Ndege yaachia njia Uwanja wa Ndege Bukoba

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,536
Watu kadhaa wamenusurika baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Auric Air waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Uwanja wa Ndege wa Manispaa Bukoba ilipokuwa ikitua na rubani kupoteza uelekeo

Ndege hiyo ilikuwa imeshatua lakini ikashindwa kusimama na kupitiliza hadi mwisho wa uwanja ndipo ilipogota kwenye mtaro.
f18b4346-6d8c-49e5-8096-c79cf5b51868.jpg
602a3cf7-417d-410e-80ca-3f1db8d7574f.jpg

============
UPDATES:

Imedaiwa ni baada ya ndege hiyo kupata pancha tairi ya nyuma ya upande wa kulia ilipokuwa inatua.

Na inasemekana ni kwa umahiri wa Rubani ameweza kui-control kama inavyoonekana pichani ikiwa pembezoni mwa Uwanja.
 
Ha ha haaa! kafara kufeli inachekesha.....tushukuru Mungua kama hakuna aliyepoteza maisha.
 
Miaka ya nyuma kuna ndege ya jeshi iliwahi kusababisha maafa hapo Bukoba kwa style hiyohiyo,mi nilidhani runway imerefushwa ,nadhani tatizo pia ni ufupi wa runway
 
Kafara limegoma, wamekosea masharti
Mkuu Mshana heshima mbele..kila ajali inayotokea lazima ihusishwe na ushetani?kuna masuala ya uzembe wa pilot,mechanical problems etc..its better u get people to focus on the positive side..hamna haja ya kuwaingiza watu kwenye uoga
 
Mshana kaniudhi, huwa namwamini, sasa amanitia majaribuni with his credibility, ruining his long built credibility!
 
Mkuu Mshana heshima mbele..kila ajali inayotokea lazima ihusishwe na ushetani?kuna masuala ya uzembe wa pilot,mechanical problems etc..its better u get people to focus on the positive side..hamna haja ya kuwaingiza watu kwenye uoga
Uko sahihi kabisa lakini kila mmoja ana uhuru wa kuja na speculations tofauti
Kwa mtazamo wangu ni vitu kama hivi na wewe pia huo ni mtazamo wako na siwezi kupingana nawe na mambo ya giza hayana ithibati za kisayansi lakini yapo
 
Watu kadhaa wamenusurika baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Auric Air waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Uwanja wa Ndege wa Manispaa Bukoba ilipokuwa ikitua na rubani kupoteza uelekeo

Ndege hiyo ilikuwa imeshatua lakini ikashindwa kusimama na kupitiliza hadi mwisho wa uwanja ndipo ilipogota kwenye mtaro.
View attachment 343784 View attachment 343785
Bukoba airport>>.111 hii ni mara ya pili..mara ya kwanza ilikuwa miaka kadhaa ndege ilposhindwa kusimama na kuparamia nyumba ya Dr. kairuki iliyopo mwishoni pembezoni mwa uwanja... natoa pole kwa wahanga.
 
Uko sahihi kabisa lakini kila mmoja ana uhuru wa kuja na speculations tofauti
Kwa mtazamo wangu ni vitu kama hivi na wewe pia huo ni mtazamo wako na siwezi kupingana nawe
Mshana mhhh!!!!!!!! Tunategemea watu wenye scientific mind watawale humu, you are, I guess, one of them!
 
Mshana mhhh!!!!!!!! Tunategemea watu wenye scientific mind watawale humu, you are, I guess, one of them!
Nimeileta kama changamoto ya upande mwingine
Lakini pia kuna keypoints kama
-Ubovu wa uwanja
-umahiri wa pilot
-ubora wa chombo
-system failure
-hali ya hewa nk nk
Vyovyote viwavyo kuna sababu kwenye kila ajali
 
Perfect! Nilitegemea hiyo toka kwako- scientific reasoning!
 
Back
Top Bottom