John W. Mlacha
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 3,504
- 1,342
Utaratibu huo haupo Tanzania, nchi ya kibabe hii. Wanajeshi walijua masaa saba kabla kwamba mabomu ya gongo la mboto yangelipuka lakini wakahamisha familia zao bila kuwatangazia wananchi kuondoka maeneo ya karibu. Wakawaacha hadi wafe. Hili li nchi yaani linaongozwa kihuni wee acha tu. Raia hawana say kwenye nchi yao. Sasa wanaungurumisha tu Madege na huku wanajua kwamba tupo kwenye mgogoro na Malawi. Wanataka sisi tuhisi tu kwamba ni salama, kama tumevamiwa je?Si suala la ugeni bali kujua nini kinafanyika. Kama wana mazoezi wangetangaza kabla ili tujuwe, haya ya kushituana wakati mnajuwa tulishawahi lipukiwa kule mbagala na gongolamboto hayafai..
hayo mazoezi ya kijeshi kwa ajili ya ckukuu ya muungano april 26, wala hamna kitu kingine chochote
Kama wana mazoezi wangetangaza kabla ili tujuwe, haya ya kushituana wakati mnajuwa tulishawahi lipukiwa kule mbagala na gongolamboto hayafai..
kuna maadhimisho ya muungano i think tarehe 26 april
Mapori yote hayo hawajayaonafanyeni mazoezi ya kurusha ndege mjini alafu yatokee yakutokea tuanze kumtafuta mchawi nani.
jamani kuna ndege zinapita kwa kasi sana hapa dar. zinakwenda kwa spidi kiasi milio.yake inastua sana. kuna nini?
Utaratibu huo haupo Tanzania, nchi ya kibabe hii. Wanajeshi walijua masaa saba kabla kwamba mabomu ya gongo la mboto yangelipuka lakini wakahamisha familia zao bila kuwatangazia wananchi kuondoka maeneo ya karibu. Wakawaacha hadi wafe. Hili li nchi yaani linaongozwa kihuni wee acha tu. Raia hawana say kwenye nchi yao. Sasa wanaungurumisha tu Madege na huku wanajua kwamba tupo kwenye mgogoro na Malawi. Wanataka sisi tuhisi tu kwamba ni salama, kama tumevamiwa je?
wanajiandaa na sikukuu ya muungano tarehe 26,,,kutakuwa na "air show".....
Wewe unaongelea milipuko ya wapi? Mimi nasema ya gongo la mboto! Kama una ushahidi wa mwanajeshi aliyekufa au familia ya mwanajeshi iliyopata hata kovu tu kutokana na milipuko ya gongo la mboto ulete hapa jamvini.aiseee! Walikuwa na taarifa saa 7 kabla ya mlipuko kumbe? Sasa wale wanajeshi waliokufa kwenye milipuko hawakuwa informed au walijitolea kufa? Na mbna mali nyingne ziliharibika jeshin mkuu? Au walizitoa sadaka?
Kwahiyo mkuu unathibitishia jamvi hapa hakuna askari yoyote aliepata madhara kwenye ile kadhia ya gongo la mboto? Kama taarifa walikuwa nazo 7hrs before si kulikuwa na uwezekano wa kufanya evacuation within that time frame? Pia wangeweza wakahamishia hyo milipuko mbali ili kupunguza ukubwa wake sasa hapa unataka kutuambia jeshi letu haliko makini au?Wewe unaongelea milipuko ya wapi? Mimi nasema ya gongo la mboto! Kama una ushahidi wa mwanajeshi aliyekufa au familia ya mwanajeshi iliyopata hata kovu tu kutokana na milipuko ya gongo la mboto ulete hapa jamvini.
Kuhusu mali za jeshi, ni kichaa tu ataanza kuhama na mali wakati wa vita. Nafikiri uhai ndiyo huwa ni first priority kuliko kingine chochote.
Wamehamisha familia zo tangu saa saba, na mabomu yameanza kulipuka saa mbili usiku. Hivi wangeamua kupita na kipaza sauti kule kuwatangazia wananchi waondoke maeneo ya karibu na gongo la mboto si wangeokoa maisha ya watu wengi tu? Au wangeleta magari ya jeshi na kuwabeba watu watu kuondoka eneo la hatari kama walivyofanya kuwabeba kuwarudisha kwenye maeneo yao, si wangekuwa wamesaidia sana?Kwahiyo mkuu unathibitishia jamvi hapa hakuna askari yoyote aliepata madhara kwenye ile kadhia ya gongo la mboto? Kama taarifa walikuwa nazo 7hrs before si kulikuwa na uwezekano wa kufanya evacuation within that time frame? Pia wangeweza wakahamishia hyo milipuko mbali ili kupunguza ukubwa wake sasa hapa unataka kutuambia jeshi letu haliko makini au?
Achana nao hawa ni wasiopenda maendeleo. Mi nakuhakikishia watu wa aina hii hata wasikie chadema wanefanya ovu gani basi watalitetea na kufanya liwe jema, lkn CCM wafanye jema lolote basi wataliponda tu. hawana kheri hawa..
btw mi mwenyewe tangu majuzi (kama wiki) naona izi ndege, lakini nazikuta ni rangi ya njano mpaka najiulize za wapi zile??? Nikafikiri mazoezi ya kujiandaa na malawi...