Nimewiwa kumpongeza sana Malafyale Rais, Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kukata kiu ya muda mrefu sana, ya ujenzi wa barabara za Katumba~Masebe~Lwangwa~Mbambo~Masoko~Tukuyu.
Nimepigiwa simu sasa hivi na mdogo wangu aliyeko Busokelo, akiwa amechanganyikiwa kwa furaha, kuwa ni Rais Magufuli aliye weka jiwe la msingi kufungua ujenzi wa barabara hiyo.
Hii imemtia simanzi kwa furaha.
Tukumbuke kuwa maraisi toka Mwinyi, Mkapa, Kikwete wote waliahidi kujenga barabara hizo lakini hawakuweza kutekeleza.
Hivyo kwa kutekeleza yale yeye mwenyewe alivyo ahidi, pamoja na ahadi za waliomtangulia, nasema Ndaga fijo na ubarikiwe sana Malafyale Dr John Pombe Joseph Magufuli.