kabwigwa
JF-Expert Member
- May 17, 2014
- 933
- 1,533
Wakuu habari zenu,Katika pita pita zangu masokoni nikakutana na hizi ndizi maarufu kama “ndizi za container” au “ndizi za umeme”.Kilichonistua ni maandalizi ya ndizi hizo mpaka kuiva.Mechanism nzima ni siku tatu mpaka nne ndizi inakua imeiva.Mechanism hii ndiyo iliyonifanya niandike uzi huu.Ndizi mbichi inapigwa dawa ya kukausha utomvu kisha inaingizwa kwenye container kisha inapigwa dawa ya kuiva haraka,kubadili rangi na dawa ya kufanya ndizi ikae muda mrefu bila kuharibika(rumor has it wanaweka dawa ya kuhifadhia maiti).Container linakua na heater ambayo husaidia ndizi kuiva,baada ya siku tatu ndizi inakua imeiva then inapoozwa na kupelekwa sokoni kuuzwa kwa wafanyabiashara na mlaji wa mwisho.
Wanasema “No research no right to speak “ mimi nimeongea ila ni aiomba serikali kupitia TBS na ofisi ya mkemia mkuu kufanya uchunguzi wa kina na kuujulisha umma kama Kuna madhara yoyote kuhusiana na ndizi hizi ambazo zimekua zikiuzwa kila kona Dar Es Salaam sijajua mikoa mingine kama zipo.Ndizi hizi ni aina ya Malindi ni kubwa nene na zina rangi nzuri ya kuvutia.
Nb:Sipo hapa kuharibu biashara za watu bali kutoa tahadhari kwa walaji wa ndizi hizo wanaokula wakiamini wanaimarisha afya kumbe wanaziharibu kwa kula kemikali.