Ndemla kupewa gari na kiongozi kutaivuruga timu

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,307
12,602
Katika mchezo unaohusisha watu wengi kuufanikisha huwezi kutoa zawadi kwa mchezaji mmoja pekee. Kitendo hicho kinaweza kutendwa na watu binafsi au taasisi nyingine lakini sio kiongozi wa timu. Kiongozi wa aina hii anawagawa na kuwavunja moyo wachezaji wengine kijiiinga kabisa.

Ndemla kacheza na kupeana pasi na wenzake kwanini kiongozi ampe mchezaji mmoja zawadi ya gari na kuwaacha wengine wote hata akina Kichuya waliofunga magoli?
 
kawape na wewe walio funga magoli, kiongozi kafurahi maana msimbazi bundi alisha tua pale kwa matokeo mabovu.
 
Katika mchezo unaohusisha watu wengi kuufanikisha huwezi kutoa zawadi kwa mchezaji mmoja pekee. Kitendo hicho kinaweza kutendwa na watu binafsi au taasisi nyingine lakini sio kiongozi wa timu. Kiongozi wa aina hii anawagawa na kuwafunja moyo wachezaji wengi kijiiinga kabisa.

Ndemla kacheza na kupeana pasi na wenzake kwanini kiongozi ampe mchezaji mmoja zawadi ya gari na kuwaacha wengine wote hata akina Kichuya waliofunga magoli?
Sehemu ya usajiri wake,Dogo si tuliambiwa a nataka kutimkia ulaya?jiongeze
 
uongozi usio na akili! hajajua impact! better akatoa bonus for the team
Matokeo ya kuzoazoa ovyo viongozi kutokana na uwezo wao kifedha. Wachezaji wengine wanaweza wasimpe Ndemla ushirikiano uwanjani. Hata kama zawadi hiyo inatolewa kwa malengo mengine ambayo hayako wazi bado, basi itolewe kisayansi bila kuwavuruga wachezaji wengine kwenye club.
 
kwani ofisini anapochaguliwa mfanyakazi bora wa mwenzi na kupewa zawadi kwani hao wengine hawafanyi kazi.
Kuna utaratibu shirikishi wa kiofisi wa kumpata mfanyakazi bora usioacha mashaka na manung'uniko kwa wafanyakazi wengine, sio kama Hanspope alivyofanya. Hata huko ofisini kama atapewa ufanyakazi bora mtu ambae sio wafanyakazi watasema na kunong'ona.
 
Soka ni ajira iyo inawafanya wachezaji wengine wajitume zaidi,hakuna upendeleo hapo
Lazima vigezo vya kupewa zawadi ya gari na uongozi wa simba vitangazwe na vifahamike kwa wachezaji wote kabla.
 
kila mtu ana haki ya kumpa amtakaye zawadi ndugu yangu. kugawanya team ni akili za kimaskini tu ndo zinaweza dhania hivyo. mimi nina kitu kizuri nataka nimpe kichuya... niogope eti kwa kumpa kichuya nitagawa team kwa hiyo niwape team nzima. swali je kavunja kanuni au taratibu za kiuongozi au kuendesha mpira? no. tusianze sasa kuweka mawazo ya kipuuzi eti kugawa team. hata katika uumbaji kuna ambao wana viuongo vyote na wengine wana upungufu lakini hatuwezi sema kuna aliye bora kuliko mwenzie mbele ya Mungu. zote hizo ni zawadi. sasa mpumbavu anaweza kusema eti kwa kuwa yeye ana ulemavu basi haoni sababu ya kumtukuza Mungu au tayari anakosa ushirikiano na walio wazima.zote ni zawadi tu.
 
Pg.24b.JPG

Wachezaji Haji Mwinyi (kushoto) na Juma Mahadhi wakipatana bei na waendesha bodaboda wakati walipowasili katika bandari ya Dar es Salaam

Ndemla%2BBreaking%2BNews.jpg

Mohamed-Hussein-Tshabalala-Gari-Jipya-Simba-Bongosoka.jpg

TANZANI+ONE+BLOG+NGASSA.JPG
 
Unataka kiongozi awape gari timu nzima? Msuva alishawahi kupewa kiroba cha mchele mbeya. Relax kijana, life is too hard to complicate...

Back
Top Bottom