Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 550
- 786
Wanajamvi nimefuatilia kwa karibu Ziara zote mbili za Chama cha Mapinduzi zilizofanyika hivi karibuni,ya kwanza ni ile ya Mwenezi Mstaafu Makonda peke yake akiwa na Serikali aliyoita Back to Back na ya pili hii ya Nchimbi akiwa na Sekretarieti ya Chama.
Nilichokiona Binafsi Ziara ya kwanza ya Makonda iliyotawaliwa na Populism iliibua Mabaya mengi sana ya Serikali na kujenga Taswira kwamba Serikali haipo na hakuna inachokifanya,katika Ziara hii upande wa pili wa Mema ya Serikali au utekelezaji wa Ilani haukunadiwa kama yalivyonadiwa Madudu.
Kiuhalisia Kero haziishi popote hata kwenye Ngazi ya Familia bado zipo mtu akiamua kuibua anaweza kukutana na Familia ikaibuliwa kero ya chakula kibaya,baba kuchelewa kurudi n.k,Naamini hata yeye akikaa Miaka 10 Arusha akija Kiongozi wa Kariba yake kutoka juu anaweza kusikiliza Kero na akazipata akamfanyia kama alivyofanyia wenzake kwa tafsiri kwamba hata alivyokuwa Dar hakumaliza Kero.
Kwa Upande wa Ziara ya pili ya kina Nchimbi naona iko tofauti inaonyesha upande wa Pili wa Serikali kwamba kuna Mema na Mazuri yamefanyika mengi kuliko mabaya hivyo inastahili kupewa nafasi nyingine kuendeleza yale mazuri.
Kwa Wataalamu na Weledi wa Kisiasa hebu tusaidieni kudadavua,kisiasa hapa nani Bingwa na nani anafanya vizuri?Zingatia neno KISIASA.
Povu Ruksa.