Ndemla kupewa gari na kiongozi kutaivuruga timu

kucheza kwa "nidhamu" ni kucheza namna gani: kutopewa kadi? kutokuzozana na refa? kutokupoteza pasi? kukubali kuingizwa dakika za mwisho bila kukasirika? au kufanya nini ndio kucheza kwa nidhamu? acheni hizo!!
Zote hizo ni nidhamu kijana yupo benchi mda wote na bado anamoyo wa kupambana hana shida na mtu na ukiona imekuuma sana kamuibie umpe unaye mtaka wewe...zawadi imetoka roho inakuuma ... Zawadi haupangiwi wa kumpa ni yeyote unayejisikia
 
Na Mimi pia nina Zawadi yangu na ' Muhogo ' nataka nikupe kwa kuwa mmoja wa Wachangiaji wa Kutukuka hapa Jamvini je upo tayari nikutunuku / nikuzawadie?
thibitisha kwanza pasipo kuacha shaka kuwa mimi ndiye mchangiaji mkubwa kuwazidi wengine humu jamvini, ukishindwa kuthibitisha nitakupa muhogo wa jangombe uhangaike nao.
 
Mchezaji aliyetengeneza nafasi mbili na mchezaji aliyefunga magoli mawili nani anastahili kupewa zawadi? Ndemla alitokea kwenye bench akatengeneza nafasi mbili, Okwi alitokea bench pia akafunga magoli 2 na Asante Kwasi ni beki lakini amefunga goli. Okwi anaongoza ligi kwa ufungaji magoli na Ndemla ana....(...taka kuhamia Yanga, ha,ha)!!
 
Mchezaji aliyetengeneza nafasi mbili na mchezaji aliyefunga magoli mawili nani anastahili kupewa zawadi? Ndemla alitokea kwenye bench akatengeneza nafasi mbili na Okwi alitokea bench pia akafunga magoli 2. Okwi anaongoza ligi kwa ufungaji magoli na Ndemla ana....(...taka kuhamia Yanga, ha,ha)!!
Chagua na wewe ukampe huyo mwenye unataka sio kulalamika kama demu
 
Hans anamzuia Ndemla kwenda Yanga kwa swahiba wake Ajibu...tumempata Feisal Simba kuweni na amani
 
Mchezaji aliyetengeneza nafasi mbili na mchezaji aliyefunga magoli mawili nani anastahili kupewa zawadi? Ndemla alitokea kwenye bench akatengeneza nafasi mbili, Okwi alitokea bench pia akafunga magoli 2 na Asante Kwasi ni beki lakini amefunga goli. Okwi anaongoza ligi kwa ufungaji magoli na Ndemla ana....(...taka kuhamia Yanga, ha,ha)!!
Tatizo unachangia bila kusikia alichokiongea hans, Nakushauli tafuta clip au ingia kwa salehejembe usome vizuri, labda unaweza kuelewa, anyway. Kwenye mpira hakujawahi kuwa na usawa, ndio maana hata mishahara hawalingani ukitaka hata zawadi zitolewe kwa usawa utanishangaza pia, suala la hans kugawa zawadi alilitangaza tokea msimu uliopita so sijajua ni kigezo gani ulichotumia kujiaminisha kuwa ni performance ya jana tu.
 
hakuchaguliwa kwa ajili ya jana tu .anastahili huyo dogo na sio wa kwanza kupewa hata shabalala alipewa na singano kipindi kile
 
Katika mchezo unaohusisha watu wengi kuufanikisha huwezi kutoa zawadi kwa mchezaji mmoja pekee. Kitendo hicho kinaweza kutendwa na watu binafsi au taasisi nyingine lakini sio kiongozi wa timu. Kiongozi wa aina hii anawagawa na kuwavunja moyo wachezaji wengine kijiiinga kabisa.

Ndemla kacheza na kupeana pasi na wenzake kwanini kiongozi ampe mchezaji mmoja zawadi ya gari na kuwaacha wengine wote hata akina Kichuya waliofunga magoli?
Acha wivu wewe....
 
Katika mchezo unaohusisha watu wengi kuufanikisha huwezi kutoa zawadi kwa mchezaji mmoja pekee. Kitendo hicho kinaweza kutendwa na watu binafsi au taasisi nyingine lakini sio kiongozi wa timu. Kiongozi wa aina hii anawagawa na kuwavunja moyo wachezaji wengine kijiiinga kabisa.

Ndemla kacheza na kupeana pasi na wenzake kwanini kiongozi ampe mchezaji mmoja zawadi ya gari na kuwaacha wengine wote hata akina Kichuya waliofunga magoli?
Ndiyo maaana mpira wa tanzania hauendelei. Unakuja n.a. hoja ya kinafiki. Kati yako n.a. huyo kiongozi nani anataka kuleta utofauti kwenye timu?.
Kutoa zawadi kwa mchezaji moja aina maana ya kuwavuruga wachezaji wengine. Kama hujitumi ndiyo utaona kama ni upendeleo kwa aliyepewa.
Watanzania tuaecheni stori au habari kama izi tuwapongeze pale panapostaili. Pia tuwatie moyo wachezaji ili wapate morali ya kushinda n.a. kuendeleza soka safi nchini kwetu.
 
Zawadi inaweza kuleta matokeo hasi au chanya. Kama haitaratibiwa vizuri zawadi inaweza kuwa destructive, ndio maana zawadi zote zinawekewa vigezo vya wazi vya kuipata au kuikosa. Huwezi kukurupuka from no where na kumpa binti yako zawadi eti yeye ndiye kaleta kibiriti cha kuwashia moto jikoni na kumuacha yule aliyepika chakula na kutenga mezani. Ukifanya hivyo familia itakusingizia mabaya kwa huyo binti yako uliyempa zawadi kwa sababu za kipumbavu kabisa.

Walioleta furaha ya wazi kwenye mechi ile ya Simba na Singida ni Kichuya aliyejipinda dakika ya 3 tu ya mchezo na kufunga bao safi kabisa, akifuatiwa na Okwi na Kwasi, kila mtu alishangalia kwa raha hata yule asiyekuweko uwanjani. Mfano, kama Ndemla angecheza vizuri kama alivyoona kiongozi wake wa Simba lakini Simba ikafungwa au kutoa sare na Singida bado hiyo zawadi ya gari angepewa Ndemla? Ni ujiinga tu. Mbona Mapinduzi cup hakutoa zawadi, hakuna mchezaji aliyecheza vizuri mechi zote zile?
unatumia muda mrefu kuandika shit..
 
Nidhamu ni jambo la msingi sana, ukiangalia mapinduzi cup nidhamu ilikosekana kwa baadhi ya wachezaji. Vigezo na masharti vimezingatiwa
 
Ubaguzi...!
Kwani hawalipwi malipo ya kwenye mikataba yao?
Hiyo ni motisha ili wachezaji waongeze bidii na kujituma.
Pia Ndemla ndio mchezaji pekee ambaye hakuwa na gari pale Timu Msimbazi.
Sasa ataweza kuwahi mazoezini sawa na wenzake.
 
na mimi Nampa offer Ndemla akipewa tuu gari namwekea mafuta ya elfu 50
 
Back
Top Bottom