Ndoa Imara ? Zingatia Haya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoa Imara ? Zingatia Haya!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 17, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  [h=3]Ndoa Imara ? Zingatia Haya![/h]

  [​IMG]
  FUNGUO ZA KUJENGA NDOA IMARA NA MAHUSIANO YA KUDUMU
  <!--[if !supportEmptyParas]-->
  USIKAE NA DONGE MOYONI
  Kitu kizito kuliko vyote kukibena duniani ni DONGE MOYONI (grudges)
  Pia unaweza kuathirika zaidi na kile umeweka moyoni kwani mwenzako anaweza kuwa hajui.
  Kuweka vitu moyoni bila kuvitoa au kuzungumza na mwenzi wako huweza kuathiri afya na amani.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  [h=1]Kawaida kama una hasira hakikisha unazimaliza mapema na kuelewana na mwenzi wako kabla jua halijazama na kama ni usiku hakikisha unaenda kulala huku umeshalitoa donge lako.[/h]
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  FAHAMU KWAMBA HONEYMOON SIYO MAISHA NDOA
  Kuna tofauti kubwa kati uchumba, Honeymoon na maisha ya ndoa, uchumba na Honeymoon hupewa moto kemikali ambazo zimo ndani yetu. Hatua ya pili ambayo ni ndoa yenyewe hapa tairi linakutana na barabara ili kuweka wazi uimara na udhaifu. Katika ndoa ni majukumu na kuwajibika na familia iliyoanzishwa, wakati uchumba na Honeymoon ni kuburudishana.
  [h=1]<!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->[/h][h=1]MUNGU KWANZA[/h]
  Kumweka Mungu kwanza katika ndoa, huleta furaha ya kweli (joy) faraja na ulinzi. Kumweka Mungu kwanza maana yake mume na mke wanaishi kwa utii na amri za Mungu mwanzilishi wa ndoa wanaomba pamoja na kuwa na mahusiano yanayoongozwa na Mungu. Kwa vipimo vya kibinadamu huwezi kuwa na furaha siku zote kwa safari ndefu kama ya ndoa furaha ya kweli hupatikana kwa kumuweka Mungu namba moja.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  MFAHAMU MWENZI WAKO NA KUJIFAHAMU WEWE MWENYEWE
  Baada ya mapenzi ya Honeymoon kwisha wanandoa huwa na mgodi wa kuanza kuchunguzana na kufahamiana. Wakiwa Honeymoon wanandoa huona kila kitu shwari, wakianza maisha ya ndoa kila mmoja huanza kuona makosa kwa mwenzake hata Kirusiyo hiyo ni nafasi ya wanandoa kufahamiana ni nafasi nzuri ya wanandoa kusifiana, kutumia muda pamoja, kupeana zawadi, kusaidiana kazi ndogo ndogo za nyumbani, kubusiana na kukumbatiana (touch)
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  KUWA MSIKILIZAJI MZURI
  Binadamu ana asili ya kupenda kuongea zaidi kuliko kusikiliza, kusikiliza kuna maana zaidi kuliko kuongea, wanaume Huongea ili kitu kifanyike na mwanamke Huongea kuchangia wazo na hisia zake. Kuna wakati kila mwanandoa anahitaji kusikilizwa wanaume ni vizuri kuwasikiliza wake zao wanapotoa mawazo yao na hisia zao. Mwanamke huongea maneno 45 elfu kwa siku, na mwanaume 15 elfu, ni nani anahitaji kusikilizwa zaidi?
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  KICHEKO
  Wanandoa wanahitaji kuwa na kicheko siyo kuwa serious kila wakati kutaniana kusikopitilizwa huongeza furaha katika ndoa pia ni zawadi kutoka kwa Mungu. Wanandoa ni muhimu kuwa na wakati ambapo wanaweza kukaa pamoja na kuwa na kicheko iwe ni kuangalia TV na kusimuliana hadithi ambazo zinawafanya mcheke ni vizuri wanandoa kucheka wakiwa wao wenyewe au wakiwa pamoja na watu wengine. Kicheko huleta raha katika ndoa.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  JIFUNZE KUKUBALI KWAMBA UMEKOSA NA KUOMBA MSAMAHA
  Binadamu wote tunafanya makosa na wakati mwingine hayo makosa huumiza tunaowapenda. Lazima tukumbuke wakati tumekosa tunahitaji tuombe msamaha. Usizunguke (indirect way) bali be straight sema “Nisamehe au I am sorry”. Pia usibadili topic au kuanza kusifia ili usiombe msamaha.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  Pia tunahitaji kufahamu kwamba wenzi wetu si mara zote wapo perfect kama ulivyo wewe (imperfect).
  Pia ni vizuri kufahamu kwamba ndoa ni kazi inayoendelea na siyo mwisho wa safari.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  MHESHIMU, USIMDHARAU
  Kumdharau mwenzi wako wakati mwingine huwa kitu rahisi sana. Mwanzo wa mapenzi hata kama kuna hitilafu mara nyingi huitilii maanani, una minimize, lakini baada ya honeymoon kwisha utaona na kukumbuka/ Tambua mambo mengi ambayo huyapendi na unaweza kuanza kupambana nayo na kumdharau mwenzi wako.
  Kumdharau mwenzi wako ni kama mmomonyoko ambao ni sumu kwenye mahusiano.
  Mwanandoa mwenye busara hawezi kumuaibisha mwenzi wake bali ataongea kwa hekima na kumaliza tofauti zozote kwa upendo.
  Kawaida angalia uwezo wake na si udhaifu wake.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  USICHUJE (filtering)
  Usimchekeche na kumbandika jina la kudumu kwamba mara zote yupo vile:
  Sentensi zinazoanza na haya maneno uwe makini sana
  Kila siku unafanya KirusiiKirusii…………………..
  Mara zote nakwambia lakini………………
  You never……………………
  You always……………………
  Mara nyingi Ukitokea msuguano wengi huanza kulalama kwa kutumia hayo maneno huwa na maana kwamba unafanya the same mistake over and over na anakupa hicho kibandiko kama jina la mkosaji wa kila siku.
  Si kweli kwamba unaweza kufanya makosa yaleyale kila siku, muda wote miaka yote.
  <!--[if !supportEmptyParas]--> <!--[endif]-->
  WEKA MKAZO KWENYE UWEZO NA SI UDHAIFU
  Mwanamke na mwanaume wapo tofauti siku zote na ni mpango wa Mungu kuwa tofauti ili kwa tofauti tuweze kusherehekea uumbaji wa Mungu na ili mke na mume waweze kila mmoja kumridhisha mwenzake.
  Huwezi kuwa na mwenzi ambaye ana udhaifu mwingi kuliko uwezo na ukiona ana udhaifu mwingi kuliko uwezo basi tatizo ni wewe si yeye.
   
 2. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  thenk to u!
  Wenye masikio wameöna
  Na wenye macho wamesikia.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  [h=3]DALILI ZA NDOA INAYOKUFA[/h]

  Jitahidi kuhakikisha unalinda moyo wako na moyo wa mpenzi wako; usije ukaupasua na kuuumiza.[​IMG]
  Wanandoa wengi hujikuta wamefika mahali ambapo ndoa haiwezi kuwepo tena (talaka) na tatizo kubwa ni kwamba wengi hukaa bila kuchukua hatua zinazostahili (serious) wakati tatizo au mgogoro unapojitokeza ili kumaliza tatizo
  Kutoshughulikia vizuri tatizo lolote kwenye ndoa hupelekea
  Chuki,
  Uchungu,
  Kinyongo,
  Kuumia hisia na
  huweza kusababisha mwanandoa mmoja kujiondoa katika muungano wa kindoa uliopo
  (kuanza kuishi kivyake katika kufikiria na kutenda).

  Zifuatazo ni dalili mbaya sana ambazo zinaonesha ndoa inayoelekea kwenye kifo

  KUFIKIRIA MAISHA KIVYAKO BILA MKE AU MUME KUMUHUSISHA
  Ukiona unaanza kufikiria uzuri wa maisha utakavyokuwa bila mwenzi wako kwa maana kwamba kuwa na yeye unaona asilimia mia moja anakulostisha, au hana maana kabisa ni dalili kwamba hiyo ndoa inaelekea kwenye kifo cha ghafla.
  Na kama unasongwa sana na mawazo kutaka kuishi mwenye au na mtu mwingine zaidi ya huyo uliye naye na kujiona utakuwa na amani zaidi basi unaelekea kubaya kwani inaonesha umeshapoteza nafasi yake ndani ya moyo wako na kitu cha msingi waone washauri wa mambo ya ndoa ili waweze kukusaidia.

  MAMBO MABAYA NI MENGI KULIKO MAMBO MAZURI KWENYE NDOA YAKO
  Kama mnajikuta ndoa yenu ina mambo mabaya mengi zaidi kama vile
  kutokuelewana, k
  ila mtu ana hasira,
  mnapishana lugha kila mara,
  hakuna kucheka wala kufurahishana na
  mambo mazuri kama kucheka pamoja,
  kufurahi pamoja,
  kujisikia bila mwenzako siku haiendi
  basi hiyo ni dalili kwamba hiyo ndoa inahitaji msaada na bila kuifanyia ukarabati basi itasombwa na mafuriko na hatimaye kufa.

  UNAJISIKIA VIGUMU SANA KUWASILIANA NA MKE AU MUME WAKO
  Je, unajisikia kupatwa na hofu au mashaka kuongea na mke au mume wako kuhusu matatizo ya ndoa yako au maisha yenu kwa ujumla?
  Mawasiliano ndiyo njia pekee ya kuondoa stress za ndoa na maisha kwa ujumla na hatimaye kujenga ndoa yenye afya kwa wanandoa.
  Kama mkiwa pamoja mnakuwa kimya bila kuongea chochote na hakuna dalili ya kutaka kuongea na mwenzako basi kuna tatizo kubwa sana, hasa kama ni tofauti sana na kawaida yenu hasa jinsi ilivyokuwa katika siku za kwanza wakati mnachumbiana.
  Kama hujisikii vizuri kuwasiliana na mwanandoa mwenzio basi hiyo ni dalili kwamba tayari umekosa imani kwake na ndoa huwa inakuwa katika wakati mgumu kukiwa kauna kuaminiana (trust)
  Pia kama wewe ni mtu wa mwisho kujua kitu chochote muhimu au kuzuri kuhusu yeye, basi hapo kuna tatizo kwani ni kawaida wanandoa kuelezana vitu vizuri vinavyotokea kwa mmoja wao.

  KILA MMOJA KUKATAA KUHUSIKA NA MATATIZO AU MIGOGORO YA NDOA INAPOJITOKEZA
  Kama kila mmoja anajilinda na kutothamini hisia za mwenzake hasa linapotokea tatizo na kuanza kumrushia mwenzake lawana kwamba ndiye muhusika na wote mnakuwa na msimamo huohuo, fahamu kwamba hapo ndoa inapitiliza hata tiba za uangalifu zinazopatikana ICU.
  Ikiwa migogoro au matatizo yanapojitokeza kuna kuwa na kushindana kwa kila mmoja kukwepa kuhusika na badala ya kupata suluhisho mnajikuta mgogoro unazidi kuongezeka basi hiyo ni dalili kwamba sasa mmeanza kubusu kifo cha ndoa.

  KUJIKUTA NI WEWE PEKE YAKO TU UNAHUSIKA KATIKA KUTATUA MIGOGORO AU MATATIZO YA NDOA.
  Je, umekata tamaa, au kujisikia vibaya kuongea masuala ya matatizo ya ndoa yako kwa sababu mwenzako anakurudisha nyumba, au imefika mahali na wewe umeamua kunyamaza na kuachana kabisa na kujishughulisha na tatizo lolote katika ndoa na matokeo yake hakuna hata mmoja anajali tena kushungulikia matatizo ya ndoa?
  Kama mpo kwenye matatizo na kila mmoja amenyamaza kimya katika kuhakikisha mnamaliza tatizo lililopo basi hii ndoa ipo ICU na kama mtabaki kimya bila kila mmoja wenu kuhusika ili kuhakikisha ndoa inarudi kwenye mstari basi ni kama bomu lililotegwa ardhini na siku mtu akikanyaga hakuna kitakachosalia.

  TENDO LA NDOA
  Kama mmoja wenu sasa hana hamu kabisa na tendo la ndoa, au wote kwa pamoja hamna hamu kabisa ya tendo la ndoa hiyo ni dalili kwamba somethings is wrong.
  Kukosa faragha ya pamoja (intimacy and affection) itawafikisha mahali ambapo ndoa inaweza kufa au kuwa na ndoa isiyokidhi haja au kukosa kuridhishana inavyotakiwa.
  Je mnaishi tu kwa sababu ya watoto ndo wamewafanya msiachane?
  Kama ni ndiyo basi mnahitaji kupata msaada wa washauri wa mambo ya ndoa kwani hakuna tatizo lolote kwenye ndoa ambalo halina jibu.
  Kama hakuna hamu ya mapenzi kwa mmoja wenu au wote maana yake hisia zenu zipo mbali sana na hiyo ni dalili kwamba kila mmoja anaenda njia yake.

  KUBISHANA AU KUGOMBANA KWA KITU KILEKILE KILA MARA
  Kama kubishana, kupishana, kugombana, kuanzisha zogo kila mara kunatokana na issue ileile moja bila kupata suluhisho basi hiyo ndoa imesimama haikui wala kuelekea kwenye uimara zaidi bali inatelemka kwenda kwenye shimo.
  Kama hakuna kitu kipya kinatokea ili kupata ufumbuzi wa hiyo hali basi tafuta mshauri wa mambo ya ndoa ili awasaidie.

  HITIMISHO
  Hakuna tatizo la ndoa ambalo halina jibu hapa duniani kuna washauri wa mambo ya mahusiano na ndoa, wazazi ambao hupenda mafanikio ya watoto wao, kuna wachungaji ambao wana hekima na busara walizopewa na Mungu kwa ajili ya kuwashauri hivyo hata kama kuna tatizo kubwa namna gani jibu lipo na tiba ipo.
  Anza kwa kuzungumza na mwanandoa mwenzako then ikishindikana nenda kwa watu mnaona wanaweza kuwasaidia, usiwe mbishi wala mbabe ndoa ni kuchukuliana na kuelewana.

   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Always Love What You eat.
  Kuna wengine hata tule namna gani mwili wapi wakati wengine wakila kidogo tu mwili unajibu.[​IMG]


  Utafiti ni msingi wa maendeleo yoyote.
  Katika nchi nyingi zinazoendelea (zilizogoma kuendelea) tafiti nyingi zinafanya na huwekwa makabatini bila kufanyia kazi na ukiuliza sababu utaambiwa serikali hazina pesa.

  [​IMG]


  Vinyago vinatambulisha utamaduni
  [​IMG]

  Je hapa ni aina gani ya mti unaujua?
  [​IMG]


  Watafiti wanasema Kucheka ni dawa basi kuna wakati mtu inabidi upige story tu ili watu mcheke na mfurahi na kupata tiba.
  [​IMG]  Kuna watoto badala ya kumfundisha yeye ndo anakufundisha pia mazingira ni kitu muhimu sana.
  Pia mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
  [​IMG]
  Dunia imebadilika, wanawake sasa wanafanya kazi zote kama vile kuwa bibi misitu, kuendesha malori, kuwa marubani nk.
  Hivyo mwanamke lazima awezeshwe ili kusaidia kuleta mafanikio katika familia
  [​IMG]  Kuna wakati unaweza kutembelea sehemu ukatamani ujenge nyumba na kufanya mkazi katika dunia asili
  [​IMG]
  Darasa
  [​IMG]
  Wale wa Njombe je hapa hii miti ina miaka mingapi?
  [​IMG]

   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  [h=3]Mambo ya Kuepuka Wakati wa shida/Mgogoro wa Mahusiano ya Ndoa.[/h]

  Hapo kila mtu kivyake, Kila mtu mbabe, kila mtu anajiona hana kosa, hakuna kuongea, hakuna kugusana hata unywele; Ndoa ina raha yake hata mkosane vipi bado mnalala pamoja, hata hivyo kwa nini msijadili pamoja na kupata jibu then muendelee na kujirusha kama kawaida.[​IMG](Picha kwa hisani ya visionofserenity)


  Kila mahusiano ya ndoa hukumbwa na migogoro ya hapa na pale, inaweza kuwa wakati wa raha au wakati wa shida kwa kuwa ni binadamu migogoro huja yenyewe hadi kifo kitakapowatenganisha.
  Kitu cha msingi ni kufahamu kwa nini kuna mgogoro au tatizo, na umesababishwa na nini na ni njia ipi itumike kutatua hilo tatizo na zaidi kusameheana kwa pamoja na kusahau.

  Tafiti nyingi zinaonesha kwamba mawasiliano mazuri kwenye mahusiano ya ndoa huongeza;
  Utamu wa mahaba,
  Kuaminiana na
  Kusaidiana,
  Na mawasiliano ovyo huweza kuharibu kabisa uimara wa ndoa na kujenga kutokuaminiana na zaidi ndoa kwenda ndivyo sivyo.
  Kuna mambo ambayo tunapofanya kwenye ndoa huwa tunaona kama vile tunatatua tatizo kumbe ni kinyume chake, hebu angalia wewe ni lipi kati ya yafuatayo umekuwa unayafanya na pia kama unaweza badilisha huo mtazamo au njia ili kuimarisha mahusiano yako na huyo umpendaye.

  Moja ya mwanandoa kukwepa tatizo au mgogoro:
  Badala ya kujadili tatizo lililopo kuna watu huamua kubaki kimya tu kana kwamba tatizo litayeyuka lenyewe kama barafu.
  Na wakati huohuo kutokana na tatizo au mgogoro mtu anakuwa na mawazo kiasi kwamba unajua kuna jambo linamsuta kwenye mawazo na moyo wake.
  Hadi tatizo au mgogoro ukue sana ndipo kwa hasira mtu anapasuka.
  Kuogopa eti tutabishana sana isiwe sababu ya kuacha tatizo liwe linakaa tu, ni jambo la busara kuelezena ukweli na kulimaliza tatizo na yule ambaye amekosea akubali na mwenzake amusamehe kwani hakuna aliye mkamilifu asilimia mia, bali kwa udhaifu wetu tunasaidiana na kukamilishana hivyo kuwa wazi na kuliezeza tatizo au mgogoro na hatimaye kupata suluhisho ndiyo dawa kamili si kubaki kimya.
  Pia wapo wanandoa ambao tatizo likitokea anakataa katakata kabisa kuongea na anaweza kusema hilo tutaongea kesho na kesho anakwambia kesho, then kesho hadi inakuwa mgogoro mzito.

  Kujilinda:
  Badala ya kufungua moyo na kumuelewa mwenzako wewe unakataa kusababisha tatizo mbaya zaidi unakwepa kwamba kuhusika katika hilo tatizo au mgogoro.
  Hapo badala ya kutatua tatizo unaongeza zaidi kwani mwenzio kwanza atajisikia kwamba hujamsikiliza na pia umemdharau kwa kujiona wewe huna kosa.
  Matokeo yake tatizo au mgogoro utaendelea kukua na kufukuta.
  Kitu cha msingi hata kama unahisi huhusiki basi msikilize mwenzako na jaribu kuangalia umehusika vipi kusababisha mgogoro au tatizo lenyewe kuliko kukimbilia kujilinda kwamba hijahusika.
  Wanaume (siyo wote) hapa ndo panatukamata sana huwa tunajiona huwa hatukosei na wakati mwingine hata kosa au tatizo likitokea, sisi tunaona si kosa wala tatizo.
  Wanawake ni watu wa hisia zaidi (emotional) na sisi tupo logical.
  Inaweza kuwa kwako mwanaume si tatizo ila kwa mwanamke ni tatizo hivyo msikilize na angalia wewe umehusika vipi na zaidi shiriki ili kupata suluhisho na uhakikishe kila mmoja ameridhika.

  Kudhani ni kawaida yake:
  Kuna wakati tatizo au mgogoro ukitokea, wapo ambao huanza na sentensi kama zifuatazo,
  “Kila siku upo hivihivi”
  au
  "siku zote huwa hunisikilizi”
  au
  “Hiyo ni kawaida yako”
  au
  “Nilijua tu utasema hivyo”
  Usilete mambo ya nyuma kueleza kwa mwenzio tatizo au mgogoro uliopo, badala ya kutatua tatizo unaliongeza zaidi.
  Kitu cha msingi mpe mwenzako nafasi aeleze jambo na pia husiku katika kuangalia chanzo cha tatizo ni nini siyo kurukia na kutoa hitimisho hata bila kujua jambo zima lipoje kisa unakumbukumbu ya makosa yake ya nyuma.
  Mwenye kujenga ndoa ni wewe na mwenye kuibomoa ni wewe, usione watu wanadumu na ndoa zao, kitu cha msingi wanakuwa makini kusikiliza na kuhusika katika kutatua matatizo kwa kushirikiana bila kujali matatizo au makosa yaliyopita.

  Kujiona mkamilifu
  Kwa kuwa wewe ni binadamu hata kama umesoma au upo smart sana kwenye ndoa kuna siku unakosea tu, na pia ukubali kukosolewa na kukubali kukosa ili usamehewe pia.
  Wapo wanandoa ambao yeye siku zote yupo sahihi na mwenzake ndo mkosaji.

  Kumsoma mwenzako:
  Wapo wanandoa hujiona wao wanafahamu na kujua kutafsiri hata mambo ambayo mwenzake anawaza au anafanya.
  Au ukifanya kitu anatafsiri anavyojua yeye.
  Kwa mfano; ukichelewa nyumbani kurudi, anakwambia humjali au humpendi, Usipimpigia simu anasema humjali au humpendi, au ukikataa tendo la ndoa kwa sababu unajisikia umechoka anasema humjali.
  Kitu cha msingi fahamu tatizo au sababu ni nini kwa kuongea na mhusika ndipo utoe maamuzi yako.

  Kutokusikiliza:
  Kuna wanandoa ambao mwenzake akianza kumueleza tatizo hata kabla hajamaliza anadakia na kuanza kubwabwaja anachojua yeye, badala ya kusikiliza point zilizomo kwenye hicho anaambiwa.
  Ni vizuri unapoongea na mke au mume na kama amekuomba aongee na wewe baada ya kuona kuna tatizo ni vizuri kumsikiliza kwa makini kuliko hata unavyomsikiliza bosi wako kazini, kwani usipomsikiliza mke au mume na mgogoro ukawepo hata kazini unaweza kufanya madudu.

  Kulaumiana
  Kuna watu ambao style yao ni kwamba tatizo likitokea tu yeye ni kulalamika na kulaumu mwenzake, bila hata kuchunguza vizuri chanzo na kiini cha tatizo.
  Hujiona kukiri udhaifu ni kujishusha sana mbele ya mwenzake, kama ni mwanaume atalalamika na kujiosha kwamba yeye hahusiki (ingawa anajua amehusika ila mfume dume) na badala yake kesho anakuletea zawadi ili yaishe, huko siyo kutatua tatizo bali ni ujanja tu.
  Tathmini hali ya tatizo kwa pamoja na shirikiana kumaliza tatizo.
  Tumia tatizo au mgogoro kama nafasi (stepping stone) ya kuweza kutengeneza ndoa kufikia viwango vya juu zaidi.

  Kuonekana mshindi
  Kama kila tatizo likitokea wewe ndo unataka kuonekana upo sahihi na mshindi ujue unadhoofisha mahusiano ya ndoa yako.
  Kila mara tunapokutana na matatizo lengo ni kutaka kushirikiana kutatua na zaidi kufikia muafaka huku kila mmoja akimheshimu mwenzake.
  Unapong’angania au kulazimisha kwamba mwenzako ndo amekosea hapo unaumiza hisia zake na kuumiza hisia za mpenzi wako ni kitu kibaya sana.

  Kumfikiria vibaya mwenzako:
  Wapo wanandoa ambao udhaifu wa mwenzake katika jambo fulani anaupa kibandiko (label) cha kudumu.
  Kwa mfano, mwanaume ambaye akivua nguo chumbani anaziweka mahali popote; mke wake anafikia uamuzi kwamba huyu ni mzembe na mvivu na anaachana naye kujadili na kumsaidia kuongea naye kuhusu hiyo tabia.
  Au mwana mke ambaye kila tatizo likitokea anamuomba mume wajadili; na mume ana chukulia kwamba ni mtu msumbufu sana kila jambo kujadili.
  Kitu cha msingi kila binadamu ana tabia imara na dhaifu; hivyo wewe ni mtu pekee ambaye unaweza kumsaidia kuondoa hizo tabia dhaifu kwa upendo na kushirikiana.

   
 6. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  piddy leo unamwaga somo na illustration juu....aminia na msg sent
   
 7. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Aante kwa thread ya maana
   
Loading...