Nchimbi atengua uamuzi wa Polisi. Seriously? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchimbi atengua uamuzi wa Polisi. Seriously?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fitinamwiko, Oct 8, 2012.

 1. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]From Mwananchi, Monday, 08 October 2012 07:34 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  James Magai
  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ametengua uamuzi wa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Ilala (RCO) Duwani Nyanda, wa kujichukulia sheria mkononi na kutoa uamuzi ambao ulipaswa utolewe na mahakama.
  RCO Nyanda alijichukuli asheria mkononi kwa kutoa uamuzi nje ya mahakama kuhusiana na mgogoro wa umiliki wa gari aina ya Suzuki Escudo lenye namba za usajili T708 BZS, baina ya mfanyabiashara Said Kachenje, na mkazi wa Zanzibar, Mohamed Ismail.
  Gari hilo ambalo lilinunuliwa na Kachenje April mwaka huu, lilikamatwa na askari Polisi, kwa madai kuwa ni la wizi na kwamba ni mali ya Ismail.
  Kachenje ambaye anadai kuwa ana nyaraka zote halisi, licha ya kufunguliwa kesi ya wizi, hata hivyo baadaye RCO Nyanda aliamua kumkabidhi Ismail gari hilo, bila kufikisha kesi hiyo mahakamani.
  Hata hivyo, Waziri Nchimbi ameamuru gari hilo likamatwe na kurejeshwa katika kituo cha polisi wakati taratibu za kisheria zikifanyika kulipeleka suala hilo mahakamani ambayo ndio itakayoamua umiliki halali wa gari hilo.
  Katika barua yake ya Septemba 20, 2012 kwenda kwa Kachenje, iliyosainiwa na Kaimu Katibu wa Waziri, Nelson Kaminyoge, Waziri Nchimbi amesema kuwa uamuazi huo aliouchukua RCO haukuwa sahihi kwani ulipaswa kutolewa na Mahakama na si Polisi.
  “Kwa msingi huo, gari hiyo imeamriwa ikamatwe na kurudishwa kituo cha Polisi wakati taratibu za kisheria zikiendelea ili kulipeleka suala hilo mahakamani,” inasomeka sehemu ya barua ya Waziri Nchimbi.
  Waziri Nchimbi alilazimika kuingilia kati suala hilo, baada ya Kachenje kumwandikia barua ya malalamiko, akidai kuwa polisi wanafanya mpango wa kumdhulumu haki yake.
  Katika barua yake ya malalamiko kwenda kwa Waziri, Kachenje alidai kuwa alilinunua gari hilo April 19, 2012, kutoka kwa Suleiman Haji, baada ya kukutanishwa na madalali wawili, aliowataja kwa jina moja moja la Hamisi na Almasi.
  Alidai kuwa kabla ya kuingia mkataba wa ununuzi wa gari hilo alifanya uchunguzi wa umiliki wa gari hilo kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo alijiridhisha kuwa gari hilo limesajiliwa kwa jina la Suleiman Haji.
  “Tulifanya mkataba wa mauziano mbele ya Wakili Margaret Mngumi, na malipo na saini zote zilitiwa mbele yake kama Kamishna wa Viapo,” alidai Kachenje katika barua hiyo.
  Aliendelea kudai kuwa wakati akiendelea kulitumia gari hilo huku akitafuta mteja wa kulinunua, April 24, 2012 alikamatwa na askari polisi kwa maelezo kuwa gari hilo ni la wizi.
  Alidai kuwa aliwekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa muda wa siku tatu hadi alipowekewa dhamana na nduguzake, lakini akafunguliwa kesi na kuambiwa kuwa uchunguzi ulikuwa ukiendelea.
  Alidai kuwa Julai 24, 2012 alipigiwa simu na askari aliyejitambulisha kwa cheo na jina la Inspekta Benjamini, akimtaka apeleke nyaraka halisi za gari hilo.
  Hata hivyo, alidai kuwa alipeleka vivuli vya nyaraka hizo na akamwambia askari huyo kuwa nyaraka halisi ziko kwa wakili wake na kwamba alipotaka kujua sababu ya kutakiwa kupeleka nyaraka hizo, alimbiwa kuwa zinatakiwa ili jalada lipekekwe kwa mwanasheria wa Serikali.
  “Nilipata wasiwasi kuwa hapa kuna mchezo unataka kuchezwa dhidi yangu. Mheshimiwa Waziri, hofu yangu ilitimia tarehe 19 Julai, 2012, pale ambapo nilipita Kituo cha Polisi Kati na kukuta gari halipo,” alidai.
  Alidai kuwa baada ya kufuatilia, RCO Nyanda alimweleza kuwa gari hilo amemkabidhi mlalamikaji, baada ya kukamilisha upelelezi na kugundua kuwa ni mali yake halali.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Safi sana Nchimbi! Safisha hao Ngunguri wamezoea kubambikia watu kesi.
   
 3. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Safi sana kwa kumwandikia barua RCO? If i was Nchimbi, ningemsimamisha kazi RCO kwa kuvunja sheria,then uchunguzi wa kina wa mazingira ya gari kukabidhiwa kwa mlalamikaji.
   
 4. h

  herimimi Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waziri ametoa uamzi sahihi, lakini inabidi RCO achunguzwe kilichomsukuma kufikia maamzi aliyotoa. kuna jambo nyuma ya pazia!
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Hakuna harufu ya mulungula kweli hapo?


  Comrade Nchimbi hilo ni tone tu zama kabisa baharini ujionee mambo
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwenye wall ya mwananchi fb niliuliza Nchimbi ni hakimu???
   
 7. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Nchimbi amechukua mamlaka ya Jaji wa rufaa
   
 8. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nchimbi umechelewa sana, haya ndio maamuzi ya kila siku katika vituo vya polisi. Mkuu wa kituo anaamua kesi nyingi kuliko jaji mkuu; tena nyingine ni nzito. Nimewahi kushuhudia mkuu wa kituo akiwapatanisha mbakaji na familia ya mtoto alibakwa, ikalipwa fidia na jalada likafungwa. Hii ndio polisi ya Tz.
   
 9. peri

  peri JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  kumwandikia barua haitoshi, huyo RCO anapaswa awajibishwe.
   
 10. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Bado sijaona. Anayekiuka sheria na taratibu ni mtuhumiwa na mtuhumiwa anakamatwa na kuwekwa rumande. Kwa nini mpaka sasa huyo RCO hayuko rumande? THIS IS DOUBLE STANDARD, WHICH IS KILLING OUR NATION.
   
 11. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sijaelewa naomba kujua, kwani kuna utaratibu gani ambao unatumika kumfikia Waziri mtu akifanyiwa uonevu na Polisi?. Au ni Uswahiba tu umetumika hapo, maana tupo wengi tu wajeruhiwa wa uonevu Polisi.
   
 12. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Huyo RCO bado anadunda mtaani na cheo chake. Sasa Nchimbi amechukua maamuzi magumu yepi hapo?
   
 13. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  huyo rco bado yupo kazini?
   
 14. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kama kweli yeye ni muumini wa good governance mbona haku step down kwa mauaji ya aliyekuwa mhandishi wa habari Daudi Mwangosi?
   
 15. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  hao manjagu ndio zao walijua kabisa kuwa jamaa kalinunua kihalali ila walita kumdhurumu kiaina.hovyo kabisa.
   
Loading...