Ndalichako: Marufuku wasio na sifa kujiunga na masomo ya shahada kwa kupitia kozi za'foundation'

Hivi waziri anaweza kuwa proud kuwa ametengeneza mazingira mazuri kwa shule ZOTE kuwezesha watoto wenye sifa wafaulu sekondari?

Hivi waziri anaweza kututhibitishia kuwa maelfu ya wahutimu waliopitia mfumo wa o-level, - certificate - diploma - degree wana elimu duni kuliko waliopitia form V/VI?

Hivi waziri anaweza kututhibitishia kuwa mabadiliko haya anayotaka kuyaleta yapo supported na tafiti za kitaalamu?
Hapo umepinga kwasababu umepinga, lakini Waziri huko sahihi. Siku zote mmekuwa mkilalamika elimu inashuka. Sasa anataka kuirudisha kwenye mstari, unapinga. Alternative hautoi. Aaaaghh!
 
Prof yuko vizur... najiuliza tu swali moja, hivi ADVANCED DIPLOMA ilikufia wapi?, nini kiliiua na kwa nini ilikufa?
 
Sasa kama ulifauli form four alafu six ukafeli then ukapat diploma kwa kupitia form four hapo sijaelewa kama ntaweza endelea
 
Big up robert kiyosaki mwandishi wa rich dady, poor dady elimu bila pesa ni sawa na engine bila oil. Ogopa sana kuongozwa na mawazo yake na baba yake na robert kiyosaki utakuwa maskini maisha yako yote. Hivi wanaoongoza uchumi wa dunia hebu chukua ile top 10 ta forbes halafu njoo kwenye dhana yetu ya elimu tunayoipata darasani nadhani utapata jibu. Unaweza kuta tunazalisha watumwa(waajiriwa) na si waajiri(wajasiliamali) harafu tunajisifu na kufurahia utumwa. Elimu ya kweli ni elimu inayoweza kukusaidia kukabiliana na mazingira yako ukayamudu na kuzalisha fursa nyingi za maendeleo yako binafsi ya kiuchumi kijamii na kiutamaduni ambayo yana mchango chanya kwa taifa na jamii nzima. Hivyo elimu ya ngazi yeyote inakuwa na maana pale inapotoa matokeo chanya kwa maendeleo yako binafsi na jamii kubwa na si majivuno ya utumwa.
 
Hapa kuna shida kidogo. Angekuwa sawa kama angesema wanazuia mtu aliefeli form four kuendelea mpaka arudie mtihani na afaulu. lakini having equivalent of form six ni acceptable dunia nzima. Nadhani wakati umefika baadhi ya mambo ya elimu yaingizwe kwenye katiba ili watu wasiweze kuyabadili kirahisi namna hii jamani
 
Huyo waziri wenu inabidi aangalie mfumo wa elimu kwanza ndio atoe mawazo yake na sio kukurupuka bila kuandaa mazingira
 
Hapa kuna shida kidogo. Angekuwa sawa kama angesema wanazuia mtu aliefeli form four kuendelea mpaka arudie mtihani na afaulu. lakini having equivalent of form six ni acceptable dunia nzima. Nadhani wakati umefika baadhi ya mambo ya elimu yaingizwe kwenye katiba ili watu wasiweze kuyabadili kirahisi namna hii jamani
Kweli unachosema 100%
 
sasa Wale wadogo zangu shwafaa na Daudi nitawapeleka wapi jamani... daaaaaaaaaaaaaaah
 
Mwaka huu jinsi gear zinavyo badilishiwa angani yaani ni vigusuvigisu
 
Sijaona wala kusikia sehemu aliyosema kwamba waliosoma diploma hawatakiwi ku apply degree na kwamba huo utaratibu utaanza mwakani.

Mwaka huu tu iliwalazimu kushusha GPA 3.5 mpaka 3.0 maana asilimia kubwa ya diploma holders wasingejiunga vyuo vikuu, halafu leo hii waseme hawaruhusiwi kusoma degree bila kupitia advance?

They must be kiddin.. If its true
 
Next watasema ukifeli form four uhurusiwi kurudia masomo ili uendelee na high school, uzuri haka ka inji ketu akija waziri mpya atabadili na yeye kadri anavyojisikia..
 
Nchi zilizo ondelea kama mfano uk ,unaweza kujiunga na elimu ya juu bila ya kuwa na leaving certificate.

Ukishajua kusoma na ku andika ikiwa upo over 18 unajiunga na college, una anza na foundation mwaka mmoja, baadae level 1 kwenda 2,3 baadae degree, level hizi ni diploma.

Maelekezo zaidi angalieni mfano East Ham college
Unataja vyuo vya uchochoroni. UK hata vyeti feki vipo
 
Lakini amechelewa sana katika hili maana hata huko anakowapeleka wakiwa na credit za form six au four plus technician certificate wanaenda kufundishwa na ma lecturer waliopata degree kupitia utaratibu huu anaoukataa.

Ili afanikiwe inabidi afanye uhakiki wa sifa za PhD holders wote kujua walifikiaje level hiyo, waliopitia kuunga unga wasifundishe wenye credit za form six.

Tena amshauri hata mtukufu aondoe watunga na wasimamia sera wake wote wenye elimu ya kuunga unga ndipo ataipata elimu bora mpya Tanzania.
 
Back
Top Bottom