Sijasema kuwa na Bombarder ni kosa... hoja yangu ni kwamba, unavyokuwa na limited resource, unatakiwa ku-invest kule ambako kutatoa higher return ili mapato yake yawe reinvested kwenye maeneo mengine!Mkuu hicho alichosema waziri mkuu wa Singapore ndio mada yangu ijayo. Yaani nina wazo hilo hilo. Kwa Bongo hakuna cha kutufaa zaidi ya kilimo. Tutapata chakula na hakuna zao la shamba lisilouzika nje ya nchi.
Nafikiria tujenge viwanda vya kufanyia processing mazao ya shamba na kuhifadhi mazao. Tuna water bodies nyingi. Tusitegemee mvua. Tufanye irrigation hasa hii ya water dripping. Tulime mahindi watu wale ugali na mwingine tuuze nje.
Ila ishu zinakuja serikali haziwi na mashamba. Ila ni kawaida serikali kuwa na mashirika ya ndege. Hapo pakinyooka nani wa kusimamia mashamba bila ya kurudi kwenye vijiji vya ujamaa wala kuwapa ardhi makaburu mimi naona kilimo ndio mkombozi wetu.
Bombardier sio kosa hata hivyo . Tutakuwa nchi gani hatuna ndege? Togo au Burkina Faso? Na usidharau unafikiri Ethiopian airline ni shirika la watalii. Uchumi wa Ethiopia bila ya Ethiopian airline si watakufa njaa tena kama miaka ile?
Kila siku iendayo kwa Mungu Ethiopian airline wanarusha ndege kutoka DC Washington kwenda Addis na mara nyingi inajaa. Kuna wanigeria, waghana na wawest wengine inabidi wapelekwe Addis kabla ya kwenda kwao. Tizama huu mtandao wa ndege unafikiri kwa siku wanaingiza ngapi?
Mbuyu ulianza kama mchicha.
.
Kinyume chake, sioni ni namna gani uwekezaji kwenye ndege unaweza kutoa return ya maana inayoweza kuwekezwa kwenye sekta zingine! Zaidi ya pride, kwamba ikiwa hata Rwanda nchi ndogo wana ndege, kwanini na sisi tusiwe nazo!!! Hiki ndicho kinatuponza badala ya kuangalia commercial and economic viability!
Kampuni nyingi za ndege Afrika ni loss making ukiacha kampuni chache sana kama Ethiopia Airline!! Sasa kwanini tuingize mtaji wetu mdogo kwenye risky investment wakati tuna alternatives lukuki?!
Hivi ni raia kutoka nchi gani anayeshindwa kuja Tanzania kwa sababu tu ATCL hawana ndege?! Hivi ni nani dunia hii anashindwa kwenda kutembelea Serengeti National Park kwavile tu ATCL hawana ndege?! Ni lini na wapi over the past 10 years nchi ilisimama shughuli zake kwa sababu tu ATCL hawana ndege?!
Yote hayo kwangu yasingekuwa muhimu endapo tu kungekuwa na possibility ya kutoa high return ambayo itakuwa reinvested! Lakini, sitarajii hiyo high return?!
So, si kwamba hakuna umuhimu moja kwa moja, lakini kwa sasa sioni ulazima huo wakati hizo billioni kadhaa zingeweza kuwekekzwa kwingine na kutoa return kubwa zaidi ambayo pengine ndo ingekuja kununua hizo ndege in the future!!!
Kuhusu Ethiopian Airline, wala usijaribu kujilinganisha nayo!!! Hivi hujiulizi ikiwa throughout Africa kuna mashirika ya ndege lakini kila wakati ni Ethiopia Airline peke yake ndiyo inatolewa mfano?! Ukiacha Ethiopia Airline labda na South African Airways pamoja na Egypt Air na kwa mbali inafuata Kenya Airways!
Ni shirika lipi kati ya hayo ambayo ATCL wanaweza ku-compete nao? Kwanini tusikusanye kwanza nguvu ili tuingie wakati tupo full prepared?!