NDOA: Hujaoa MBUNGE umeoa MKE

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,090
762
Jamani maada hii nimeiona ikizagaa kule FB nikaona niipost huku Kwa Wenye NDOA vurugano .. Kama itakusaidia OK ..

Bihagaze DIAGRAM

* Mume X * *.... *Mke Y
* * * * * * * 1The5:22
*1.) *roho(x)........roho(y)

*2.) nafsi(x) ........nafsi(y)

*3.){ mwili(x)<==>mwili(y)}
* * * * * * * *Mwa 2:24

Kwa kifupi Bihagaze diagram inalenga kuweka bayana maana halisi ya NDOA Na mahusiano yanayofanana Na hayo..maada nyingi sana humu nadhani majibu yake ni diagram hili ambalo limejengwa Kwa ufunuo huu..

1The5:22 *Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

Mwanadamu ni vitu au maeneo au lingano la utatu, roho yake (1kor2:10) ,nafsi Na Mwili.. Labda nifafanue kiasi..

ROHO: hili ni eneo la kiimani la Mtu, mwanadamu anafanya mawasiliano yake Na roho Kwa kuamini.. Roho ndiyo inayotia uzima Wa mwanadamu, mwanadamu ana roho yake(small r not Cap R), pili ana roho ngeni ambazo ni utashi wake kuzikaribisha, AMA roho chafu, ambazo ni roho ya dunia, roho kutoka Kwa shetani Na roho ya Shetani., au Roho kutoka Kwa Mungu(Roho mtakatifu) au Roho ya Mungu.. Huwezi kuwasiliana Na Mungu usipokuwa Na Roho itokayo Kwa Mungu(holy spirit) ambayo hutuombea Kwa Roho ya Mungu Kwa kuugua kusiko weza tamkika..sio lengo langu Kwenye somo kubwa la Roho but what I mean masuala ya imani ni ya Mtu Binafsi Na Mungu wake.. Baba hatauchukua uovu wa mwanae, haki yake mwenye haki itamkalia yeye.. So kila Mtu anapigania Imani yake Na kila Mtu atajibu kivyake mbele Za Mungu, kila Mtu atakufa Kwa siku yake Na kuhukumiwa sambamba Na alivyotenda, Mke kivyake Mume kivyake.. Usiwe mwepesi Wa kucoclude kwamba wote kanisani WAMEOKOKA, no kila Mtu anajijua mwenyewe.. So eneo la Roho ni Muhimu sana Kwa makuzi ya Mtu..Na kila Mtu kivyake. Mume kivyake Mke kivyake..

NAFSI: hiki ni kitengo Muhimu au Moyo wa mwanadamu, hapa ndipo Sasa Elimu, tabia, utashi, Na mengineyo yamejificha, hapa ndipo makaazi ya nyota ya Mtu, kupata au kipaji, uwezo Wa Mtu kusoma, kufanya biashara, kuhubiri, kuongea, uongozi, fedha Na fahari kadiri anavyoikuza potential yake.. Kila Mtu ana potential yake inategemea Na anavyo I maximize.. Katika familia Mume ana potential yake Mke, Watoto kila Mtu yake Na anahangaika nayo kivyake.. Mtu kuwa Na elimu, Mali, fedha, uongozi nk ni jinsi anavyoitumia karama(potential) yake Kwa bidii.. Ni eneo ambalo kila Mtu Mungu kamwekea lake.. (AKILI)

3: MWILI:- hii ni kama nyumba ya vitu vitatu nilivyoelezea, roho Na nafsi, Hukaa Kwenye nyumba, mwili.. Na mwili ni responsible Kwa kuzaa..
Tunasema roho+nafsi = Mtu, but roho+nafsi+mwili =binadamu..(take it from here).. Mtu akiondoka ndani ya mwili wanasema amekufa, Yaani nyumba haina wakaaji, mwili katika makuzi yake husafiri mamilioni ya nyuzi, Na Kwenye mapito yake hupitia mabadiliko ambayo watu hudhani ni magonjwa Na wakakimbilia tiba Za kemikali nzito ambazo huuharibu mwili zaidi.. Mwili hauna magonjwa Kwa asili yake Bali matatizo yote hutokea rohoni.. Roho ikiwa okay mwili uko okay.. Roho ni dereva wa mwili, Dereva mbovu nsikilizie GARI kama litadumu mwaka.. Ndio maana asili ya ubovu Wa dereva ni dhambi, ukitubu dhambi unakuwa okay..

Tukirudi Sasa Kwenye diagram letu, tunaomba watu wawili Mume X NA Mke Y kila Mtu ana roho yake, mwili wake Na nafsi yake, Sasa ukisoma*

Mwa2:24Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Unganiko la NDOA ni MWILI.. Mwili tu Na mambo ya mwilini sio roho wala nafsi ya Mtu .. Watu wengi sana hawaelewi hii kitu Na watu wangu wanaangamia Kwa kukosa maarifa.. Unapooa jua umeoa mwili sio Roho yake hivyo huwezi kuingilia privacy Za Imani yake.. Utaskia Mtu anafura sali huku sali huku, dini hii dini hii.. Ni makosa makubwa, NDOA nyingi zinavunjika kisa mmoja Wa wanandoa kaokoka, Kwani huyo Mume alioa Roho?? Yeye alioa mwili tena iko wazi biblia inasema Kwa mambo ya mwilini Mke Hana AMRI juu ya mwili wake Bali mumewe vilevile mume Hana AMRI juu ya mwili wake Bali mkewe sio AMRI juu ya Roho yake(Imani, dhehebu,Kanisa,dini nk) wala mwanandoa Hana AMRI juu ya nafsi ya mwenzake(fedha, Mali, mapato, elimu, uongozi n.k).. Hujaoa mbunge, umeoa Mke Ubunge Na mambo yanayofanana Na hayo ni yake.. Hujaoa degree, hujaoa Mali, umeoa Mke mengine ni yake, hela ni yake, Mali ni zake, elimu ni yake.. Wewe chako ni mwili .. Tena Mungu akasema wazi kanisaa zaaneni mkaongezeka .. So NDOA ni tendo la NDOA, Na maana ya tendo la NDOA ni Kuzaa Na kuongezeka Basi.. Kama NDOA ipo Na tendo la NDOA hilipo hapo hakuna NDOA hata nikiivunja sintasema navunja NDOA manake tokea hapo haikuwa NDOA .

Mwanaume akiwa darasa la Saba Na mwanamke PhD, maadam ana mwili Na mambo ya mwilini yako ok NDOA inaendelea, hapana mwanaume kuingilia mambo ya Mwanamke.. Kama mwanamke ni milionea Na mwanaume kiatu njaa, hapana shaka as far mambo ya mwilini yako Ok, hapana mwanaume kuingilia biashara au account Za mkewe, yeye anachojali apewe zake tendo la NDOA , wazae bas.. Hajaoa nafsi ameoa mwili tu..*

Nadhani Kitabu changu Cha Amani kitaelezea yote haya ili kufungua faham Za watu.. Ubarikiwe Kwa kusoma .. Kama utaelewa Basi Mungu akupe nguvu mpya..

AMEN

* *
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom