Ndalichako: Marufuku wasio na sifa kujiunga na masomo ya shahada kwa kupitia kozi za'foundation'

Hivi waziri anaweza kuwa proud kuwa ametengeneza mazingira mazuri kwa shule ZOTE kuwezesha watoto wenye sifa wafaulu sekondari?

Hivi waziri anaweza kututhibitishia kuwa maelfu ya wahutimu waliopitia mfumo wa o-level, - certificate - diploma - degree wana elimu duni kuliko waliopitia form V/VI?

Hivi waziri anaweza kututhibitishia kuwa mabadiliko haya anayotaka kuyaleta yapo supported na tafiti za kitaalamu?
Kazi ipo. Maana yake ni kwamba hata ule mpango wa kutambua taaluma nje ya mfumo rasmi unazikwa! RPL=Recognition of Prior Learning
 
Vyuo vingi kwa mfano UDSM kuna kozi za Certificate ktk Computer Science na Diploma ktk Computer Science.
Vijana wanaomaliza hapo wanakuwa na uelewa mpana wa concepts za ICT na wanapojiunga Degree wanakuwa advanced kabla ya hawa waliotoka High school hawajacatch up!

Serikali isiue ndoto za Vijana wa nchi hii kutimiza ndoto zao.

Serikali lazima ifahamu kuwa, Graduates wengi ni muhimu sana kwetu sisi ndani ya EAC, la sivyo Wakenya watakomba kazi zote.

Kinachotakiwa ni kuboresha vyuo, na viwango, mitala, na ubora siyo kufuta mifumo!.

Elimu ya high school, imejengwa ktk misingi ya kuchuja watu, ndiyo maana kuna watu walikesha Wanasoma Organic Chemistry lakini baada ya kumaliza NECTA hawajawahi kuitumia popote, Lakini mwanafunzi anayepitia Diploma, Akiingia chuo anakuwa na msingi mzuri

Kama serikali inataka kuboresha elimu. Ianzie chini huku kuanzia Lindergarten, otherwise hizi measures nyingine zitaumiza wananchi!
 
Mh, halafu asimamie mitihani vizur ili kusiwe na cheating, maana hali ni ngumu.
 
Mkuu lakini siyo kweli kama alivyotaka kutudanganya huyu mleta mada. Waziri alikuwa anazungumzia foundation courses za OUT. Nafikri mleta mada ana uelewa mdogo kuhusu foundation courses yeye akajumuisha ni pamoja na wenye diploma. Hebu jaribu kuisikiliza hiyo clip aliyoweka hapo kama utasikia kwamba anapiga marufuku mtu mwenye diploma kwenda kumilki degree! Mbona hata yeye hakwenda moja kwa moja form 6? Hebu atuwekee hapa CV yake tuione si unaona hata kule kwenye biography ya bunge hajaweka yote hayo sijui anamficha nani? Kaanzaia walimu wa kawaida huyo akajiendeleza mpaka kufika hapo alipo!! SUA mbona kuna maprof kibao ambao wamesoma certificate mpaka kuwa maprof na wanapiga mziki siyo kawaida? Hata Banna mwenyewe si kaanzia kule chini? Haiwezi ikawa hivyo!
Hii issue inapigiwa siasa tu. Mjadala umekuzwa bila sababu. Wanamuwekea maneno ambayo hajatamka.
 
Nchi zilizo ondelea kama mfano uk ,unaweza kujiunga na elimu ya juu bila ya kuwa na leaving certificate.

Ukishajua kusoma na ku andika ikiwa upo over 18 unajiunga na college, una anza na foundation mwaka mmoja, baadae level 1 kwenda 2,3 baadae degree, level hizi ni diploma.

Maelekezo zaidi angalieni mfano East Ham college
Mkuu naona ulinganisho unaofanya sio kwa sababu kwa tulipokuwa tumefikia ni majanga
Mwache prof aweke mambo sawa ndio urudi tena na swaga zako za uk
 
Swali la msingi, je wale wote waliojiunga na degree Kwa Sifa ya diploma ndo anaongoza Kwa kudisco au kupata supplementary??
Kimsingi sioni km waziri ana hoja ya msingi ktk hilo, kiukweli mwanafunzi aliemaliza diploma na kujiunga degree atakuwa more competanty.
Hoja ya waziri ndalichako haliwezi kunizuia kujiendeleza mwanangu toka diploma to degree bila kusoma form six.
Atasoma hata nje ya nchi na akawa msomi mzuri Sana.
Kama wameshindwa kuwapatia wanafunzi mikopo sasa wataanza kutafuta namna ya kupunguza idadi ya wahitaji mikopo mwakani
 
Hivi waziri anaweza kuwa proud kuwa ametengeneza mazingira mazuri kwa shule ZOTE kuwezesha watoto wenye sifa wafaulu sekondari?

Hivi waziri anaweza kututhibitishia kuwa maelfu ya wahutimu waliopitia mfumo wa o-level, - certificate - diploma - degree wana elimu duni kuliko waliopitia form V/VI?

Hivi waziri anaweza kututhibitishia kuwa mabadiliko haya anayotaka kuyaleta yapo supported na tafiti za kitaalamu?

Kaka bora ww umeliona hili! Leo hii unaweka competition ya mtu mweny div one aliyemalza feza au marian na mtu mweny div one kutoka government scul kucompete nafas za chuo
 
Kingne cha kufahamu n kwamba UGUMU WA ELIMU(ugumu wa kufaulu) cio ubora wa elimu. Itz useless kuwa na elimu ngum qmbayo haitatui mattzo yanayokuzunguka
 
Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila kupita kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katika mwaka ujao wa masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.

Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na kwenda kusoma certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu hawataruhusiwa kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia (reseat) masomo yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na wafanye mitihani ya kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo vikuu.

Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne watakaoruhusiwa kusoma shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni wale waliofaulu kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma katika vyuo vya ufundi daraja la kati (Technicians). Lakini wale wanaokosa "credit" za kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mwisho wao utakuwa diploma, na diploma zao hazitaruhusiwa kutumika kama equivalent pass ya kujiunga chuo kukuu hadi watakaporeseat.

Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa.

"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza Ndalichako.

Unaweza kumsikiliza zaidi hapa:
 
Issue nikwamba awana pesa ya kuwapa mikopo wanachuo so wanatafuta njia yakupunguza udaili.ebu waongee ukweli.nikama no bunge live but kuna makonda live
 
Hakuna mtu anaejitaid kurudisha elimu yetu kwenye ubora wake kama waziri Ndalichako......
Elimu za hovyo, na digrii dhaifu zilijaa mtaani
Hata hivyo ulisikiliza hiyo clip hajasema hivyo..
Kwani lazima kila mtu aww na digrii?
Zamani digrii zilikuwa za vipanga tu, huko ndipo tunapotakiwa kwenda.
Ha ha ha ha et degree zlkuwa za vipanga wakat vipanga wa juz ndo watumishi wa leo walio tayar kioana tanzania ikinazama bila kusema kitu
 
Hakuna mtu anaejitaid kurudisha elimu yetu kwenye ubora wake kama waziri Ndalichako......
Elimu za hovyo, na digrii dhaifu zilijaa mtaani
Hata hivyo ulisikiliza hiyo clip hajasema hivyo..
Kwani lazima kila mtu aww na digrii?
Zamani digrii zilikuwa za vipanga tu, huko ndipo tunapotakiwa kwenda.
Hivi kama hao wenye diploma walijiunga vyuo vikuu na kumaliza vyuo vikuu bila kushindwa hapo kosa ni mwanafunzi au mkufuzi?

Hivi kuna nchi gani Duniani ambapo imeweka kikomo cha elimu kwa watu wake kama Tz inavyo taka kuweka kizingiti?

Je serikali ina uthibitisho gani wa kuwa watz wenye shahada na ambao walijiunga vyuo kwa kuwa na diploma ndo wana kiwango duni cha ufahamu,?

Mimi nadhani tuna kimbilia kukata matawi ya matatizo ya elimu yetu na wala si mashina na mizizi ya matatizo
 
wh wasiweke mahitraji ya form4 pia kwa anayeingia chuo,

meaning hata kama ana certificate/diploma analazimika pia kuwa na C 3 za form 4! nadhani itaondoa ujinga jinga wa vicertificate kibaaao visivo na tija
 
Back
Top Bottom