Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,681
- 46,369
Hizi ndizo nchi zenye majeshi yanayofanya biashara na kumiliki sehemu kubwa ya uchumi wa nchi wa nchi zao. Hizi nchi ukitaka biashara zako binafsi zikuendee vizuri inabidi utafute koneksheni na "godfathers" wajeda.
1. Misri
Jeshi la Misri lina mkono mrefu sana katika uchumi wa nchi hiyo. Linamiliki mahoteli makubwa, kumbi za starehe, viwanda vya cement, vyakula na bidhaa nyingine za kawaida, biashara za real estates na biashara kubwa ya silaha.
2.Pakistan
Jeshi la Pakistan lina ukwasi unaotokana na uwekezaji na biashara za kila aina nchini humo. Inakadiriwa maslahi yake ya biashara katika nchi yanaweza kufika dola billion 20.
3.Sudan.
Jeshi na wanamgambo nchini Sudan wanakadiriwa kuchangia zaidi ya asilimia 50 katika uchumi wa nchi hiyo kutokana biashara za mafuta, dhahabu, real estates na bidhaa nyingine za kawaida
4.Algeria
Nchini Algeria jeshi lina maslahi mapana katika sekta muhimu kama mafuta na nyingine nyingi na linahusika pakubwa kuamua sera za uchumi nchini humo.
5. Myanmar
Jeshi nchini huko ambapo ambako limekuwa likitawala nchi wakati wote na kupelekea vikawazo vikali vilivyoifanya nchi hiyo kuwa kama Zimbabwe ya Asia linafaidika pakubwa kupitia biashara za rasilimali za madini, maliasili na mihadarati ya Opium.