Nchimbi na Kamala hawana PH.D

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
14,211
13,725
Imekwishadhihilika wazi kuwa Nchimbi na Kamala ambao ni naibu waziri na waziri respectively kwenye serikali ya muungwana kuwa hawa jamaa walikuwa na vyeti feki vya doctorate; hii imejionesha pale waliporegister upya na Mzumbe University kusomea shahada hizo. Swali langu ni kwanini vyombo vya habari, yaani magazeti,redio na TV bado wanawaita kuwa hawa jamaa ni "DR". Je inawezekana ikawa ni kwasababu ya uelewa mdogo wa hawa wanahabari wetu/ kuwa na makanjaja wengi? Ni kosa la jinai kutumia title ya uongo ili kujipata kipato!!
 
nakuunga mkono tatizo kwa sasa lipo kwa hawa baadhi ya waandishi wenye uelewa mdogo...
 
Hata Idi Amin alipojiita "His Excellency Al Hajj Field Marshall Dr Idi Amin Dada, VC, VSO, CBE, Lords of the Fishes of the Sea and the Beasts of the Earth, Conquerer of the British Empire in Africa in general and Uganda in particular", waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi walimwita hivyohivyo alivyotaka.

Na kuna wanasoka wa kibongo wamejiita majina yasiyo yao kama Cannavaro, Boban,etc na waandishi wamefuata mkumbo huohuo.

Hatupaswi kulaumu waandishi, kama kuna kosa aulizwe huyo aliyetoa taarifa ama utambulisho wa kimakosa kwa waandishi. Wao kazi yao ni kuripoti tu, wakikuuliza jina lako, lile utakalowapa ndilo watalotumia katika taarifa zao.
 
Mimi naona wanawataja kwa mazoea kwani tangia waanze kuitwa madokta ni muda mrefu, hivyo kuja kuzoea kuwaita tofauti na awali itachukua time.

Ila inabidi msisitizo uwekwe ili tuweze kuwataja kwa kile wanachostahili kwani academic titles sio za kuchezea jamani esp PhDs.
 
Hivi ile ya 'Dr Mzindakaya' nayo ni academic au ni ya kiaje? Halafu majuzi nimesikia Dr Karume na Dr Kikwete.
 
Hata Idi Amin alipojiita "His Excellency Al Hajj Field Marshall Dr Idi Amin Dada, VC, VSO, CBE, Lords of the Fishes of the Sea and the Beasts of the Earth, Conquerer of the British Empire in Africa in general and Uganda in particular", waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi walimwita hivyohivyo alivyotaka.

Na kuna wanasoka wa kibongo wamejiita majina yasiyo yao kama Cannavaro, Boban,etc na waandishi wamefuata mkumbo huohuo.

.

heheheeeeeeee..... hii kali!!!

Na kuna waganga wajadi wanaitwa dokta, professor nk.
 
mimi nina ugomvi na hawa wawili profesa jei na dokta remi ongala tafadhari sana wakatazeni.
 
Heheee kuna ka-Obama, B52, Mwalimu wa walimu, Diouf, etc.

Sasa Kamala na Nchimbi bado wanadeserve kuwa mawaziri iwapo CV zao lina invalid information?
 
Mimi nawasifu Wamarekani kwa jinsi wanavyo-handle suala la u-dr na u-prof. Hizi title wanazitunia tu pale wanapokuwa kwenye shughului za academic. Kwa mfano prof akiacha kufundisha akawa mbunge au mfanyabiashara, title ya prof au dr hazitumiki katika shughuli zake za siku hadi siku. Anakuwa ni mr tu. Akina Obama na Clinton usiwaone hivyo - wale ni maprof wa sheria!
 
kwani hamjui waandishi wetu wengi ni makanjanja au wanaishi kwa vibahasha vya hawa waheshimiwa vihiyo? sasa waache kuwaita madocta na maprof waone kama hawafi njaa! kwa taarifa mkuu wengine hutungiwa hizo nyazifa na hawa waandishi na kusambaza ktk jamii hatimaye jamii inamtambua mtu ana phd kumbe kihiyo
 
Back
Top Bottom