Ndalichako: Marufuku wasio na sifa kujiunga na masomo ya shahada kwa kupitia kozi za'foundation'

Weka video yote mleta mada.Mama anakataa mambo ya kufanya zile foundation course za mtu asiye na sifa ya kujiunga elimu ya juu(Hana diploma wala principal passes za A Level)

Maana yake ni kuwa kama upo kazini unataka kujiendeleza chuo kikuu huria,kama huna sifa huwezi kujiunga tofauti na zamani za foundation course
 
tuache kupotosha, prof kasema jambo la msingi haiwezekani mtu anaziro anaenda kusoma foundation course wiki tatu anadahiliwa chuo kikuu hapana, tusigeuze elimu kuwa biashara ya bodaboda.
Foundation course ni pure advanced jua hilo labda useme kuchukua d5 badala ya c3nashauri wangeongeza viwango vya ufaulu tu ila foundation kwa open ni mziki mzito
 
Go Go Go Profesa ule utani wa kudahili kwa kutumia masomo ya dini (Divinity/Islamic Knowledge kwenye kozi za shahada zisizo za dini) ukomeshwe.
 
Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi wasio na sifa kujiunga kujiunga na masomo ya Shahada (degree) kwa kupitia Foundtion Course, bila kupita kidato cha sita. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.


Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa.

"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza Ndalichako.

Unaweza kumsikiliza zaidi hapa:


Je, nini maoni yako? Unakubaliana na Ndalichako au unampinga?
 
Hakuna mtu anaejitaid kurudisha elimu yetu kwenye ubora wake kama waziri Ndalichako......
Elimu za hovyo, na digrii dhaifu zilijaa mtaani
Hata hivyo ulisikiliza hiyo clip hajasema hivyo..
Kwani lazima kila mtu aww na digrii?
Zamani digrii zilikuwa za vipanga tu, huko ndipo tunapotakiwa kwenda.
 
Hivi waziri anaweza kuwa proud kuwa ametengeneza mazingira mazuri kwa shule ZOTE kuwezesha watoto wenye sifa wafaulu sekondari?

Hivi waziri anaweza kututhibitishia kuwa maelfu ya wahutimu waliopitia mfumo wa o-level, - certificate - diploma - degree wana elimu duni kuliko waliopitia form V/VI?

Hivi waziri anaweza kututhibitishia kuwa mabadiliko haya anayotaka kuyaleta yapo supported na tafiti za kitaalamu?
 
Nchi zilizo ondelea kama mfano uk ,unaweza kujiunga na elimu ya juu bila ya kuwa na leaving certificate.

Ukishajua kusoma na ku andika ikiwa upo over 18 unajiunga na college, una anza na foundation mwaka mmoja, baadae level 1 kwenda 2,3 baadae degree, level hizi ni diploma.

Maelekezo zaidi angalieni mfano East Ham college
 
Mungu anatuona. Msimamo na mfumo wa elimu duniani ukoje tusije kuwa kisiwa cha ajabu kwa mifumo usiyoweza kutuvusha tulipo. Madocta walimu na engineer uzoefu ni muhimu kuanzia level za kati kisha degree na masters hadi PhD. Ngoja nifuatilie speech ya waziri ili nijue
 
Back
Top Bottom