MILAN 4-0 SIENA...Dinho HAT-TRICK hero

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
8,790
Likes
842
Points
280

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
8,790 842 280
Ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Sansiro klabu ya soka yenye mafanikio mengi zaidi ya kimataifa yaani AC Milan iliweza kuibuka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya timu ya Siena.

Shujaa wa Milan ktk mechi hiyo ambaye pia alichaguliwa mapema kuwa ndie Man of the match alikuwa ni kijana wa kibrazil anayeaminika kusakata kabumbu maridhawa wanalocheza Mbinguni yaani Ronaldo de assis de Moreirra almaaruf kama Ronaldinho Gaucho.

Dinho alifunga magoli matatu ktk mechi ambayo vyombo vyote vya habari vya magharibi vimesadiki kuwa Dinho amerudi ktk kiwango chake kileee, huku goli jingine likifungwa na Marco Boriello.

Goli la Boriello limepelekea wachambuzi wa soka kulifananisha na goli lililopata kufungwa na mkongwe wa AC Marco Van Barsten miaka hiyo.

''Hakika hii ndio AC Milan, klabu ambayo kila nyota anahaha kuja kucheza'' ...alisikika makamo wa Rais wa AC Adriano Galliani baada ya mechi.

Nae kocha wa Siena alisikika na kukaririwa akidai nanukuu ''siwezi kumlaumu mchezaji wangu yeyote wala kumshutumu kwa kushindwa kumkaba Dinho. Mtu yeyote timamu anaekabiliwa na mtihani wa kumkaba huyu mtu basi hawezi kupata usingizi kwa wiki nzima mpk anywe Valium'' alisikika kocha huyo huku akionekana kuguswa na aina mpya ya chenga toka kwa Dinho.

January/24/2010 Milan wataingia uwanja kupambana na klabu ya Inter ktk mechi yenye upinzani na inayofahamika kama Della maddonina.

FORZA MILILAN
 

Forum statistics

Threads 1,189,736
Members 450,798
Posts 27,645,707