Nchi zetu zinaendeshwa kwa kubahatisha

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,672
1,814
Ukitazama Tanzania, licha ya kuwepo viongozi wengi ambao hawana track record ya mafanikio yeyote, sheria na mifumo inayotungwa pia haina hata chembe za realism kulingana na mazingira ya nchi na wananchi wake.
Nitachukua mfano wa bei za nyumba: makazi ni jambo la kwanza muhimu kwa mtu yeyote. Utakuta hata zile nyumba zinazojengwa na serikali, kwa makusudio yanayotangazwa dhahiri ya kuwasaidia watu wa kipato cha chini (kwa mishahara ya Tanzania ya kweli, hawa ni asilimia 98 ya civil servants), hakuna mtu wa kipato hicho anayeweza kununua hata mlango tu wa nyumba hizo.; sembuse nyumba yote!
Hili linamaanisha nini? Linamaanisha kwamba serikali inatoa 'carte blanche' kama Wafaransa wasemavyo )(kadi nyeupe, ruhusa isiyo mipaka) kuwa ni 'ruksa' kuiba, udokoziena ulaji rushwa katika njia ya kuwapatia makazi mema kwa familia yako.
Katika elimu ya falsafa tunasoma "kitu ambacho bila yake wajibu hautekelezeki, hicho pia kitakuwa ni wajibu" Kama wajibu wa kuipatia familia yangu decent accommodation haikamiliki bila ya kuiba....
Kwa kweli sera hizi za kubahatisha na zisizokuwa na mashiko katika hali halisi, ndiyo kichocheo cha kwanza cha uvunjaji wa sheria kwa wafanyakazi, na utovu wa nidhamu kwa ujumla.
Sijui wana sheria watatuambia nini: ikiwa mtu anaiba ili aipe familia yake maisha ya kawaida ya binadamu wa sasa, si zaidi ya hapo.... hukumu yake ni nini? Hasa baada ya kufahamu serikali yenyewe ndiyo iliyoahidi hivyo.
Haya ndiyo masuala ya kushughulikiwa kwanza badala ya kuanza na bomoabomoa au kufukuza wageni. JMP's priorities are extremely misplaced!
 
Viongozi wetu wengi wanataka madaraka wakishayapata hawajui wayafanyie nini Dull Professors according to trump
 
Back
Top Bottom