POTOSHI Nchimbi amesema “unataka kuniteka kwa sababu nasema ukweli”?

POTOSHI Nchimbi amesema “unataka kuniteka kwa sababu nasema ukweli”?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Kumekuwa na video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook, ikidai kuwa inaonesha kauli inayohusishwa na makamu wa raisi , Emanuel Nchimbi, ikinukuliwa akisema:“Unataka kuniteka kwa sababu nasema ukweli ?
je ni upi ukweli wa kauli hii inayoambatana na video?



1776583284731.png
 
Tunachokijua
Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ni makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye awali alikuwa katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Akiwa katibu mkuu wa CCM Balozi Nchimbi, Aprili 13, 2024 alifanya ziara mkoani Katavi na kufanya mikutano kadhaa ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka viongozi wa chama hicho kukubali matokeo ya uchaguzi pindi yanapotoka na kuacha kutoa lawama zisizo na maana.

Mkutano huo ulikutanisha, Wajumbe wa Mashina na Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji na Miitaa, Viongozi wa Chama ngazi zote, Wazee mashuhuri, Viongozi wa Dini pamoja na Watendaji wa serikali ngazi zote na Taasisi zisizo za kiserikali.

Madai

Kumekuwapo na kipande cha video kinachosambazwa mtandaoni kikimuonesha Balozi Dkt. Nchimbi kikiwa ni sehemu ya hotuba yake ya Aprili 13, 2024 mkoani Katavi huku kikiambatanishwa na kichwa cha habari kinachosema 'Unataka kuniteka kwa kusema ukweli'

Je, ni kweli kauli hiyo ilitolewa na Balozi Nchimbi?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia marejeo ya video umejiridhisha kuwa kauli hiyo haikutolewa kabisa na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi katika hotuba yake ya Aprili 13, 2024.​
Back
Top Bottom