Ndalichako: Marufuku wasio na sifa kujiunga na masomo ya shahada kwa kupitia kozi za'foundation'

Kwa hili naunga mkono 100%, Degree za CBE zilikuwa zinaongezeka. Bado la mafunzo ya ualimu kuwa chini ya Nacte, wataalamu wa elimu ya ualimu hawajawahi kuona ualimu kama technical education.Labda mie niliandaliwa vibaya ila mwenye maarifa na hili anielimishe.
 
Kwa hatua tuliyofikia hilo naona halina taabu.Tuna High schools nyingi ambazo zinaweza kutoa watu wa kuingia vyuo vikuu.

Tatizo ninaloliona ni hii hulka ya kuona kama mambo fulani yalifanyika kimakosa.Watanzania wanasahau kuwa miaka michache fursa zilikuwa chache na wengi ilibidi wapitie njia mbadala kabla ya kuingia vyuo vikuu.

Chuo Kikuu huria kimeanza na kimeendeleza watu wengi ambao hawakupata fursa ya kwenda conventional universities.

Kada mbalimbali zilianzishwa kukidhi mahitaji ya nchi lakini leo watu wanaona kama waliofanya vile ilikuwa makosa (Mwakyembe na mahakimu).

Ushauri wangu kwa Ndalichako ni kuwa wasikurupuke kwani with time kuna mambo yataphase out!!!
 
Yuko sawa...
Waziri safi sana. Anajitambua na zaid anafata misingi ya utawala bora kwa kusimamia sheria na taratibu tulizojiwekea.
Misingi ya tawala bora gani sasa??

Na Ww unasapoti??

Toa strong reason kwann na siyo kuitikia ndio tu.
 
Mungu anatuona. Msimamo na mfumo wa elimu duniani ukoje tusije kuwa kisiwa cha ajabu kwa mifumo usiyoweza kutuvusha tulipo. Madocta walimu na engineer uzoefu ni muhimu kuanzia level za kati kisha degree na masters hadi PhD. Ngoja nifuatilie speech ya waziri ili nijue
Nadhani Ndalichako hajamaanisha kwamba mtu asipitie certificate hadi degree anachomaanisha ni kuwa mtu aliyeshindwa kupata sifa za kuingia kidato cha tano azitafute kwanza na asome advanced level.
 
Kwa hili sasa ni kiboko ya yote. Nawahurumia vijana wetu wanaohangaika kusaka elimu popote Tanzania. Serikali yetu inataka sasa kuturudisha kule kule ambapo watoto wetu walipelekwa kusaka elimu Uganda na Kenya.
Ingawa ni ghali nashindwa kuelewa itakuwaje watoro wataosoma nje chuo kikuu na wakapata shahada zao wakiwa wameingia kwa ufaulu wa diploma. Je, serikali yetu haitatambua shahada hizo. Bila kupepesa macho nasema tunajitia aibu sisi wenyewe.
 
Misingi ya tawala bora gani sasa??

Na Ww unasapoti??

Toa strong reason kwann na siyo kuitikia ndio tu.
Kilichoandikwa hapo hakihitaji strong reasons kivile. Elimu ya chuo inajulikana ni kwa wale wanaojiweza kulingana na carrier zao... Wewe na division four yako unapitia chuo (diploma) then uende degree. Rudi ukarudie Form four kwanza.
 
Kwa system hii hata Sizonje(aliyeshindwa kujiunga na degree moja kwa moja akakimbilia kusoma diploma)angekuwa ana-reseat mpaka muda huu......mwaka huu tumepata leaders kwakweli
 
Back
Top Bottom