nimeshuhudia mwenyewe kuna mwingine hadi leo akili zimemruka. wakati anaoa alikuwa na watoto 2 aliozaa na marehemu mkewe. watoto walikuwa wakisoma secondary kidato cha 4 na cha 1. alimuoa dada mmoja wa miaka 23 wakati huo mwaka 98 akiwa na elimu ya kidato cha nne akanza kwa kumsomesha kozi ya kingereza, A- level (QT) na baadae chuoni pale Tumaini ya Dar, alipomaliza akapata kazi na wamezaa mtoto mmoja, dada huyu kwa sasa anchukua masters UDSM. Visa vikaanza baada ya mama kupata aliyekuwa anamuona ni hitaji la moyo wake, mzee wa watu aliishia kupewa maneno ya kashfa kama mimi sio mzee mwenzio katafute wa kwako (mzee huyu kwa sasa ana karibu miaka 57, ndoa yenyewe ilikuwa ni ya kunilazimisha wewe na wazazi wangu n.k kinachomfanya achanganyikiwe mzee huyu ni kwamba nguvu yake yote alihamishia kwa dada huyu akasahau watoto wake kwa kushindwa kuwaendeleza kielimu sasa amekosa la kufanya baada ya kutengana na msaada uliopo ni watoto wake na ndugu tu.