Ndani ya JF: Hakuna ambalo halijawahi kusemwa Juu ya Yanayotokea Ndani ya CHADEMA

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,431
2,000
Awali ya yote nawaomba Mods wasiuunganishe huu uzi wala kuuhamisha hapa. Lengo la huu uzi ni kudhihirisha ujungu kuu wa JF. Hivyo, hapa nitarejesha nyuzi mbalimbali za miaka kadhaa nyuma iliyotoa mwangwi wa hiki kinachodhihirika kwa wengi hivi leo juu ya vijana wa CHADEMA.

Tuanze na uzi huu wa December, 2011: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...n-saanane-waweza-kuanzisha-chama-kingine.html


Ukweli wake unathibitika kwenye kitubio (Confession) ya Ben Saanane mwaka huu. Soma hapa chini:

Tulikubaliana katika kundi hili tuwe na mkakati wa siri na tukusanye fedha nje na ndani ya chama.suala la kukusanya fedha nje ya chama nililipinga sana.Nakumbuka Mchange ndiye aliyeleta wazo la kukusanya fedha nje ya chama.miongoni mwa walengwa walikua
-David Kafulila
-Mwigulu Nchemba
-Deo Filikunjombe
na baadhi ya wafanyabiashara

Draft niliyoandika ilionekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa wale ambao walikua potential donors.

Pia Habibu Mchange alileta taarifa kwenye kikao kwamba Zitto amemwambia tuandae bajeti ya kundi hili. Zitto alisafiri siku hiyo bila kutuambia na tulilalmika sana sana. Baada ya hapo alikua akiwasiliana na mtu mmoja mmoja. Hata hivyo kwa kuwa ulikua mpango wa siri nilipendekeza tutumie code names au namba zilizochanganywa na herufi kama mbinu mojawapo ya kijasusi. Mwishowe kila mmoja alikubaliana tutumie tu majina kwa kuwa walihofia kusahau code names.tulibatizana majina na jina langu likawa COBRA, Mchange-Mdude, Shonza-Benazir, Mwampamba-Kony na code name ambayo tuliitumia kwa Zitto ni Prezzo au Dogo

Role yangu mimi ilikua katika fedha baada ya majadiliano kwa kuwa kila mjumbe alisema Ben ndiye tunayemuamini pekee katika usimaizi wa fedha na kubuni vyanzo vya fedha. Nilipewa kazi ya kuandaa bajeti.Lakini nilikataa kwa kuwa nilisema bado siridhishwi na mwenendo wa kukusanya fedha nje ya chama.

Shonza Alikuwa Mwenyekiti wa PM7 strategically ili awe na wajibu mkubwa kwa kuwa alikua kiongozi wa juu wa BAVICHA. Mchange alijichagulia kuwa makamu Mwenyekiti, Mwampamba Katibu, Festo Sanga alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE akisaidiana na mchange na Mwampamba. Tulikubaliana iwe taasisi kwa kundi lote la Masalia ili itumike panapolazimika. Sikuwahi kuitumia kwa kuwa niliwaambia nitaendelea kutumia ID yangu kwa kuwa siatamtukana mtu au kuzusha kitu hata kama michango yangu ingeniweka matatani

Hata hivyo baadae nilikubali na niliandaa bajeti ya Sh. 25,000,000 kwa awamu ya kwanza na tukachora ramani ya jinsi tutakavyogawana mikoa.

Lengo lilikua kuingia mikoani hata kwa lazima na kufanya mikutano ya hadhara na kujenga mtandao. PM7 ilikuja kubadilika na malengo yakawa too narrow kwa kuwa yalilenga kuimarisha kundi ndani ya chama. Badala ya Patriotic Movement ilikuja kuwa PINDUA MBOWE-7. Lengo hapa lilikua kumtenganisha mwenyekiti na Katibu mkuu ili kundi liweze kuimarika na kupenya kati kati. Hapa ndipo kazi ambayo ilikua imekwisha anza mwezi wa 4 katika kampeni za Arumeru Mashariki ya kumchafua Mbowe na Katibu mkuu kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE iliposhamiri

Actually, niliona hatari ya kukichafua chama hasa tuhuma zilizokuwa ziktumika zilikua tuhuma za uongo na uzushi.Wakati tunafanya maandalizi ya kufungua akaunti benki, nilikutana na Dr. Kitila kwa haraka na kumweleza kama zitto au yeyote amemweleza kuhusu kundi hili. Alinijibu kwamba hana taarifa hizo.Hata hivyo tulikubaliana tukutane haraka na Zitto tuweke mikakati mipya kwa kuwa alishangaa ni kwa nini amewahusisha akina Mchange na Mwampamba huku akijua siyo watu makini katika strateggy na ni waropokaji. Aliniomba nifanye mpango wa kulivuruga kundi hili na Pm-7 ife taratibu. Baadae alinieleza kwamba tutapanga siku tutoke nje ya Dar mimi, yeye na zitto tuweke mikakati upya kwa kuwa hapa dar tulikua tunafuatiliwa sana sana. Nilifanikiwa katika mipango hii ya kuiua Pm-7 taratibu na hata wakati mwingine tuligombana sana na baadae kwenye kiakao karibu na Pacific hotel pale Manzese, Mchange na Mwampamba waliibuka na hoja kwamba kuna haja ya kwenda kula viapo kwa mganga ili tusisalitiane katika kazi hii pm-&. Kwa bahati nzuri shonza, Mimi naMwakajila tulipinga vikali upuuzi huu. Shonza hili unalijua na unajua ni kiasi gani nilikasirika siku hiyo. Uliniandikia Message na kunisihi tuendeleze kundi hili

Baada ya hapo wakati kikao cha bajeti kinaendelea Shonza na Mwampamba walinipigia simu kuhusu kikao cha dgharura na David Kafulila. Ilikuwa Tarehe 4/07/2012. Tulikutana Tamal Hotel. Kafulila alitudokeza juu ya kusajiliwa kwa chama cha CHAUMMA, tulijadili mambo mengi.Nilishirikishwa juu ya kujiunga na CHAUMMA na kuhakikisha kinasajiliwa rasmi kwa usajili wa kudumu. Kafulila alinisihi sana na kuniambia ndani ya CHADEMA yatanikuta yaliyomkuta yeye kwa hiyo tuungane. Nilimwambia nitafikiria. Hussein Bashe alikuja dakika za mwisho kwenye kiako kile. Yeye ni miongoni mwa mashuhuda. Kafulila aliniambia mzee Hashim Rungwe pia atajiunga na anafanya mawasiliano na Zitto. Tulipanga kukutana siku iliyofuata. Mwampamba alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao pamoja na Shonza. Siku hii mchange hakuwepo

Tarehe 7/07/2012 nilikuwa ndani ya Ofisi ya CHAUMMA. Nilitambulishwa kwa viongozi wote tukaweka mikakati. Mingine sitaiandika hapa kwa sasa. Walinipa kazi ya kuandika sera ya Vijana na sera ya mambo ya nje huku Kafulila akisema kwenye uchumi sera ya gesi atashirikiana na Zitto kwa kuwa wote wana utaalamu kutoka holand na Norway. Niliwakubalia kimkakati hasa nilipogundua wanapanga kupunguza kura za CHADEMA mwaka 2015 huku akiniahidi kwamba kundi kubwa litatoka CCM na CHADEMA baada ya chaguzi za ndani mwaka huu na mwaka ujao respectively. Aliniambia hata akina Hashim Rungwe wapo nyuma ya kundi hilo na vigogo wa CCM. Mliniambia CHAUMMA kitakua chama darasa. Kafulila anaweza kuthibitisha hili.

Katibu Mwenezi wa CHAUMMA ndg.Mawazo Athanas kutoka kigoma alinisihi sana nimsaidie na Zitto akiwa nje amemuhakikishia kwamba sisi tutamsaidia yaani masalia group au PM-7. Hapa Dr. Kitila mkumbo hakuhusika.Ikumbukwe Mawazo athanas alikua Mgombea Ubunge kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi huko kigoma na baada ya kuhama alitaka kujiunga na CHADEMA. Nilimshawishi sana ajiunge na CHADEMA lakini baadae nilimsikia yupo CHAUMMA. Nilikuwa nikifahamiana naye hapo kabla. Tuliendelea kuwasiliana nae kwa karibu na pia nikamuahidi Kafulila na uongozi wa juu wa CHAUMMA kwamba nitatoa ushirikiano ila waandae vitendea kazi. Nitaweka baadhi ya mawasiliano yetu hapa. Hata ID ya CHAUMMA hapa JF niliifungua mimi nikiwa ndani ya Ofisi za CHAUMMA na tulipeana Password. Kafulila alitaka nimpe paswd yeye, Katibu Mwenezi na katibu mkuu huku akiahidi kwamba atampa zitto itakapobidi. Alinisihi nisiwape akina Mchange na wengine kwa kuwa wanaweza kuharibu na kuonyesha wazi kwamba lengo la CHAUMMA ni kuigawa CHADEMA. Alitaka tuende kimya kimya. Akina Mchange na Mwampamba waliendelea kutumia ID Fake na ID ya TUNTEMEKE. Hii ni sehemu ndogo tu,sitaki kuharibu mambo mengi hapa hasa nyeti kwa kwa chama.

Nitaendelea....Nikihitajika nitakuja tena
 

Jallen

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
516
225
Let us wait and see!!
Nadhani huu si mwisho wa mwanzo bali ni mwanzo wa mwisho
 

Acha Uvivu

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
526
195
Mganga wao angekuwa nani CHAUMMA? Sure, a coward is a coward no matter what his level of education is. This is the poorest mastermind ever by those who claim to be hypes.

Hivi Kafulila, Machange, Zitto, Saanane etc wakati wanafanya yote haya walikuwa wanacheka, wanatabasamu, wanahuzunika, wamenuna au wanasikitika?

Heri yao kama walikuwa wamenuna, wanahuzunika na kusikitika maana hayo yangeashiria huu mwisho wao.
 

Freshthinking

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
621
170
Kuna maswali najiuliza bado sijapata majibu kuhusu Zitto:

1) Kimya chake ni busara kwa ajili ya kujenga chama au ukweli wa yanayoelezwa dhidi yake?

2) Kama hizi habari si za kweli, nini hatua atakayochukua? Kuomba radhi and move on, kuhama chama? or quit politics?

3) Ataamua kuchukua hatua za kisheria na kufungua kesi kwa kudhalilishwa?

All in all, kimya kingi kina mshindo mkuu.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
88,440
2,000
Nakuunga mkono kwa asilimia zote , Jf ilidadavua haya yote mapema sana , kwa wenye kumbukumbu nzuri hakuna jipya , labda hili la wengine kuanza kutubu sasa , japo huyu Mchange alishatubu siku nyingi kwenye uchaguzi wa Bavicha !
 

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,431
2,000
Soma sehemu hii ya kitubio:
…Lengo hapa lilikua kumtenganisha mwenyekiti na Katibu mkuu ili kundi liweze kuimarika na kupenya kati kati. Hapa ndipo kazi ambayo ilikua imekwisha anza mwezi wa 4 katika kampeni za Arumeru Mashariki ya kumchafua Mbowe na Katibu mkuu kwa kutumia ID ya TUNTEMEKE iliposhamiri

Unganisha tarehe na matukio yaliyofuatia kama ninavyojaribu kukupa dondoo hapo chini kisha umwambie kipofu kuwa mnyama aliye mbele yake siyo Tembo bali Sisimizi!

Kweli leo nimestushwa sana na habari kuhusu kile kinachoitwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa. Ingawa habari yenyewe imeondolewa lakini madhara yake yatakuwa ni makubwa sana kama Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa nikikaa kimya. Sijui kama huyo anayejiita TUNTEMEKE kama hata anajua ni kwa jinsi gani watu wanapambana kuuondoa mfumo mbovu uliopo.
Nawasilisha!!
Allen Kilewella
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa

Mgombea wa CCM Sioi Sumari ameendelea kukonga nyoyo za wana Arumeru leo baada ya kuhutubia maelfu na maelfu ya wananchi wa Arumeru leo na kuvunja rekodi kabisa ya Chadema katika mji wa USA River hii leo.

Wakati huohuo Viongozi wa Chadema wamepoteza munkari ya kuendelea kunadi sera za chama chao kutokana na kauli nzito iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe ya kutangaza kuwania nafac ya Urais wa Tanzania kupitai chadema 2015. Vilevile wanachama na mashabiki wa chadema wameendelea kugawanyika katika makundi makuu mawili moja likimuunga mkono muasi Zitto Kabwe na lingine likumuunga Mkono Slaa a.k.a Wade wa bongo hivyo timu ya kampeni imeshindwa kujipangilia kabisa na kufanya mikutano ya leo na jana kupwaya sana.
CCM tunaendelea kuchanja mbuga, Chadema endeleeni kugombania Uraisi
 

ingwe

Member
Apr 1, 2012
27
0
Mimi naomba waendelee na mpango wao bila kuegemea CDM. Ndo maana Wasira alisema kwa mdomo mpana kuwa CDM itakufa kabla ya 2015. Mungu kawaumbua kajipangeni upya. Zitto, waweza kujibu hizi tuhuma?
 

mhindijohn

JF-Expert Member
Nov 25, 2012
469
195
That why i said ! Kutubu kunahitajika! Sisiem masalia,nccr masalia na cdm masalia! Upanga unashuka bado haujakata na nafasi ya kutubu bado ipo sijui kwa wanaoamini uchawi! God knows
 

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,431
2,000
Mganga wao angekuwa nani CHAUMMA? Sure, a coward is a coward no matter what his level of education is. This is the poorest mastermind ever by those who claim to be hypes.

Hivi Kafulila, Machange, Zitto, Saanane etc wakati wanafanya yote haya walikuwa wanacheka, wanatabasamu, wanahuzunika, wamenuna au wanasikitika?

Heri yao kama walikuwa wamenuna, wanahuzunika na kusikitika maana hayo yangeashiria huu mwisho wao.

Wakati wa Mahojiano hivi karibuni Wana-JF walipigwa changa la macho kwenye suala la chama kipya kama ifuatavyo:

AshaDii said:
Vipi tetesi kuwa wewe na Kafulila mmeanzisha chama na una mkakati wa kutimkia huko?
Swali hili na lililotangulia yanaonyesha kuwa hizi kweli ni tetesi tu. Sasa kama unasema nina mkakati wa kuhamia CCM. Tena kuna tetesi nimeanzisha chama na nataka kuhamia huko, sasa mimi nina vyama vingapi nitakavyohamia. Sijawahi hata kufikiria kuanzisha chama cha siasa. Chama changu ni CHADEMA na sitaondoka CHADEMA. Kinachonisikitisha ni kwamba kuna viongozi wa CHADEMA wamekula sumu hii na bila woga wanaisema kana kwamba ni kweli.

Kitubio kinasema haya juu ya uwepo wa chama kipya na kinadokeza waanzilishi nyuma ya pazia:

...Baada ya hapo wakati kikao cha bajeti kinaendelea Shonza na Mwampamba walinipigia simu kuhusu kikao cha dgharura na David Kafulila. Ilikuwa Tarehe 4/07/2012. Tulikutana Tamal Hotel. Kafulila alitudokeza juu ya kusajiliwa kwa chama cha CHAUMMA, tulijadili mambo mengi.Nilishirikishwa juu ya kujiunga na CHAUMMA na kuhakikisha kinasajiliwa rasmi kwa usajili wa kudumu. Kafulila alinisihi sana na kuniambia ndani ya CHADEMA yatanikuta yaliyomkuta yeye kwa hiyo tuungane. Nilimwambia nitafikiria. Hussein Bashe alikuja dakika za mwisho kwenye kiako kile. Yeye ni miongoni mwa mashuhuda. Kafulila aliniambia mzee Hashim Rungwe pia atajiunga na anafanya mawasiliano na Zitto. Tulipanga kukutana siku iliyofuata. Mwampamba alipewa kazi ya kuandika kwenye mitandao pamoja na Shonza. Siku hii mchange hakuwepo
 

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,264
2,000
Chadema will pass this test, hao vijana wameingi aktk ujinga, na huo ujinga ndio utawaponza kuishi ktk ujinga na kuwa, wajinga, wajinga, watakuwa wajinga wasioweza tena toka ktk huo ujinga ua hata kuisumbua CDM tena.
 

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
Mkuu Omutwale umegonga Ikulu,,,

Lakini ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua kuwa Zitto anawatumia tu hawa vijana lakini tamaa yake iko kwenye gesi ya Mtwara. Hebu fikiria ile Thread ya TUNTEMEKE ya Barua ya watu wa kusini kwa Zitto inayohusu gesi, then nenda kwenye maelezo ya Kafulila kuwa Zitto ndio atatengeneza sera ya gesi ya CHAUMMA na maandiko yake mengi ambayo Zitto huwa anayatoa kuhusu gesi... Huyu dogo ni hatari sana kwa usalama na ustawi wa Taifa letu, na kwa kuwa anajilinda kishirikina anakuwa anajiamini kupita kiasi
 

MD25

JF-Expert Member
Jan 28, 2012
3,075
1,195
Mkuu Omutwale
umegonga Ikulu,,,

Lakini ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua kuwa Zitto anawatumia tu
hawa vijana lakini tamaa yake iko kwenye gesi ya Mtwara. Hebu fikiria
ile Thread ya TUNTEMEKE ya Barua ya watu wa kusini kwa Zitto inayohusu
gesi, then nenda kwenye maelezo ya Kafulila kuwa Zitto ndio atatengeneza
sera ya gesi ya CHAUMMA na maandiko yake mengi ambayo Zitto huwa
anayatoa kuhusu gesi... Huyu dogo ni hatari sana kwa usalama na ustawi
wa Taifa letu, na kwa kuwa anajilinda kishirikina anakuwa anajiamini
kupita kiasi

Zito ni mshirikina kupita maelezo. Ukitaka habari kamili muulize Mudhihiri Mudhihiri, alivyokatika mkono hule hule aliomnyooshea Zito Matunguli bungeni....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom