Bila shaka Kama watu waliofariki wanaweza kuona yanayoendelea Duniani na wakaumizwa au wakafurahia Basi Nina hakika Mwl Nyerere anapita katika maumivu ya ajabu kuliko ugonjwa uliomtoa duniani!
Taifa ambalo aliliacha likiwa na sifa ya utulivu na ustaarabu limekuwa ni Taifa la ajabu Kabisa, imekuwa ni sehemu ya kutekana bila aibu, matukio yanajirudia huku vyombo vya dola vikiishia kutoa sababu za nyepesi kwamba wanakiteka wenyewe. Taifa ambalo Sasa watu wote wanaishi kwa hofu kubwa si wananchi wa kawaida, watumishi wa Serikali, maskini kwa matajiri wanahisi wako kwenye nchi iliyokuwa ya Idi Amini.
Leo wako watu wanaweza kusema wanachotaka hata Kama ni Cha hovyo lakini vyombo vya dola ni Kama haviwasikii, lakini masikio yao yanasikiliza vilio vya wenye haki na hao ndio wanachukuliwa hatua kwa kuusema ukweli!!
Vyombo vya Serikali vinafanya dhuruma mchana kweupe bila aibu!! Msajili wa vyama Sasa ni wazi bila kificho anafanya kazi ya CCM, tume ya uchaguzi ni Kama wanaandaa makaburi ya kuwazikia Watanzania. Wenye hekima hawasemi!!
Waliokuwa wakijinasibu kuwa wanafahamu farsafa za Mwalimu wamezigeuka hekima za Mwalimu, sasa bila aibu wanatumikia matumbo yao kwa hofu zao. Hatukuzoeshwa uhuni huu, Sasa inatugharimu!