Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Matatizo ya ndugu au wazazi kuingilia ndoa ni suala linalotajwa sana katika kuvunjika kwa ndoa nyingi. Wengi wetu tunajua kwamba kwa mila na desturi zetu(ambazo ni potofu hata hivyo) ndoa inakuwa ni ya ndugu na wazazi pia, siyo wanandoa peke yao.
Lakini kwa bahati mbaya sana, katika ndoa nyingi, ndugu wa wanaume ndio ambao huingilia ndoa kwa kuwasakama wake katika ndoa hizo. Kwa mila na desturi hizo hizo, wanaume wengi hujikuta wakiwaunga mkono wazazi au ndugu zao dhidi ya wake zao.