Inter 0-1 Milan...Ibra the Hero

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
8,790
Likes
845
Points
280

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
8,790 845 280
Ikicheza ndani ya Dakika 30 za mwisho huku wakiwa pungufu uwanjani Klabu yenye mafanikio kuliko klabu zote hapa Duniani yaani AC Milan imeweza kuwabamiza klabu ya Inter kwa goli moja kwa bila, goli lililowekwa kimiani kunako dakika ya 5 ya mchezo na jiwe kuu la pembeni ambalo waashi walilikataa yaani Zlatan Ibrahimovic.

Ktk mpambano huo ambao Inter ndio walikuwa wenyeji walijikuta wakipelekwa puta muda mwingi.

Kipindi cha pili dakika ya 60 ulimwengu ulishuhudia beki wa Milan Ignazio Abate akipewa kadi nyekundu kwa kosa la kumtendea madhambi Goran Pandev.

Washabiki wa Inter walionekana kuwa tofauti msimu huu baada ya kubeba mashuka makuubwa yenye ujumbe wa kupona haraka na kurudi uwanjani kwa mshambuliaji hatari ambaye ameweka rekodi mpya hivi karibuni Super Pippo Filipo Inzaghi mwenye miaka 37 ambaye ameumia vibaya, kitu kitachopelekea akae nje kwa msimu woote huu uliobaki.

Milan sasa wanaongoza Ligi huku Inter wakiwa nafasi ya Tano.
 

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
8,790
Likes
845
Points
280

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
8,790 845 280
Mbon Al-Jazeera leo asubuhi imesema wametoka sare bila ya kufungana na A.C Milan sasa waongoza ligi..................What is happening?
Achana na Al-jazeera weweee.
Wale wanachojuwa ni habari za milipuko tu.
Milan wanaongoza ligi na hao Inter jana wamepodolewa mixer kupaka hina...
 

gutierez

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2010
Messages
1,254
Likes
21
Points
133

gutierez

JF-Expert Member
Joined May 14, 2010
1,254 21 133

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
8,790
Likes
845
Points
280

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
8,790 845 280
inzaghi the legend
Inzaghi ndie mshambuliaji wangu booora kabisa Duniani.
Na ktk thread ya AC Milan ambayo iko ktk maandalizi ya mwisho kabisa kabla haijarushwa hapa JF amepewa nafasi kuubwa sana ya kuzungumziwa.

Pippo kaumia, lakini amesema wazi kuwa atarudi uwanjani na atafunga magoli kama kawa.

Kwa kukusaidia tu ni kuwa Pippo keshawafunga Manchester UTD magoli mawili, Bayern magoli mawili, Liverfool magoli mawili, na Madrid magoli mawili na magoli hayo huyafunga ktk mechi moja...

Nani kama Pippo?
 

Forum statistics

Threads 1,203,079
Members 456,570
Posts 28,098,970