Ndege ya Jeshi yaanguka na kuwaka moto uwanja wa ndege Mwanza, rubani anusurika!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Taarifa kutoka Mwanza Airport ni kuwa kuna ndege ya Jeshi imelipuka na kuteketea.

Rubani wa ndege hii, ndg Peter Augustino kafanikiwa kuruka kwa parachuti na kunusurika ingawa inadaiwa kavunjika mguu na kukimbizwa hospitali.

Taarifa zaidi zinafuata

attachment.php

attachment.php


=======
UPDATES:
=======
Ni kweli imeanguka na kulipuka moto.

Ni ndege ya Jeshi ambayo hubeba mabomu, ilikua kwenye mazoezi ya kawaida ambayo hufanyika mara kwa mara. Lakini kwa leo haikuwa na mabomu na ilikuwa na Rubani pekee.

Rubani amenusurika kwani aliruka na mwavuli, amepata majeraha kidogo na kukimbizwa hospital ila ndege yote imeteketea kwa moto.
Ni jet fighter, ilikua kwenye routine exercise za kila wiki. Zilikuwa zinaruka mbili kwa formation. Wakati zina take-off moja ikaanza kuwaka moto nyuma. Rubani alitoka kwa ejector seat, amepona. Ndege imeharibika vibaya.

Moshe Dayan.
 

Attachments

  • ajali_ndege_jeshi_Mwanza_jamiiforums.jpg
    ajali_ndege_jeshi_Mwanza_jamiiforums.jpg
    45 KB · Views: 32,023
  • ajali_mwanza_jwtz_ndege.jpg
    ajali_mwanza_jwtz_ndege.jpg
    71.7 KB · Views: 22,258
Ndege ya jeshi imeanguka mda si mrefu uwanja wa ndege mwanza. tukio na picha vinakuijia mda si mrefu
 
imeanguka ilikuwa na wanajeshi au ilikuwa inafanyiwa majaribio?
 
Ni kweli imeanguka na kuripuka moto.

Ni ndege ya Jeshi ambayo hubeba mabomu, ilikua kwenye mazoezi ya kawaida ambayo hufanyika mara kwa mara. Lakini kwa leo haikuwa na mabomu na ilikuwa na Rubani pekee.

Rubani amenusurika kwani aliruka na mwavuli, amepata majeraha kidogo na kukimbizwa hospital ila ndege yote imeteketea kwa moto.
 
mwanajeshi gani anakimbia na parachut.. angebaki apambane mpaka mwisho!!!

Hahah mkuu ndege za kijeshi especially zile zenye kuwa na rubani mmoja au wawili wakati wa may day rubani anajifyatua kitini kuokoa uhai...

Kufa wakati kuna namna ya kujiokoa si ujasiri huo...
 
Back
Top Bottom