Ndege Robinho atua kwenye Mti wenye Matunda...

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
Klabu yenye mafanikio zaidi hapa ulimwenguni na klabu ilopata kusajili nyota weeengi wa ukweli hapa Duniani yaani AC Milan imefanikiwa kumnyaka kiungo mwenye tashtiti na pilika zenye mafanikio yaani Robinho.

Habari zilizotapakaa kwenye vyombo vya habari Barani Europa vimeripoti kuwa Robinho ametua ktk klabu hii yenye mafanikio zaidi na tayari wachambuzi wa maswala ya soka wameweka wazi kuwa kwa muungano wa Robinho na Gaucho basi lazima mabeki watapike ama wafungulie kabla ya Muda ktk mwezi huu wa Ramadhan.

Robinho amefuatana na mshambuliaji ambaye alipokuwa Ajax aliwapa ubingwa wa ligi ya huko mara kadhaa, halikadhalika alipohamia Juve, Pia aliwapa ubingwa Inter, na Kisha Barca na sasa katua Milan huyu si mwingine bali ni Zlatan Ibrahimovic.

Nami kwa niaba ya makamu mwenyekiti wa Klabu muheshimiwa Adriano Galliani napenda kumtakia kila la kheri Robinho.
 
Teh teh teh teh teh!! wewe ni nani Ac Milan unamtakia kila la kheri? Anyway, hongereni kwa kumrudisha dogo naona sasa atacheza mpira. Ila pale City alikuwa anaua kipaji chake tu.
 
Mkuu naona utaanza kumpamba robinho nae kama ulivyokuwa unampamba Ronaldhino lol,tatizo wa Brazil hawachelewi kukuangusha wanapenda starehe kama hawana akili vizuri.
 
Robinho ni kifaa si utani, man city haikuwa timu haswa anayo paswa kuchezea, sasa ametua kwenyewe, AC Milan!nakumbuka Chelsea tulimkosa dakika za mwisho mwisho kabla hajatua man City.
 
Ndo maana nikasema Ndege katua kwenye mti wenye matunda.
Akitaka siku tumpangie vijana wenzake basi tutampangia kina Pato, Flamini, Antonini, Silva, Abate, Boateng na wengine wachache.

Ila siku akitaka apangiwe makocha basi pale mbele atasimama na Super Pippo, kulia atatokea Mzee Gatusso, kushoto Mzee Seedorf, Dimba la juu Mzee Ambrosini, jiko la chini Uncle Pirlo, fullback Mzee Zambrotta, Fullback Mzee Janckulovsky, Mkoba Uncle Nesta, Kiba Mzee Abiati..

Forza Milan.
 
Mkubwa Gang Chomba sikuona umuhimu wa kumsajili Robinho

  1. Huyo dogo ni msumbufu sana ,sidhani kama atamaliza misimu 2 hapo Milan ,ataanza kulilia kurudi Brazil
  2. Tayari Milan kuna Pato,Ronaldinho,Pirlo,Zlatan,Inzaghi,Boateng,Seedorf sidhani kama atapata nafasi kwa hao wachezaji waliopo
But huenda msimu huu AC MILAN (ROSSONERI) ikarudi kwenye chati Thiago Silva,Pato,Gaucho,Ibrahimovic,Pirlo,Pipo wakiwa OK naamini Juve hamna kitu na Inter baada ya kumpoteza Mourinho huenda MILAN ikarudi
 
Klabu yenye mafanikio zaidi hapa ulimwenguni na klabu ilopata kusajili nyota weeengi wa ukweli hapa Duniani yaani AC Milan imefanikiwa kumnyaka kiungo mwenye tashtiti na pilika zenye mafanikio yaani Robinho.

Habari zilizotapakaa kwenye vyombo vya habari Barani Europa vimeripoti kuwa Robinho ametua ktk klabu hii yenye mafanikio zaidi na tayari wachambuzi wa maswala ya soka wameweka wazi kuwa kwa muungano wa Robinho na Gaucho basi lazima mabeki watapike ama wafungulie kabla ya Muda ktk mwezi huu wa Ramadhan.

Robinho amefuatana na mshambuliaji ambaye alipokuwa Ajax aliwapa ubingwa wa ligi ya huko mara kadhaa, halikadhalika alipohamia Juve, Pia aliwapa ubingwa Inter, na Kisha Barca na sasa katua Milan huyu si mwingine bali ni Zlatan Ibrahimovic.

Nami kwa niaba ya makamu mwenyekiti wa Klabu muheshimiwa Adriano Galliani napenda kumtakia kila la kheri Robinho.
Gang Chomba,Heshima yako. Nakutakia kila la heri msimu huu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom