake alifariki muda sana. Mama yake ana maela ya urithi kama hana akili nzuri. Huyo kijana amemuoa rafiki wa dada yangu. Wanaishi kwenye nyumba ya urithi; bonge la house kwa kuwa baba yake aliacha several houses tena zote ziko strategic areas.

Sasa mama mkwe wa huyo dada ana sauti mwanzo mwisho. Yani kuna moja ni kali jamaa alikuwa anatoka ulaya; mama kaenda kumpokea wakakutana na wife airport; mama akaamuru kijana aende moja kwa moja nyumbani kwake wameandaa dinner ataenda kwa mkewe kesho yake.

Haya mambo ya sijuho mtoto anapokea, sijuhi nini, mama anawaamulia mpaka wajukuu wavae nini.

Wamama kama hawa wanakuwa wamewalea watoto wao wa kiume kuwatii saana na huwezi kubadili hilo ni kukubali matokeo.

Na ukirogwa ukatamka sijuhi chagua moja mimi au mama yako, utazimia maanake possibility ya mama kuwa chaguo ni 99%

Watu kama hao wanaoa tu kutimiza wajibu but they feel that they have everything being with their family (mom and sisters)

mimi huamini wadada wanao olewa na wanaume wenye kutoka familia tajiri
hujuta.......

mwanaume atafute pesa yake mwenyewe,ajue shida na umasikini ukoje
ndo anakuwa kakomaa.
hao born with silver spoon in their mouth,hawawezi majukumu mengi,hata ya kitandani pia ni wachovu lol
kwa sababu hawajui kuwa rejected au kutokubalika inakuwaje
uki experience hivyo vitu,lazima ujifunze to up your game....na also how to humble sometimes
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom