Ndaga, Malafyale Magufuli

Ndaga, Malafyale Magufuli

Ninavyojua ni Kuwa Population ya Mbeya kwa Vyombo vya Usafiri hata binadamu ni Kubwa Kuliko Moshi, Iringa na Pengine Hata Arusha, Lakini note huko wamewekew Double road.
Na nijuavyo najua hata hiyo ByPass itajengwe wakati wa Kupitisha Barabara Kuu itakayoendelea Toka Igawa kuelekea Tunduma, sasa nadhani hapo ndipo ilikuwa nafasi ya Utanua hata Barabara ili iwe na Njia nne!
Lakini kwaajili ya Chuki na Mbeya, Trust me hawatafanya hivyo ili kuwakomoa.
Mkuu kama ule mfuoa wa barabara za Tukuyu unatafunwa, huu wa doble way Mbeya utafanyika tu.
Ndo maana nasema its a matter of time.
 
Mkuu Lole Gwakisa, katika hili Nampongeza saana Magufuli, Ila haliwezi kunitoa Ufahamu eti ndiyo niseme CCM Imeanza Uzuri ghafla. Walikuwa wapi Muda wote huo uliyopita? Na hatutakiwi Kusahaua Kuwa Juhudi za Mwandosya pia Zimesaidia.

Ndagha Fijo Mwaisa, loli Jiwe akamundu Nnunu Fijo, ni Jambo la muda tu utaelewa Malafyale. Masopakyindi, Lusungo,Green City.
Mkuu viongozi wote si sawa, na ni jana tu hata Magufuli amesema hata yeye ana mapungufu.
Tuchukuliane kwa wema na kupendana.
Pale penye makosa tukosoane ili sote tusonge mbele.

Tukubali kuwa huko Tukuyu Magufuli katekeleza ahadi ambazo aliziweka, kwa hilo tumshukuru.
 
Nimewiwa kumpongeza sana Malafyale Rais, Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kukata kiu ya muda mrefu sana, ya ujenzi wa barabara za Katumba~Masebe~Lwangwa~Mbambo~Masoko~Tukuyu...
nasema Ndaga fijo na ubarikiwe sana Malafyale Dr John Pombe Joseph Magufuli.
Waliokuwa na nia mbaya wameumbuka, Magufuli amefanya ziara yenye mafanikio na amepokewa na wananchi wengi sana haijapata kuonekana Mbeya.
Mkuu mdogo wangu alivonipigia simu toka Busokelo, furaha yake niliisikia akitaka kulia kwa shukrani. Tumeteseka sana kwa barabara hizi za kwenda milimani, asante Magufuli.
Siye tunashukuru kwa matendo mema, naona roho yako inaomba laana ikutokee.
Unapo ahidi wananchi, ustaarabu ni kutekeleza. Pamoja na kuahidi kila kampeni ya urais kama ilani ya chama, sina kumbukumbu marais wetu ingakao kufika huko makwetu. Magufuli aliahidi, sasa anatekeleza. Ndaga Magufuli.
...sisi tunampongeza Magufuli kwa barabara hizi zilizotutesa miaka nenda rudi. Nakumbuka ndugu zetu waliofariki basi zima kwenye kilima kile baada ya kijiji cha Suma. Basi la Mwambipile liliua watu karibia 30. Lile genge basi lilipopinduka ni zaidi ya Kitonga, wengi wenu hamjapita njia hiyo, Rais kapita kajionea.
Mkuu hilo ni kweli kabisa, Mbeya bado ni ngome ya CCM. KUNA wanafiki hata ndani ya CCM wameumbuka walisema Mbeya kuna ukabila, ati wanamchukia Magufuli! Nyomi iliyojitokeza kumpokea Magufuli imewaumbua vibaya.
Duh! Njaa mbaya sana, hizo sifa! Kwa majaliwa ukumbukwe enzini... Kumbe huko Mbeya kuna wao na sisi! Nilidhani mkusanya kodi ni moja tu! Heri mlioambulia barabara, wapo walioambulia risasi za moto na wengine kuishia magerezani kama si kupoteza kabisa maisha!
 
Duh! Njaa mbaya sana, hizo sifa! Kwa majaliwa ukumbukwe enzini... Kumbe huko Mbeya kuna wao na sisi! Nilidhani mkusanya kodi ni moja tu! Heri mlioambulia barabara, wapo walioambulia risasi za moto na wengine kuishia magerezani kama si kupoteza kabisa maisha!
Simple minds mnafikiria njaa.

Tukuyu na Mbeya kwa ujumla hakuna njaa ya aina yoyote.

Tatizo ni maendeleo.

Bila kichocheo cha miundombinu bora, tatizo lililopo toka uhuru, maendeleo yatakuwa ndoto.

Naamini hujafika Mwakaleli, hivyo hujui kinachoongelewa hapa.
 
Mbeya tunajuwa ujenzi wa barabara ni kodi zetu. Ajenge ila siyo kigezo cha kutafuta kura.
 
Mbeya tunajuwa ujenzi wa barabara ni kodi zetu. Ajenge ila siyo kigezo cha kutafuta kura.
Tutampa kura tu kwa kutimiza ahadi.
Kuna walioahidi na kutotekeleza, hata kuja kushukuru tu hawakuja.
 
Back
Top Bottom