Ndoa inaelekea kumshinda, ushauri wenu tafadhalii

Ndoa inaelekea kumshinda, ushauri wenu tafadhalii

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,435
Reaction score
5,077
Kwema wana MMU

Niende kwenye mada,

Kuna mwanaume mmoja ana mke na watoto wawili, na yupo kwenye ndoa kwa miaka nane sasa. Ila ndoa ilipofikisha muda wa mwaka mmoja aliingiwa na pepo la uzinzi akaanza kuchepuka tangu hapo ndoa ikawa inayumba.

Mke akawa kila akijua mchepuko mpya wa mumewe ni ugomvi usio na mfano, unatokea kati yake na mmewe. Sasa mwanaume anaona kama mke mkorofi, na anadai anambana pia hana akili maana badala ya kufatilia maisha yeye anamfatilia mmewe.

Pia anasema mkewe anatakiwa i atumie busara ya kushuka hata kama anakosewa na mme wake waziwazi haijalishi maana yeye ni mwanamke anatakiwa kuwa chini tu sio kutumia nguvu kubwa badala ya kutumia busara kusolve tatizo.

Hivyo akazidi kuchepuka zaidi. Pia kuna mchepuko ambao kadumu nao kwa miaka mitano tangu kipindi hicho hawajawahi gombana na huo mchepuko maana mchepuko hana makuu yeye kila kitu sawa hata akikosewa anaomba msamaha. Na unampost mtandaoni hivyo anaona kama una mapenzi ya dhati na unajielewa sana kuliko mkewe .

Sasa mwanaume huyu kaamua kuvunja ndoa na mkewe ili amuoe huyo mchepuko ambaye hakasiriki mwanaume akichepuka.

Je yupo sahihi kumuacha mkewe na kumuoa mchepuko au mnamshauri nini {Ndoa ni ya kanisani }
 
Mwanamke akishakuwa ndio main road anageuka na kuwa selfish
Kuchungwa kunaanza upya.
Huyo mwanaume bwege.
Anachepukaje mpaka kudisturb familia?
Mwanaume unatakiwa mkeo akisikia unachepuka akutetee kabisa.
 
Kuchepuka nje lazima kuwepo na sababu,mfano labda jamaa ana nguvu nyingi ambazo mkewe hawezi kuhimili n.k Pia anapochepuka ahakikishe 3/4 ya mapato yanarudi kwa mkewe/familia,na 1/4 inayobaki ndio achepuke nayo.Mwanaume akifanya hivyo,ugomvi hautakuwepo....ila kama 3/4 ndio inaenda kwa mchepuko na sababu ya kuchepuka labda ni tamaa hapo lazima mgogoro uwepo.Kwa hiyo inategemea na sababu.
 
Hapo ndipo baadhi ya wanaume wanapokosea, heshima ni lazima iwepo ndani kwako inakuaje unaruhusu siri zako nje mke wako ajue. Watu tunavisimu vidogo vile vya tochi na number nyengine kabisa ukirudi home unakiacha kazini au unakificha sehem salama kwenye gari na unahakikisha kipo silence.
 
Aoe mchepuko afikiri kama ataendelea kumskiliza ivo, wamedumu miaka 5 ndoa itavunjika ndani ya miezi6 utakuja na mrejesho apa siku si nyingi
 
Huyo mwanaume ni mpumbavu, kosa lake yey anamshushia mzgo mkewe?? Baada ya kugundulika amechepuka alitakiwa awe mtulivu (mana ni ujinga kuchepuka had mkeo anajua, inakuwa syo staha)
Na anafikiri mchepuko ana heshima kuliko mkewe eti kila kitu kwake ni sawa, anakubaliana ivo kwa sababu ndo nafasi yake, asifikiri atamuweka ndani km mke afu aendelee kuwa mpole, yaan atakuwa kichaa zaidi ya mke wa kwanza wataachana ndani ya miezi atamrudia mkewe anayemuumiza saivi anaona hana maana
 
Hebu kuweni serious kidogo, yani uhalalishe uzinzi? Tena uache mke! Taasisi ya ndoa imepoteza watetezi, wamebaki makimbukeni.
 
Back
Top Bottom