Ndege yaanguka ziwa Manyara

Kuna viboko wengi sna hapo awe waangalifu.

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
Nimepokea taarifa hizi kutoka huko Arusha lakini sina uhakika, na kwa kuwa hapa ndo kwao na uhakika, kama kuna mtu ana data kamili atujuze.
 
Duh, nilifikiri mwandishi amekosea tu kuandika, kumbe kweli kuna shirika la ndege linaitwa tanzanair? Sijawahi kulisikia.
Wee na akina sie ndio Omujubi ametuambia ni lile kundi la watu wanaofikiria kidogo au hatupotezo muda kabisa kufikiria, sasa tutawezaje kufikiria habari za tanzaniair, zanair, eagle air n.k? Wacha tusikilizie new Challenge au Sumri ndio saizi yetu kaka.
 
huyo rubani ni jinias
Naam, bila shaka. Hii ni fani ambayo haitaki kuingiliwa. Kuna Rubani mmoja wa Air Tanzania alitua kwenye majani Oman miaka ile ya Air Tanzania ya kweli baada ya tairi kugoma kufunguk, na abiria wote walisalimika bila majeruhi. Hao ni marubani ambao walikuwa trained jeshi, Entebbe then Russia au Cuba kabla hajapewa ndege. Nashangaa siku hizi eti kuna vyuo vya urubani hadi 'Tabata Magengeni' na vinaachwa tu. tutarajie maafa makubwa huko tuendako?
 
Nimepokea taarifa hizi kutoka huko arusha lakini sina uhakika, na kwa kuwa hapa ndo kwao na uhakika, kama kuna mtu ana data kamili atujuze.

kweli according to Lau Masha

Lawrence (Lau) Masha ‏@laumasha3h
A plane has just crashed into Lake Manyara with 12 passengers on board including my Partner P. Ishengoma , they need help now.


Lawrence (Lau) Masha ‏@laumasha
2h

The plane has been cited , rescue teams are approaching. Ishengoma is injured but alive. Thank you all for your prayers and assistance.
 

Imetua katika Ziwa kwa dharura badala yake ingeanguka nchi kavu hakungekuwa na kiumbe hai. Hongera kwake rubani maana kutua ziwani nako ni tukio la kutisha sana.
 
Nawapa pole waliopata hio ajali. Lakini ufike wakati sasa ufanyike uchunguzi wa kina kujua chanzo cha hizi ajali za ndege hasa ukanda huo manake kuna nyingine ilianguka recently

Na hilo ndio jambo la msingi mkuu, nimeshuhudia hivi karibuni ajali ya ndege iliyotokea Marekani 14 August 2013, UPS A300F4-622R; Birmingham. Uchunguzi wa hiyo ajali ulienda mbali hadi jinsi nagazi au madaraja yanavyoathiri mawasiliano baina ya wafanyakazi na kuona mchanganyiko wa wafanyakazi kutoka marekani na mataifa mengine.

Hii yote ilikua kuona kwamba huenda mtu wa chini akawa na habari muhimu ambayo ingeweza kuepusha ajali, lakini jinsi anavyoitoa inategemea anamwambia nani na yuko daraja gani, ikaonekana ajali ingeweza kuzuiliwa kama mtoa taarifa kwa rubani angetoa maelezo ya hali halisi kwa rubani badala ya kutumia lugha ya upole na kuogopa kumweleza ukweli kwamba aongeze speed ya ndege ili iweze kutua salama.

Naunga mkono hoja yako kwamba utafiti wa hizi ajali zinazoendelea kutokea hapa kwetu ufanyike kwa ufanisi na lengo iwe kupunguza au kuzuia matatizo kama hayo kutokea mbeleni.
 
Tukio lolote linaripotiwa jomba!!!wacha kulalamika kitabaka!
 
Tanapa wamefanikisha uokoaji wa ndege husika ndani ya ziwa manayara wahusika baada ya tatzo waliomba msaada tanapa kikosi cha uokoaji cha tanapa kikawahi na kuwaokoa abiria wote wakiwa ziwan ambapo kuna vboko na mamba mungu mkubwa tanapa wamesaidia abiria wote wapo salama
 
usalama wa anga hasa kwa ndege ndogo ni mdogo sana hapa nchini.... ndege ndogo nyingi ukifuatilia hawana hata engineering department au zinamilikiwa binafsi tu!!! sijui ni shirika gani hili lakini kwa route iyo nadhan ni auric air!!!
 
 
Air Tanzania, sikio la kufa! Ni hujuma au uchawi, hili shirika mbona linateketea kwa kasi ya kutisha sana?

Wewe mburula hiyo ni ndege ya kampuni ya TANZANAIR na sio Air Tanzania!!
 
kikosi cha uokoaji cha shirika la TANAPA wamesaidia uokoaji abiria wote wapo salama...MASHRKA KAMA HAYA NI MFANO WA KUIGWA HAYANA URASMU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…