Ndege ya Rais yazuiliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndege ya Rais yazuiliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Jan 25, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  • IKO NJE KWENYE MATENGENEZO, SERIKALI YAKWAMA KUILIPIA

  na Mwandishi wetu


  UKATA unaoikabili serikali, umesababisha kukwama kuilipia ndege maalumu ya Rais, inayofanyiwa matengenezo nje ya nchi, Tanzania Daima Jumatano limebaini. Kutokuwepo kwa ndege hiyo, kumesababisha Rais Jakaya Kikwete na ujumbe wake wa zaidi ya watu 14, ulioondoka nchini jana kwenda Davous, nchini Sweden, kuhudhuria mkutano wa dunia wa mambo ya uchumi, kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la Qatal. Habari ambazo gazeti hili imezipata, zilisema kuwa ndege ya Rais mahususi kwa ajili ya safari za aina hiyo imezuliwa nje ya nchi baada ya serikali kukwama kulipia gharama za matengenezo yake.

  Kutokuwepo kwa ndege hiyo iliyonunuliwa kwa sh bilioni 40 na kuibua mzozo mkubwa wakati serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kunaelezwa kuwa kumeongeza gharama kubwa kwa ziara za Rais Kikwete ambaye amekuwa akitumia ndege za kawaida kwenye safari zake nje ya nchi. Habari kutoka ndani ya msafara wa Rais, zilisema kuwa zaidi ya sh milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya kugharimia ziara hiyo ya siku nne nchini Sweeden. Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinatumika ndani ya siku nne kuanzia Januari 25 hadi 29 ambapo Rais na ujumbe wake watakuwa wanahudhuria mkutano huo ambao wataalamu wa uchumi, wameuelezea kwamba hauna tija kwa taifa. Inaelezwa kuwa Rais Kikwete ameshahudhuria mikutano hiyo mara nyingi, lakini hakuna faida inayopatikana kitaifa baada ya serikali kushiriki katika mikutano hiyo inayoratibiwa na Wizara ya Fedha na Uchumi. “Jana Rais Kikwete ameondoka, yeye na msafara wake watatumia zaidi ya sh milioni 300 kwa siku nne tu, atakazohudhuria mkutano wa uchumi, Davos nchini Sweeden. Angekuwa na ndege yake, gharama zingepungua,” kilisema chanzo chetu cha habari. Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa kwa takriban miezi miwili sasa, ndege hiyo iko nje ya nchi ikifanyiwa matengenezo kutokana na kuwa na hitilafu.

  Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Ndege za Serikali, Keenan Mhaiki, alikiri kuwa ndege hiyo iko nje kwa matengenezo, lakini alisema ni matengenezo ya kawaida yaliyomo ndani ya ratiba ya ndege hiyo ya kisasa. “Ndege ya Rais iko kwenye matengenezo. Sio kwamba ni mbovu, hapana ni matengenezo ya kawaida ambayo yanachukua zaidi ya mwezi mmoja,” alisema Mhaiki. Alipoulizwa kwamba ndege hiyo iko nje kwa muda mrefu baada ya serikali kukwama kulipa deni la matengezo yake, Mhaiki alikana na kuongeza kuwa hana taarifa za serikali kushindwa kulipia deni la matengenezo. “Kwanza nikwambie tu kuwa ndege hiyo sio mbovu, lakini pia sisi hatuhusiki na malipo ya matengenezo yake, kwa kawaida ikishakuwa tayari tunapewa taarifa nasi tunaandaa utaratibu wa kuifuata,” alisema.

  Alipoulizwa kuhusiana na serikali kukwama kuikomboa ndege ya Rais, Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu, alijibu kwa kifupi kwamba hawezi kuulizwa swali hili kwenye simu. Alipotakiwa kufuatwa ofisini ili kutoa ufafanuzi, Waziri Ndundu alikuja juu na kusema yuko jimboni, hivyo waulizwe wasaidizi wake walioko Dar es Salaam. “Mimi niko jimboni, pale ofisini kuna watendaji wa wizara. Mimi siyo wizara, nenda pale utapata majibu yote,” alisema Waziri Ndundu
   
 2. M

  Makunga JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 772
  Likes Received: 497
  Trophy Points: 80
  mmh,kweli tuna Rahisi! Mil300 kwa siku 4!! Inashangaza sn,tungekuwa na rais labda angekuwa anatuonea huruma.
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tsh 300,000,000/4 days na hakuna faida yoyote?? Nashindwa kuelewa nimchukulie hatuagani huyu rais wa tz
   
 4. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Quatar watulipe hata ndege ya Rais kwa wale wanyama waliodabua kupitia KIA. sijui kesi ikoje maake Rais anahusika!!
   
 5. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,348
  Likes Received: 6,698
  Trophy Points: 280
  Hii ndiyo Tanzania bana!
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  "Hata watu wakila nyasi, ndege ya raisi lazima inunuliwe!"- Basil P. Mramba :A S embarassed:
   
 7. Caelish Lishman

  Caelish Lishman Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  mkwereeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee:lol:
   
 8. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,808
  Likes Received: 1,123
  Trophy Points: 280
  Ndio maana siku hizi rahis wetu hasafiri, kumbe ndege iko matengenezoni kwa miezi minne. Dah ndege imesababisha rahis asiende mara kwa mara kutuombea chakula nje mwishowe garama za maisha zimepanda. Poor Tanzania.
   
 9. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Vitu Kama hivi uniharibia siku yangu. ..... Ngoja nikapate konyagi kidogo kurudisha mood....
   
 10. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,583
  Trophy Points: 280
  Ipigwe mnada huko huko udhia wishe.
   
 11. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Na hiyo ndege ikae huko huko isirudi.............aghhhhhhhhhhhhrrr
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,464
  Likes Received: 5,707
  Trophy Points: 280
  Nini raisi
  airbus la atcl nalo si limezuiliwa wacheni wafu wazike wafu wao
   
 13. Ground Zero

  Ground Zero JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Is Davos in Sweden? I doubt the accuracy of the information!
   
 14. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mgodi wa nzega unatoa dhahabu ya bil 130 kila wiki tunashindwa hata kutoa machungu ya kula nyasi?
  iptl tunawanunulia mafuta mazito ta mil 120 kila siku tunashindwa kulipa kweli?

  r.i.p ccm.
   
 15. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wacha watu waendelee kurudisha kadi za CCM,kwa staili hii.
   
 16. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Waandishi wetu wa habari noma, kwanza sio
  Davous ni Davos na muhimu zaidi haipo Sweden ipo Switzerland. Yaani mambo ya kugoogle kwa dakika mbili yanawashinda.
   
 17. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  insane!
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hakuna shirika la ndege hapa duniani linaloitwa QATAL,wala hakuna waziri anayeitwa NDUNDU.
  Halafu hii habari ni ya kiumbea kwa sababu hili gazeti halijui hiyo ndege iko nchi gani zaidi ya kuzusha nje ya nchi.gazeti makini haliwezi kuandika udaku kama lilivofanya hili.wajinga ndio waliwao.
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kama ulikuwepo mkuu,hawa jamaa wababaishaji kweli,hata shirika la ndege eti wanaandika QATAL,Waziri NDUNDU mara nje ya nchi,afazali nawe umeliona hilo...Ndo matatizo ya copy and paste kaka.
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,464
  Likes Received: 5,707
  Trophy Points: 280
  unaweza pewa ka deti na mwanamke akakwambia yuko sinza mapambano kwa kuwa ufahamu mapambano sinza yenyewe ukaijua basi inatosha kuuliza wapi ilipo na ukaenda kumwona aanaekusubiri
  naona akuna kilichoharibika swala tumejua iko huko na tunashukuru kwa taarifa kumbe mnajua ilipo mmekaa kimya mnakula hela zetu

  mbaya zaidi naomba niwaombe radhi kuna ma engineer wa ndege wako kule zaidi ya mwezi sasa wanakula perdiem huku aijulikani fedha zinatolewa lini hii ni dhambi iliyoiua atcl kwa kupeleka ma engineer zaidi ya wawili wakilipwa doller 350 kwa siku huku wakijua ndege ni mbovu aiishi leo mwisho wasiku ndege imebaki jamaa wamerudi kuchota fedha zzao imagine miezi mitatu doller 350kwa siku hii si laana mnategemea nini
  ??
   
Loading...