Ndoa bila commitment ni bure kabisa

harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,889
1,346
Juzi tulikua kwenye msiba wa Mwalimu wangu mmoja.Wakati hili likiendelea nikawa nauliza kwamba ni nini hasa kilipelekea kifo cha Mwalimu huyu.
Nikaambiwa Hospitali Docta alisema kwamba jamaa alikua na stress ya muda mrefu stori ikawa hivi :

Huyu mwl. kabla hajaenda kusoma Canada na Marekani alikuwa ameoa halafu baada ya hapo wakapata mtoto mmoja sikuuliza kwamba ni wa kike au kiume kwani ningezidi kufukunyua mambo.Wakati akiwa nje alikua anatuma fedha za matumizi kama kawaida na baadae alituma fedha za kununua kiwanja na ramani ya nyumba pamoja na fedha za kujenga nyumba hiyo .Cha kumpa stress ni pale aliporudi kumwambia mkewe wahamie kwenye nyumba yao sasa mkewe akamkana na kumwambia hata mtoto sio wake.

Hapa ndio ukawa mwanzo wa ile stress ya yule mwl. wangu ikafanya moyo uwe mkubwa kupita kiasi ,ilivyochangiwa na kisukari pamoja na umri yule mwl. akatutoka .Mungu mpumzishe sehemu yenye mazingira mazuri upepo mwanana,Amen.


Mwangalie mpenzi wako je anakupa stress, na mtatizo mengine kama ndio atakuua.
 
pole kwake ila fudisho hapa sio kuhusiana na stress...fundisho hapa ni kwamba wanandoa wengi wanajidanganya sana pale wanapoenda nje masomoni na kumwacha mwenzie home peke yake akidhani kuwa atakuta mambo yapo shwari.

huo ni kutakakupata miujiza tuu ...married couples should never live in diferent cities come su come rain.....kama kweli ndoa yako unaivalue basi lazima ukubali kuwa kuna mmoja wenu lazima amufuate mwenzie!!!
 
Sio wanawake wote wanakua na akili fupi kama za huyo mwangine,wako wanaopenda maendeleo kwani kuanguka kwa mumeo ndio kwako kama mwanake atafikiria.....
 
pole kwake ila fudisho hapa sio kuhusiana na stress...fundisho hapa ni kwamba wanandoa wengi wanajidanganya sana pale wanapoenda nje masomoni na kumwacha mwenzie home peke yake akidhani kuwa atakuta mambo yapo shwari.

huo ni kutakakupata miujiza tuu ...married couples should never live in diferent cities come su come rain.....kama kweli ndoa yako unaivalue basi lazima ukubali kuwa kuna mmoja wenu lazima amufuate mwenzie!!!

Hilo nalo ni wazo pia! teteteteeeeeeeee, natamani ungeenda uchagani wewe
 
Mh?pole kwa ndugu ,jamaa na marafiki wa huyo marehemu........hivi bado wapo wanawake katika karne hii wasopenda maendeleo.Bila shaka huyo mke akapimwe kama harmashauri ya kichwa chake iko sawa..
 
Tena huyo mwanamke ni kutoka uchagani ile sehemu wanayosema ni kw wapalestina ni hatari tupu na mitihani.
 
nimeshuhudia mwenyewe kuna mwingine hadi leo akili zimemruka. wakati anaoa alikuwa na watoto 2 aliozaa na marehemu mkewe. watoto walikuwa wakisoma secondary kidato cha 4 na cha 1. alimuoa dada mmoja wa miaka 23 wakati huo mwaka 98 akiwa na elimu ya kidato cha nne akanza kwa kumsomesha kozi ya kingereza, A- level (QT) na baadae chuoni pale Tumaini ya Dar, alipomaliza akapata kazi na wamezaa mtoto mmoja, dada huyu kwa sasa anchukua masters UDSM. Visa vikaanza baada ya mama kupata aliyekuwa anamuona ni hitaji la moyo wake, mzee wa watu aliishia kupewa maneno ya kashfa kama mimi sio mzee mwenzio katafute wa kwako (mzee huyu kwa sasa ana karibu miaka 57, ndoa yenyewe ilikuwa ni ya kunilazimisha wewe na wazazi wangu n.k kinachomfanya achanganyikiwe mzee huyu ni kwamba nguvu yake yote alihamishia kwa dada huyu akasahau watoto wake kwa kushindwa kuwaendeleza kielimu sasa amekosa la kufanya baada ya kutengana na msaada uliopo ni watoto wake na ndugu tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom