Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyoagizwa na Serikali imeanza kupamba kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyoagizwa na Serikali imeanza kupamba kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, huku mabango kadhaa jijini Dar es Salaam yakiikaribisha katika anga la Tanzania.

Ndege hiyo bado haijatua nchini, lakini duru zinasema wakati wowote mwezi huu itaanza kupeperusha bendera ya Tanzania angani ikitoa huduma za usafiri za ndani na nje ya nchi.

Kuingia kwa ndege hiyo kubwa kutalifanya Taifa kuwa na ndege mpya nne zilizonunuliwa tangu Rais John Magufuli aingie madarakani.

Ndege nyingine ambazo tayari ziko nchini na zinafanya safari ni Bombardier Q400 tatu ambazo zinasafirisha abiria ndani na nje ya nchi zikiwa chini ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Ndege hizo kila moja ina uwezo wa kuchukua abiria 76, lakini Dreamliner inayokuja ina uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 242 wakiwa katika madaraja matatu yenye hadhi za juu.

Kuanzia mwaka 2011, ATCL imekuwa ikisuasua huku ikitumia ndege moja aina ya Bombadier kufanya safari zake. Rais Magufuli aliingia madarakani akiwa na mpango wa kuifufua ATCL na kuibuka na mkakati wa kununua ndege sita mpya kati ya mwaka 2016 na 2018.

Kwa mujibu wa Shirika la Boeing linalotengeneza pia Boeing 787-8 Dreamliner, aina hiyo ya ndege ilianza rasmi kufanya kazi mwaka 2011 likitaka kuziondoa kwenye soko ndege zake aina ya 767-200ER na 767-300ER pamoja na kuongeza soko la safari za mbali ambalo ndege kubwa zaidi haziwezi kufanya kazi kwa faida. Dreamliner 787-8 inamiliki robo tatu ya soko la ndege aina ya 787 zinazoagizwa na wateja kutoka shirika hilo.

Ujio wa ndege hiyo nchini utaongeza ushindani wa soko la usafirishaji kwa ndege katika ukanda wa Afrika Mashariki ambalo kwa sasa limetawaliwa na Kenya, Ethiopia na Rwanda.

Kutokana na ujio wa ndege hiyo, hivi sasa ATCL imeanza kuwinda masoko ya Kenya, Burundi, Rwanda, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Pia kampuni hiyo inatupia jicho kwenye masoko ya masafa marefu yakiwamo ya Mashariki ya mbali, Mashariki ya kati, Ulaya, Afrika Kusini na Afrika Magharibi.

Ndege%2Bpic.jpg
 
Nchi hii ina watu wa ajabu, Kenye wanazo ngapi, is there something strange to celebrate?
Ukiniona naonea aibu Utanzania wangu usinishangae mkuu Retired, hivi ni kukosa elimu au ni shida gani inayolisumbua taifa hili? mbona huko siku za nyuma hatukuwa hivi?
 
Hahaaaaa, leo nimeshuhudia Jangwani jijini Dar wtembea kwa miguu wakiongezeka hata wanashindwa kupanda daladala kutokea mwembechai wakijipa moyo kwamba, Muhimbili au K/koo ni karibu sihitaji kupanda daladala. Huyo wa kupanda ndege atatoka wapi? hivi hamjui kuna anguko la uchumi Tz? kalagabaho.
 
Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyoagizwa na Serikali imeanza kupamba kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, huku mabango kadhaa jijini Dar es Salaam yakiikaribisha katika anga la Tanzania.
Ndege hiyo bado haijatua nchini, lakini duru zinasema wakati wowote mwezi huu itaanza kupeperusha bendera ya Tanzania angani ikitoa huduma za usafiri za ndani na nje ya nchi.

Kuingia kwa ndege hiyo kubwa kutalifanya Taifa kuwa na ndege mpya nne zilizonunuliwa tangu Rais John Magufuli aingie madarakani.
Ndege nyingine ambazo tayari ziko nchini na zinafanya safari ni Bombardier Q400 tatu ambazo zinasafirisha abiria ndani na nje ya nchi zikiwa chini ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Ndege hizo kila moja ina uwezo wa kuchukua abiria 76, lakini Dreamliner inayokuja ina uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 242 wakiwa katika madaraja matatu yenye hadhi za juu.
Kuanzia mwaka 2011, ATCL imekuwa ikisuasua huku ikitumia ndege moja aina ya Bombadier kufanya safari zake. Rais Magufuli aliingia madarakani akiwa na mpango wa kuifufua ATCL na kuibuka na mkakati wa kununua ndege sita mpya kati ya mwaka 2016 na 2018.

Kwa mujibu wa Shirika la Boeing linalotengeneza pia Boeing 787-8 Dreamliner, aina hiyo ya ndege ilianza rasmi kufanya kazi mwaka 2011 likitaka kuziondoa kwenye soko ndege zake aina ya 767-200ER na 767-300ER pamoja na kuongeza soko la safari za mbali ambalo ndege kubwa zaidi haziwezi kufanya kazi kwa faida. Dreamliner 787-8 inamiliki robo tatu ya soko la ndege aina ya 787 zinazoagizwa na wateja kutoka shirika hilo.

Ujio wa ndege hiyo nchini utaongeza ushindani wa soko la usafirishaji kwa ndege katika ukanda wa Afrika Mashariki ambalo kwa sasa limetawaliwa na Kenya, Ethiopia na Rwanda.

Kutokana na ujio wa ndege hiyo, hivi sasa ATCL imeanza kuwinda masoko ya Kenya, Burundi, Rwanda, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Pia kampuni hiyo inatupia jicho kwenye masoko ya masafa marefu yakiwamo ya Mashariki ya mbali, Mashariki ya kati, Ulaya, Afrika Kusini na Afrika Magharibi.View attachment 802953
 
mtukufu sana raisi naomba hizi ndege ziitwe kwa majina yako, tena yote manne yakitanguliwa na "Air" halafu kule mwisho kabisa tuweke "here job only". Hahaaa.
 
Yaani hadi raha

Magufuli oyeeeeeeeeee

Hiyo wengine na mie tutaipanda tu kumsapoti JPM kama kuyapanda tumeshayapanda. Mtuambie wapi kuna burudani tuje tusaze tugeuze ndani ya masaa 24

Trip ya kwenda kuuona mlima kilimanjaro tena kufika KIA na kugeuza baada ya kupumzika kwa hoteli nzuri huko..

IMG-20180704-WA0051.jpg
 
Hahaaaaa, leo nimeshuhudia Jangwani jijini Dar wtembea kwa miguu wakiongezeka hata wanashindwa kupanda daladala kutokea mwembechai wakijipa moyo kwamba, Muhimbili au K/koo ni karibu sihitaji kupanda daladala. Huyo wa kupanda ndege atatoka wapi? hivi hamjui kuna anguko la uchumi Tz? kalagabaho.

Uwezo wako wa Kuchambua masuala yahusuyo Uchumi ni mdogo sana halafu unaonekana hata IQ yako nayo ni ya kushikiwa na Kamba ili isianguke. Ethiopia na Uturuki wao walianza zamani sana kuwekeza katika Biashara za Ndege na kwa 75% ' driving force ' ya Uchumi wao unatokana na kuwepo kwa Ndege nyingi ambazo zinawaingizia Watalii wengi kila mwaka lakini hata hivyo katika hizo nchi bado matatizo ya Kijamii yapo tena pengine hata kuzidi ya huku Kwetu sema tu Watanzania wengi hasa mnaojifanya ni ' Wanaharakati ' huwa hampendi kuwa wafuatiliaji wa mambo mengine ya nchi zingine.

Kidunia sasa hivi Uchumi bado hauko vizuri ukipata muda tembelea Jarida la the Economist ili uweze kufahamu namaanisha nini hapa. Ni kweli yawezekana ujio wa hizo Ndege unaweza bado usilete Tija ya haraka au kutatua matatizo ya haraka ya Watanzania ila angalau ujio wake unaweza kuimarisha Sekta ya Usafirishaji, Kuzidisha idadi ya Watalii na hata Wafanyabiashara mbalimbali kuweza kusafirisha kwa uharaka bidhaa zao hali ambayo itaimarisha kidogo Uchumi wetu na Serikali kupata mapato ambayo yakiongezewa na yale yanayopatika Kiujumla basi huduma zingine za Jamii zinaweza zikaanza kupatiwa ufumbuzi na pengine huwezi jua yatanunuliwa Mabasi mengi tu ya Usafiri na hilo tatizo lako ulilolipata au ulilolishuhudia leo hapa Jangwani likapatiwa ufumbuzi na kuwa Historia. Siku zingine jitahidi kuwa unafikiri Kisomi na unapokuja humu JamiiForums tafadhali ila bado unahitaji mno Kujiimarisha Kimaarifa, Kitaarifa na hadi Kiupeo.
 
Ahsante kwa kuni-let down ila ukweli utatuweka huru. Wewe unaridhika na uchumi wa kugushi unao semwa kila siku kwamba uchumi wa Tz unakua kwa 7%!!.
 
Naunga mkono hoja yako...ili kuunga juhudi za mtukufu raisi hizi ndege iitwe kwa majina yake
mtukufu sana raisi naomba hizi ndege ziitwe kwa majina yako, tena yote manne yakitanguliwa na "Air" halafu kule mwisho kabisa tuweke "here job only". Hahaaa.
 
Ahsante kwa kuni-let down ila ukweli utatuweka huru. Wewe unaridhika na uchumi wa kugushi unao semwa kila siku kwamba uchumi wa Tz unakua kwa 7%!!.

Mimi kubishana nawe ni sawa sawa na kutaka kuwapambanisha Mchezaji Neymar Jr wa Brazil na PSG pamoja na Mchezaji Emanuel Martin wa Yanga SC ya Tanzania. Namalizia kwa kusisitiza tena Kwako kwamba jibiidishe Kwanza na uwezo wako wa akili hasa katika kuyajua na kuchambua mambo mbalimbali kisha hakikisha kila siku iendayo kwa Mungu unaongeza maarifa fulani katika Kichwa chako ila katika kukurahisishia tu Kazi hakikisha mara kwa mara hukosekani hapa JamiiForums The Home of Great Thinkers ili tukusaidie Kufikiri ' Kisomi ' zaidi kusudi siku zingine usiendelee kuonekana ' Kituko ' na ' Mpuuzi ' wa Kutukuka.
 
Hahaaaaa, leo nimeshuhudia Jangwani jijini Dar wtembea kwa miguu wakiongezeka hata wanashindwa kupanda daladala kutokea mwembechai wakijipa moyo kwamba, Muhimbili au K/koo ni karibu sihitaji kupanda daladala. Huyo wa kupanda ndege atatoka wapi? hivi hamjui kuna anguko la uchumi Tz? kalagabaho.
Sio kila mtu anatakiwa kupanda ndege na hio si Tanzania tu hata huko walikoendelea sio kila mtu anapanda ndege. Wa kupanda ndege wapo wengi tu na hilo anguko la uchumi.

Halafu utakuwa umekuja mjini juzi, hapo Jangwani watu wanakatiza kwa miguu tangu enzi za Nyerere, tena kuna short cut wengine walikuwa wanatokea Kinondoni wanapita bondeni huko.
 
Back
Top Bottom