Ndani ya JF: Hakuna ambalo halijawahi kusemwa Juu ya Yanayotokea Ndani ya CHADEMA

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,429
1,045
Awali ya yote nawaomba Mods wasiuunganishe huu uzi wala kuuhamisha hapa. Lengo la huu uzi ni kudhihirisha ujungu kuu wa JF. Hivyo, hapa nitarejesha nyuzi mbalimbali za miaka kadhaa nyuma iliyotoa mwangwi wa hiki kinachodhihirika kwa wengi hivi leo juu ya vijana wa CHADEMA.

Tuanze na uzi huu wa December, 2011: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...n-saanane-waweza-kuanzisha-chama-kingine.html


Ukweli wake unathibitika kwenye kitubio (Confession) ya Ben Saanane mwaka huu. Soma hapa chini:

 
Let us wait and see!!
Nadhani huu si mwisho wa mwanzo bali ni mwanzo wa mwisho
 
Mganga wao angekuwa nani CHAUMMA? Sure, a coward is a coward no matter what his level of education is. This is the poorest mastermind ever by those who claim to be hypes.

Hivi Kafulila, Machange, Zitto, Saanane etc wakati wanafanya yote haya walikuwa wanacheka, wanatabasamu, wanahuzunika, wamenuna au wanasikitika?

Heri yao kama walikuwa wamenuna, wanahuzunika na kusikitika maana hayo yangeashiria huu mwisho wao.
 
Let us wait and see!!
Nadhani huu si mwisho wa mwanzo bali ni mwanzo wa mwisho

...dah!...haya maneno yanaweza kukusababishia "brain concussion"...yaaani halijulikani lipi jike na lipi dume...
 
Kuna maswali najiuliza bado sijapata majibu kuhusu Zitto:

1) Kimya chake ni busara kwa ajili ya kujenga chama au ukweli wa yanayoelezwa dhidi yake?

2) Kama hizi habari si za kweli, nini hatua atakayochukua? Kuomba radhi and move on, kuhama chama? or quit politics?

3) Ataamua kuchukua hatua za kisheria na kufungua kesi kwa kudhalilishwa?

All in all, kimya kingi kina mshindo mkuu.
 
Nakuunga mkono kwa asilimia zote , Jf ilidadavua haya yote mapema sana , kwa wenye kumbukumbu nzuri hakuna jipya , labda hili la wengine kuanza kutubu sasa , japo huyu Mchange alishatubu siku nyingi kwenye uchaguzi wa Bavicha !
 
Soma sehemu hii ya kitubio:

Unganisha tarehe na matukio yaliyofuatia kama ninavyojaribu kukupa dondoo hapo chini kisha umwambie kipofu kuwa mnyama aliye mbele yake siyo Tembo bali Sisimizi!


 
Mimi naomba waendelee na mpango wao bila kuegemea CDM. Ndo maana Wasira alisema kwa mdomo mpana kuwa CDM itakufa kabla ya 2015. Mungu kawaumbua kajipangeni upya. Zitto, waweza kujibu hizi tuhuma?
 
That why i said ! Kutubu kunahitajika! Sisiem masalia,nccr masalia na cdm masalia! Upanga unashuka bado haujakata na nafasi ya kutubu bado ipo sijui kwa wanaoamini uchawi! God knows
 

Wakati wa Mahojiano hivi karibuni Wana-JF walipigwa changa la macho kwenye suala la chama kipya kama ifuatavyo:


Kitubio kinasema haya juu ya uwepo wa chama kipya na kinadokeza waanzilishi nyuma ya pazia:

 
Chadema will pass this test, hao vijana wameingi aktk ujinga, na huo ujinga ndio utawaponza kuishi ktk ujinga na kuwa, wajinga, wajinga, watakuwa wajinga wasioweza tena toka ktk huo ujinga ua hata kuisumbua CDM tena.
 
Mkuu Omutwale umegonga Ikulu,,,

Lakini ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua kuwa Zitto anawatumia tu hawa vijana lakini tamaa yake iko kwenye gesi ya Mtwara. Hebu fikiria ile Thread ya TUNTEMEKE ya Barua ya watu wa kusini kwa Zitto inayohusu gesi, then nenda kwenye maelezo ya Kafulila kuwa Zitto ndio atatengeneza sera ya gesi ya CHAUMMA na maandiko yake mengi ambayo Zitto huwa anayatoa kuhusu gesi... Huyu dogo ni hatari sana kwa usalama na ustawi wa Taifa letu, na kwa kuwa anajilinda kishirikina anakuwa anajiamini kupita kiasi
 

Zito ni mshirikina kupita maelezo. Ukitaka habari kamili muulize Mudhihiri Mudhihiri, alivyokatika mkono hule hule aliomnyooshea Zito Matunguli bungeni....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…