Nchi yetu imeshakuwa ‘Taifa la Propaganda’

field marshall1

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2017
Posts
1,594
Reaction score
3,606
Nilisoma kwenye gazeti la Kiswahili kuwa gavana wa Banki kuu Prof. Florens Luoga akisema uchumi wetu unakua vizuri na tuna akiba kubwa ya USD 5.0 Billions na hii itatosha kuendesha nchi kwa miezi mitano bila ya nchi kukusanya kodi au watu kufanya kazi, siku hiyo hiyo Rais Magufuli akatamka maneno hayo hayo.

Ninamfahamu Prof. Luoga kama mwalimu wangu na mkuu wa Chuo wakati nikisoma, nilimuona kama mtu mwenye credibility kubwa kwenye jamii ila kilichonishangaza aidha kwa kutojua au kwa makusudi alinishangaza aliposema kuwa hiyo akiba ya fedha za kigeni ni kubwa kuliko akiba ya nchi za Africa Mashariki! Ilishangaza sana.....

Sikutaka kushangaa zaidi hivyo nilienda kwenye website ya Central Bank of Kenya na kuangalia reserve ya siku hiyo.

Kifupi tu ni kwamba hatujawahi kuwa na akiba kubwa ya pesa za kigeni kuishinda Kenya kwa sababu Kenya wana tax base kubwa na kodi zao zinalipika tofauti na kwetu ambapo ni wachache tu wanaolipa kodi lakini wanakamuliwa kodi kubwa zisizolipika.

Namwelewa Dr. Patrick Ngugi Njoroge (Gavana wa Central Bank of Kenya) kama mtu makini sana, mchumi mzuri wa IMF, si hivyo tu huyu gavana pia kwa kiasi kikubwa aliaminika na Umoja wa Mataifa hadi kuchaguliwa mwenyekiti wa U.N Task force ya mambo ya Digital Financing ya SDG mwaka jana akiwa bado Gavana...Ningeweza kumfananisha na Prof. Assad kwa uchapaji kazi wake au kama Prof. Benno Ndullu kabla ya kuchanganya professional yake na siasa!

Wakati gavana wetu, Prof. Luoga mwalimu wangu wa Tax Law akisema tunayo akiba kubwa ya kutosha miezi mitano bila kufanya kazi ya USD Billions 5.0 niliamua kucheki akiba waliyonayo wenzetu wa kaskazini kwetu, Kenya. Akiba waliyonaya Kenya kwenye Banki kuu yao ilikuwa USD. 8.8 Billions na haijawahi kushuka kufika Billioni 7 au chini, sisi akiba yetu ya miezi mitano haijawahi kuvuka USD 5.8 Billions kwa kipindi tajwa sasa leo professor wa Tax Law na gavana wa banki kuu atasema vipi kitu ambacho si sahihi??? Leo tutamwamini vipi mtu kama huyo? Hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kushindwa kujua ipi ni kubwa kati ya 5 na 8.8!
Je ni utamaduni wetu kudanganya?

Katika kipindi hiki tangu aingie rais Magufuli mbona Propaganda zimekuwa nyingi...Kuna kitu wanaficha au wanataka wasifiwe hata kama hawastahili sifa? Sijasema wakati wa Kikwete hakukuwa na hizi propaganda, la hasha zilikuwepo ila hazikuwa nyingi hivi na za kijinga jinga kama za wakati huu, Sishangai kusikia rais mwenyewe alijifanya kushangaa kutekwa kwa Mo Dewji na wazungu wabantu na sarakasi nyingi na maigizo mengi yaliyofuata baadaye.

Ukienda Youtube utakutana na propaganda za akina Musiba anachoongea hakina sense ila ni comedy...Akili ndogo zinazoendelea kumtuma akaongee senseless zinashangilia. Akitukana, kuchafua wengine, kuropoka nk kwa hao anaonekana shujaa. Kweli Taifa letu limepotea!

Mambo madogo madogo ya “Dr. Shika” yanapewa kipaumbele.......watu wanasahau mambo ya msingi kuhusu maisha ya watanzania. Madawa hayapo, yaliyopo aidha yameisha muda wake au hayafai kwa matumizi ya binadamu (Refer: Report ya CAG), bajeti ya afya imetekelezwa kwa asilimia chini ya 40, bajeti ya dawa kwa asilimia 16. Wao wanapelekwa India, Africa kusini na nchi nyingine vipi Watanzania kama mimi na wewe ambao baba na babu zetu hawakuwa na nafasi serikalini....Si tutaishia hospitali za wilaya ambazo kwanza kulazwa hapo unatoka na ugonjwa mwingine, badala ya kupona unapata magonjwa mengine? Ni nini kinashindwa kuboresha huduma za afya angalau zikafanywa universal, tukose mengine yote lakini tuwe na haki ya kuishi?

Nchi ni yetu sote, Watanzania tuna akili za kuweza kutambua tunakoelekea, leo hii uchumi wetu unaenda kwenye asilimia 4 kutoka 7.2% halafu watu na akili zao watakwambia ni kitu cha kawaida kwa vile hata Marekani uchumi wake unakua kwa asilimia 2....Kweli hata akili za utambuzi mdogo tu hakuna? Ni wapi wamesikia uchumi wa nchi za dunia ya kwanza unakuwa kwa asilimia 7? wasomi wetu wanashindwa kuelewa hata hilo..Ndiyo maana wajenzi wa TBA kwenye hosteli za Chuo Kikuu walisema kuwa eti ile mipasuko ya kuta Expansion joint.....Sawa ni expansion joint sasa ilikuwaje mlikimbilia kuziziba?

Inabidi tuangalie kama elimu yetu inatosha na inasaidia kunyanyua taifa letu maana yanayofanyika sasa yanashangaza.
 
Ngoja waje vijana wa Lumumba uone watakavyokuzodoa...

Viongozi wetu wako bize na kina Piere Konki kujiweka juu kileleni... afu mtu makini kama Prof Assad anaonekana si lolote...

Wabunge wetu makini ndo kina Msukuma na Lusinde.... Aliyetuloga sijui kajificha wapi.
 
Ni kweli mkuu nchi yetu imejaa propaganda za kishenzi sana kuanzia watu wa kawaida mpka viongozi, uongo uongo kila mahali hii hua inanikera sna yan mfano tu kwenye daladala konda anakwambia ingia ukae siti zipo za kutosha ukiangalia hakuna siti na watu kibao wamesimama yaan upuuzi upuuzi mwingi.

Na hii inarudisha nyuma maendeleo ya taifa hasa inapofanyika kwenye mambo ya msingi ya taifa.

Hakuna uwazi kabsa siku hizi.
 
Tanzania exported $5.3B and imported $8.17B, resulting in a negative trade balance of $2.88B.
source https://atlas.media.mit.edu/en/profile/country/tza/

Kenya exported $6.17B and imported $17.1B, resulting in a negative trade balance of $11B
Source https://atlas.media.mit.edu/en/profile/country/ken/

Tanzania tourism receipts were 2.157 USD bn in 2016
Source https://www.ceicdata.com/en/tanzania/tourism-statistics/tz-international-tourism-receipts

Kenya's Tourism Revenue reached 2 USD bn in Dec 2016
Source https://www.ceicdata.com/en/indicator/kenya/tourism-revenue

Not good but Tanzania credit rating according to Moody's is B1
Source https://www.reuters.com/article/tan...dys-for-negative-rating-outlook-idUSL5N1QN4U8

Even worst is the Kenyan credit rating given by the same agency (Moody's) B2
https://www.ft.com/content/c145f044-16f5-11e8-9e9c-25c814761640
..........................................................................................................................................................................................................

That is to say ingawa wote Tanzania na Kenya hoe hae, hila Tanzania is more financial stable kushinda Kenya all the indicators shows that.
 
USA ina current account balance ya mwisho duniani ipo namba 206 lakini uchumi wao wai kwanza duniani, sisi yetu ni nzuri lakini uchumi wetu ni hohehahe. Kenya wako chini yetu lakini wana uchumi mzuri ndiyo maana wao GDP yao ipo USD 98 Billions, sisi yetu ni USD 56 Billions na hatusogei mbele kwa vile Growth rate yetu imekuwa estimated kuwa ndogo kwa mwaka huu na mwaka ujao, kwa hiyo hata tu-rebase ukuaji wa uchumi bado hatutakwenda mbali.
 
Unaweza kuitwa Bungeni au Ikulu kujieleza kwa kuidhalilisha nchi kuwa ni ya PROPAGANDA
badilisha kauli tafadhali au PROPAGANDA ni neno la KIUCHUMI?
 
Nilisoma kwenye gazeti la Kiswahili kuwa gavana wa Banki kuu Prof. Florens Luoga akisema uchumi wetu unakua vizuri na tuna akiba kubwa ya USD 5.0 Billions na hii itatosha kuendesha nchi kwa miezi mitano bila ya nchi kukusanya kodi au watu kufanya kazi, siku hiyo hiyo Rais Magufuli akatamka maneno hayo hayo.

Ninamfahamu Prof. Luoga kama mwalimu wangu na mkuu wa Chuo wakati nikisoma, nilimuona kama mtu mwenye credibility kubwa kwenye jamii ila kilichonishangaza aidha kwa kutojua au kwa makusudi alinishangaza aliposema kuwa hiyo akiba ya fedha za kigeni ni kubwa kuliko akiba ya nchi za Africa Mashariki! Ilishangaza sana.....

Sikutaka kushangaa zaidi hivyo nilienda kwenye website ya Central Bank of Kenya na kuangalia reserve ya siku hiyo.

Kifupi tu ni kwamba hatujawahi kuwa na akiba kubwa ya pesa za kigeni kuishinda Kenya kwa sababu Kenya wana tax base kubwa na kodi zao zinalipika tofauti na kwetu ambapo ni wachache tu wanaolipa kodi lakini wanakamuliwa kodi kubwa zisizolipika.

Namwelewa Dr. Patrick Ngugi Njoroge (Gavana wa Central Bank of Kenya) kama mtu makini sana, mchumi mzuri wa IMF, si hivyo tu huyu gavana pia kwa kiasi kikubwa aliaminika na Umoja wa Mataifa hadi kuchaguliwa mwenyekiti wa U.N Task force ya mambo ya Digital Financing ya SDG mwaka jana akiwa bado Gavana...Ningeweza kumfananisha na Prof. Assad kwa uchapaji kazi wake au kama Prof. Benno Ndullu kabla ya kuchanganya professional yake na siasa!

Wakati gavana wetu, Prof. Luoga mwalimu wangu wa Tax Law akisema tunayo akiba kubwa ya kutosha miezi mitano bila kufanya kazi ya USD Billions 5.0 niliamua kucheki akiba waliyonayo wenzetu wa kaskazini kwetu, Kenya. Akiba waliyonaya Kenya kwenye Banki kuu yao ilikuwa USD. 8.8 Billions na haijawahi kushuka kufika Billioni 7 au chini, sisi akiba yetu ya miezi mitano haijawahi kuvuka USD 5.8 Billions kwa kipindi tajwa sasa leo professor wa Tax Law na gavana wa banki kuu atasema vipi kitu ambacho si sahihi??? Leo tutamwamini vipi mtu kama huyo? Hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kushindwa kujua ipi ni kubwa kati ya 5 na 8.8!
Je ni utamaduni wetu kudanganya?

Katika kipindi hiki tangu aingie rais Magufuli mbona Propaganda zimekuwa nyingi...Kuna kitu wanaficha au wanataka wasifiwe hata kama hawastahili sifa? Sijasema wakati wa Kikwete hakukuwa na hizi propaganda, la hasha zilikuwepo ila hazikuwa nyingi hivi na za kijinga jinga kama za wakati huu, Sishangai kusikia rais mwenyewe alijifanya kushangaa kutekwa kwa Mo Dewji na wazungu wabantu na sarakasi nyingi na maigizo mengi yaliyofuata baadaye.

Ukienda Youtube utakutana na propaganda za akina Musiba anachoongea hakina sense ila ni comedy...Akili ndogo zinazoendelea kumtuma akaongee senseless zinashangilia. Akitukana, kuchafua wengine, kuropoka nk kwa hao anaonekana shujaa. Kweli Taifa letu limepotea!

Mambo madogo madogo ya “Dr. Shika” yanapewa kipaumbele.......watu wanasahau mambo ya msingi kuhusu maisha ya watanzania. Madawa hayapo, yaliyopo aidha yameisha muda wake au hayafai kwa matumizi ya binadamu (Refer: Report ya CAG), bajeti ya afya imetekelezwa kwa asilimia chini ya 40, bajeti ya dawa kwa asilimia 16. Wao wanapelekwa India, Africa kusini na nchi nyingine vipi Watanzania kama mimi na wewe ambao baba na babu zetu hawakuwa na nafasi serikalini....Si tutaishia hospitali za wilaya ambazo kwanza kulazwa hapo unatoka na ugonjwa mwingine, badala ya kupona unapata magonjwa mengine? Ni nini kinashindwa kuboresha huduma za afya angalau zikafanywa universal, tukose mengine yote lakini tuwe na haki ya kuishi?

Nchi ni yetu sote, Watanzania tuna akili za kuweza kutambua tunakoelekea, leo hii uchumi wetu unaenda kwenye asilimia 4 kutoka 7.2% halafu watu na akili zao watakwambia ni kitu cha kawaida kwa vile hata Marekani uchumi wake unakua kwa asilimia 2....Kweli hata akili za utambuzi mdogo tu hakuna? Ni wapi wamesikia uchumi wa nchi za dunia ya kwanza unakuwa kwa asilimia 7? wasomi wetu wanashindwa kuelewa hata hilo..Ndiyo maana wajenzi wa TBA kwenye hosteli za Chuo Kikuu walisema kuwa eti ile mipasuko ya kuta Expansion joint.....Sawa ni expansion joint sasa ilikuwaje mlikimbilia kuziziba?

Inabidi tuangalie kama elimu yetu inatosha na inasaidia kunyanyua taifa letu maana yanayofanyika sasa yanashangaza.
Tumeamua au niseme imeamuliwa, kwamba ujinga, ubabe, uongo, ufisadi, fitina na gilba ni mambo ya kawaida na ndio nyenzo ya mamlaka tusitegemee zaidi au tofauti na tunachokipata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada nashukuru umetoa vitu vizuri. Mimi naongeza kidogo tu baya kuliko lote kuwa na reserve nchi yoyote ni kitu cha lazima na sijui kila mara wa kiongelea hilo wanataka watu wajue nini au tufaidike na nini? lazima ajue hapo katika akiba ipungue 0.5 tu billion aone Tsh itaenda wapi, ni aibu kwa kweli kusikia mtu kila mara sio mara moja kuwa tuna akiba ya miezi 5 tuko vizuri. tuache propaganda katika mambo ya uchumi tufanye siasa tu number hazidanganyi. mfano mwepesi ni kuwa baba anafanya kazi na ana save kiasi inafika kipindi kasave sawa na kiasi cha mshahara wake wa miezi 5 halafu siku kafukuzwa kazi unadhani atafanya nini na akiba yake. ataanza kutumia akiba na zaidi maisha ya nyumbani yataanza kuwa mabaya watoto itabidi watoke private kama wako huko na kama ilikuwa kila siku kuku basi mwendo wa kisamvu na watapunguza kila kitu na kwa Mangi hakopesheki tena ni shida. sasa kuwa na akiba sio kitu cha ajabu ni kitu cha lazima hata katika level ya kifamilia. ukiona huweki akiba kinachoingia unatumia basi ujuwe uko katika shida la kufanya kupunguza matumizi hata kama itakubidi kuhama nyumba ya umeme kwenda isiyokuwa na umeme.
 
USA ina current account balance ya mwisho duniani ipo namba 206 lakini uchumi wao wai kwanza duniani, sisi yetu ni nzuri lakini uchumi wetu ni hohehahe. Kenya wako chini yetu lakini wana uchumi mzuri ndiyo maana wao GDP yao ipo USD 98 Billions, sisi yetu ni USD 56 Billions na hatusogei mbele kwa vile Growth rate yetu imekuwa estimated kuwa ndogo kwa mwaka huu na mwaka ujao, kwa hiyo hata tu-rebase ukuaji wa uchumi bado hatutakwenda mbali.
Kutangulia sio kufika if anything Kenya walitakiwa wawe mbali asilimia kubwa ya viwanda walivyoachiwa na mkoloni bado vipo, (kutokana na vigezo vya inflow and outflow ya uchumi, hizo ndio advantage pekee walizonazo zidi yetu). Unlike us tulivyojenga tumeshaua kwa ivyo walikuwa wana advantage ni sawa na kuanza mashindano ya mita mia mwenzako kasimama mita ishirini mbele halafu mjifananishe.

Lakini kwa sasa tunakwenda indicators zote sahihi zipo upande wa Tanzania, pamoja na changamoto za nchi ambazo kuna mijitu kila siku inakimbiza potential investors kwa maswala ambayo hayana kichwa wala miguu na washauri ambao utaalamu wao una mashaka.

Lakini hili aliondoi ukweli raisi anapambana kwa upande wake na yeye si mtaalamu kila sehemu, mtu yeyote makini alijua hatua za awali za serikari ya tano zitaathiri ukuaji wa uchumi mbeleni, yale yalikuwa maamuzi ya wataalamu kwa mujibu wa nafasi zao. Na walipokuwa wanaanza tu sie tuliokuwa tunapiga makelele December 2015 what will happen mbeleni ndio tunaonekana waropakaji with time watajifunza unaona kabisa wanaanza kuwa waoga wanaonza ni swala la kurudisha investment confidence za ndani bila ufisadi maana nalo lilikuwa tatizo.

Lakini by any means Tanzania ina stability ya foreign currency kushinda Kenya kilichokesana hapo ni kujua kiasi cha FDI kilichopo kati yao na kwetu lakini kwa data za inflow and outflow za uchumi we are better off na lenders wanatuweka sisi juu ya Kenya in terms of stability ya kulipa madeni yetu.
 
Back
Top Bottom