Ndoa bila watoto inawezekana?

isamilo1982

Member
Jan 17, 2012
55
5
Nimekuwa nikisikia malalamiko mengi juu yandoa zinazovunjika visa niving lakn hili la watoto linashika kasi,je kuna ukweli wowote?
 
unajua ndoa bila kuwa na mtot inawezekana pale tuu ambapo both parties kabla ya ndoa walikuwa wamekubaliana kuwa hawataki watoto na actually mwanaume akaenda kuhasiwa na mwanamke kufunga tubes zake....
 
Yes and No!

Yote inategemea na wahusika, watu wengine wanaoa/olewa ili wapate watoto hivyo wakikosekana wanahisi kama wanapunjika. Hiyo hupelekea kuwa na malalamiko ndani ya ndoa ,kitu ambacho husababisha wahusika kutoelewana. Wengine wanaingia kwenye ndoa ili wawe na wenzi wao kwa karibu na kihalali kwa mujibu wa dini zetu hivyo swala la kupata watoto au la sio la kuwakorofisha. Wakipata wanafurahi, wakikosa wanatafuta namna nyingine ya kujiridhisha kwa hilo.
 
unajua ndoa bila kuwa na mtot inawezekana pale tuu ambapo both parties kabla ya ndoa walikuwa wamekubaliana kuwa hawataki watoto na actually mwanaume akaenda kuhasiwa na mwanamke kufunga tubes zake....

Mmh ngum kumeza lakini.
 
unajua ndoa bila kuwa na mtot inawezekana pale tuu ambapo both parties kabla ya ndoa walikuwa wamekubaliana kuwa hawataki watoto na actually mwanaume akaenda kuhasiwa na mwanamke kufunga tubes zake....
Acha kupotosha ukweli. .
Sio kila ambae hana mtoto anapenda kutokua na mtoto au amefunga kizazi. Kama hufahamu wapo watu wasio na uwezo wa kuzaa, au wana matatizo yanayofanya iwe ngumu kwao kushika/sikisha mimba.
 
Inawezekana., Haiwezekani..

ITAWEZEKANA pale tu ambapo wanandoa watakuwa wamekubaliana kutokuwa na watoto kutokana na sababu zao binafsi.

HAIWEZEKANI endapo katika familia mmoja akawa anauhitaji mkubwa wa mtoto/watoto wakati mwenzake pengne hana uwezo wa kupata mtoto kwa wakati huo/maishani hapo lazima ndoa iwe hatarini..
 
Acha kupotosha ukweli. .
Sio kila ambae hana mtoto anapenda kutokua na mtoto au amefunga kizazi. Kama hufahamu wapo watu wasio na uwezo wa kuzaa, au wana matatizo yanayofanya iwe ngumu kwao kushika/sikisha mimba.

nilivyomuelewa mtoa mada ni kama wanandoa wanaweza kukaa bila watoto by choice na sio kwa sababau mmoja imetokea hawezi kuzaa....ndio maana nikajibu vile. wee kama imetokea mmoja wenu ndio sababisho la kutokupata mtoto basi kubali tuu yaishe bana. ndio ilishakula kwako
 
Ni kweli kukosekana kwa watoto huleta migogoro kwenye ndoa nyingi hasa zile ambazo imani yao ni ndogo. Wanashindwa kuamini kama watoto ni majaaliwa ya allah na kukosekana watoto pia ni mipango yake.
Kuwa na watoto haimaanishi kuwa ndoa yenu itakuwa na furaha muda wote, nyie wenyewe iruhusuni furaha na amani zitawale ndoa zenu hata kama hamna watoto.
 
Kupata watoto hayo ni majaliwa ya Mungu. Kama wote Mume na Mke wakikubali kuwa Mungu ndiye anayeweza kuwapa watoto basi wataishi kwa amani kabisa,pasipoa na shida yoyote ile.
 
Back
Top Bottom