Nchi zenye Dhahabu nyingi zaidi duniani

Nchi zenye Dhahabu nyingi zaidi duniani

Mimi nasema shida ni wao sio sisi, kwasababu wao ndio chanzo Cha machafuko kwenye kila nchi yenye rasilimali wanayoitaka Africa pindi anapotokea kiongozi mzuri wa kuwapinga tu basi tegemea taifa hilo litaingia kwenye machafuko makubwa kisha mali zote kukombwa.

Mfano Mzuri ni hapo tu Congo walipoona Lumumba hadanganyiki haraka sana wakamuua Kisha kuweka puppet wao Mobutu na vikundi vya waasi kibao huku wao wanajizolea madini yote.
Yaani Africa akipatikana tu kiongozi mzuri wa kusimamia masilahi ya waafrica basi lazima tu atapata msuko suko mkubwa wa kutengenezwa kwa makusudi kabisa.

Washatujua wajinga why Mobutu akubali kuwa puppet? Shida ni sisi na si wao, kama tungekuwa na umoja mzungu asingesogea ila wanatujua tunapenda matumbo mtu yuko tayari auze nchi kisa tumbo lake tukiamua kwa umoja wetu tunaweza kwani wao nani?
Na hata wakiamua kutuua unafikiri watatumaliza? Tukiamua kuwa wamoja wataogopa ila ndio washatusoma wakaona nguvu nyingi za kupigana akili kisoda
 
Wao wanatusaidia kupigania democracy na kutusambazia silaha ili tuasi nchi zetu (silaha zenyewe ni outdated technology) kisha sisi tunawaachia migodi wanachimba dhahabu ndio maana wanazo nyingi kuliko sisi mkuu.
Kama ndo hivyo basi viiongozi ambao tunao ni ma_bogus kabisa
 
Nchi zilizo na akiba mingi ya dhahabu

1 United States - 8,133.46 T
2 Germany - 3,363.60 T
3 IMF -. 2,814.04 T
4 Italy - 2,451.84 T
5 France -. 2,436.01 T
6 Russian Federation - 2,299.87 T
7 China - 1,948.31 T
8 Switzerland - 1,040.00 T
9 Japan -. 765.22 T
10 India - 657.67 T
11 Netherlands - 612.45 T
12 Turkey - 583.00 T
13 ECB. - 504.77 T
14 Taiwan - 422.69 T
15 Portugal - 382.54 T
16 Kazakhstan - 378.48 T
17 Uzbekistan - 342.76 T
18 Saudi Arabia - 323.07 T
19 United Kingdom - 310.29 T
20 Lebanon - 286.83 T

View attachment 1541700
hata hii Lebanon ambayo ina uchumi mbovu kiasi kwamba utoaji wa fedha atm ulikuwa restricted kwa week kiasi fulani? alafu sisi tanzania atupo na niwazalishaji wakubwa tu africa kwa gold
 
WaLebanon wengi ndio madalali wa vito vya thamani ,hivyo vingi vinaishia kwenye makabati yao
hata hii Lebanon ambayo ina uchumi mbovu kiasi kwamba utoaji wa fedha atm ulikuwa restricted kwa week kiasi fulani? alafu sisi tanzania atupo na niwazalishaji wakubwa tu africa kwa gold
 
mkuu kwa kiswahili chepesi ni kwamba. haitazamiwi dhahabu kushuka thamani hata kidogo, maana matumizi ni makubwa kuliko upatikanaji wake, ndio sababu watu hawasiti kuihifadhi kuliko kuitumia.

matumizi yake ni.

1,urembo
2,utengenezaji wa nyenzo za kielectronic, kama vifaa vya simu na computer.

almas

1,urembo
2,mashine na mitambo ya kukatia vitu vigumu, kama chuma na miamba nk.



Sent from my G3226 using JamiiForums mobile app
Hii sio kweli kabisa, dhahabu haitumiki kutengeneza sijui nyenzo za elektroniki na vifaa vya simu na computer. Kasome tena vizuri.
 
hata hii Lebanon ambayo ina uchumi mbovu kiasi kwamba utoaji wa fedha atm ulikuwa restricted kwa week kiasi fulani? alafu sisi tanzania atupo na niwazalishaji wakubwa tu africa kwa gold
Mfinyanzi hulia gaeni.
 
Hii sio kweli kabisa, dhahabu haitumiki kutengeneza sijui nyenzo za elektroniki na vifaa vya simu na computer. Kasome tena vizuri.
unawaza kusoma tu, hujamaliza bado??? wengine tuliishamaliza tunafanya mambo mengine[emoji116][emoji116][emoji116]

unajua hii michirizi ya njano ni kitu gani au unadhani ni rangi rangi tu zimepakwa kwa brush ya rangi ya kucha.
images.jpg


Sent from my G3226 using JamiiForums mobile app

na kama una bundle jifunzie hapo
 
Sasa Afrika tungekuwa tuna hifadhi dhahabu si ingetusaidia sana hasa ukizingatia currency za Afrika hazipo stable..
Utawezaje kuhifadhi dhahabu wakati huwezi hata kugharamia kuichimba. Yaani kwa mfano umepata mgodi,umewekeza pesa ya utaalam na mitambo..Then uichimbe bila kuiuza popote lkn uweze kulipa mishahara,kukarabati na kununua mitambo mipya kila inapohitajika bila kuuza dhahabu yako.

Kwa kifupi uhifadhi wa dhahabu unatokana na uwezo wako kiuchumi.

Na dhahabu ni substute ya fedha una sio kitu kingine chochote .Ukiwa na fedha una dhahabu na ukiwa na dhahabu una fedha.
 
Mala zote ukiwauliza watu hua wana blaa blaa mingi sana kuhusu kazi ya dhahabu au almasi, mala ooh inatengenezea siraha, mala ooh kwenye ndege kuna madini wanayotumia, watu hawa wote hua hawana uhakika na kinachojulikana kazi kubwa ya dhahabu ni vidani tu vya kuvaa vaa hivi ambavyo siamini kama vinaweza kurudisha gharama ya uchimbaji ambayo hua ni kubwa nasa,

Yamkini kuna siri zao zilizo jificha au ni kitu tu cha thamani kinachokaa kwenye mabenki na ghala za kuhifadhi thamani ya muhusika anazo miliki, labda
Mala,au Mara?🤔
 
Wao wanatusaidia kupigania democracy na kutusambazia silaha ili tuasi nchi zetu (silaha zenyewe ni outdated technology) kisha sisi tunawaachia migodi wanachimba dhahabu ndio maana wanazo nyingi kuliko sisi mkuu.


Sasa si uone sisi ni wapumbavu!
 
Dhahabu ina thamani ya kihistoria na imekuwa juu kwa sababu, kwa miaka mingi sana imetumika kama "store of value" na watu wamejaribu kuitengeneneza kwenye lab wakashindwa. Hivyo pure gold ina a measure of authenticity. You just can't fake it, as in create it in a lab.

Ukisoma historia ya Chemistry, enzi za Alchemy, watu walijaribu kila njia kutengeneza dhahabu wakashindwa.

Na hii inatokana nabsababu kubwa mbili. Kwanza, dhahabu hai react na vitu vingine. Pili, namna pekee ya kuitengeneza dhahabu ni kutumia nuclear reactions zenye nishati kubwa sana kiasi gharama za kuitengeneza hiyo dhahabu zitaizidi thamani ya dhahabu itakayotengenezwa. Hivyo hiyo itakuwa biashara kichaa. Dhahabu tuliyonayo ilitengenezwa katika nuclear reactions katika nyota mbalimbali ambazo ziliishia katika kupasuka kwenye supernovae.

Tabia hizi mbili za dhahabu za kuto react na vitu vingine (ukilinganisha na kitu kama chuma kinacho oxidize na kupata kutu), pamoja na kutoweza kutengenezeka kwenye lab, pamoja na thamani ya kihistoria kama "store of value" (kihistoria fedha zilihesabiwa kwa dhahabu na chumi nyingi za dunia zilitumia "the gold standard" mpaka karne iliyopita.

Kuna mengi mengine ambayo yanahusika, lakini kwa uchache kabisa hayo ni ya muhimu.
- Uko sahihi, except hapo ulipoandika dhahabu haireact na vitu vingine.

- Dhahabu inareact na halogens na kutengeneza complex compounds. Hydrothermal gold deposits zinatengenezwa baada ya dhahabu kuprecipitate from solution.
 
Back
Top Bottom