NAMELES LANDABU
Member
- Nov 7, 2016
- 9
- 3
Watu ni mimi na wewe . Watu ni wao , wale , hao na hata yule. Hivyo, kwa pamoja kila mwanajamii ni mtu.
Watu na jamii au watu na utaifa
Ifahamike kwamba hakuna jamii yenye mtu mmoja na ikaweza kusimama imara wala hakuna jamii yenye watu wawili ama watatu ama hao wachache nayo ikasinama kidedea.
Kumbe kunahitajika watu yaani mimi, wewe ,wao ,hao, wale ,yule na yeye ili tuweze kuwa na jamii moja, taifa moja lenye nguvu.
Naomba ifahamike kuwa watu ni mamlaka isiyo na mashaka ndani yake.
Watu na uchu
Ugumu wa mambo hapa ndipo unapokuja kuanzia , kukuta wale au mtu yule kuweka kusudi lake mbele ya watu waliounda jamii moja akitaka wafuate vile yeye anataka eti kisa mkononi mwake ameshikilia mamlaka ya watu wake, watu wale miongoni mwa watu wa jamii
Hili haina tofauti na hili jambo la hawa kutaka kikubwa au kuwa na sauti zaidi kuliko wale ndani ya jamii moja
Mfano mzuri ni pale utakapowaona ndugu wale wa kaskazini kutaka madaraka ya kuwatawala watu wa kusini kwa ya matakwa yao waliojiwekea bila kujali misingi ya jamii nzima iliyopo na kutupilia mbali matakwa ya watu wa jamii yote.
Si ajabu utamuona mtu akisema na watu kwa ajili ya manufaa yake mwenyewe mfano mzuri ni pale utakapo muona mama mwenye familia ya watoto wawili akiaga watoto wake anaenda kutafuta kisha anarudi na taarifa za madeni na wakati huo anarudi nyumbani kwake akiwa ameshiba chakula alichokula akiwa matembezini.
Si ajabu mama kama huyu akawepo kwenye jamii hii ya watu.
Hali kama hii daima hauwezi kupiga hatua kwa sababu kesho familia ikitaka kujinasua kiuchuni basi haitaweza kamwe badala yake itaishia kujinasua na madeni nasi na si kuondokana na umasikini
Watu wa taifa wanaangamia kwa kumkosa mtu wa watu
, Kiongozi na si msemaji, mtendaji na si mtambaji. Hili ni janga la mwambao mzima.
Watu wa taifa kamwe ni ngumu kuweza kufikia malengo kirahisi
Ikiwa kuna wale ambao huwa hawajilikishwi kwenye uundaji mipango ila cha kushangaza kwenye utekelezaji wanaachiwa wasikilizaji na wasindikizaji ila watu wanabaki kama watazamaji na wakosoaji.
Ni Kweli hakuna jamii isiyo na wakosoaji au wasemaji ila huku hawa wanakithiri sana.
Hawana dira maalumu ya wapi tufike zaidi ni madeni chungu nzima ya kutaka kulisha matumbo na kufurahisha macho na viuno vyao.
Sauti ya umma unahitajika kwenye muongozo wa hati ya watu wa taifa. Sauti hii ikipatiwa ufumbuzi basi hapatakuwa na ujinga wowote wa kundi flani kutaka kitu flani wakati kuna wengine hawanufaiki moja kwa moja na kitu hicho.
Bado kuna tatizo la sauti ya ya yule kutawala zaidi kila mahali kiasi kwamba hakuna haki baina ya watu wa jamii nzima, watu wa taifa . Hili ni tatizo kubwa sana . Ni lazima mtu kama huyo apunguziwe majukumu .
Hivi baba au mama akibeba majukumu yote ya familia unahisi kipi kitatokea?
Kama si dharau na kuwepo kwa matukio na upigaji na udanganyifu!
Katika hali hii ni rahisi sana kwa watu wa taifa moja kuzungukana na kupishana . Kwa sababu mtu mmoja hawezi kuwa mkamilifu wa kila kitu kiasi cha kuamu kila jambo na hata kama ikitokea bado imani yake kwa watu anao waongoza haitakuwa sawia kutokana na kwamba wale walio chini yake wanaweza wasimkubali mtu huyo kwa kutokuwa na imani naye ya moja kwa moja.
Watu na ardhi yao , watu na utu wao watu na mamlaka yao inawezekanaje kupoteza sauti kwenye kilicho chao?
Huu ni uzembe wa hali ya juu.
Kwani kuna ulazima gani wa kutaka kufanya starehe ya muda mfupi na wakati huna uwezo wa kuiendeleza furaha hiyo ikaweza kudumu katika maisha yako yote.
Watu na maamuzi yao
Jamii inahitaji kuwa na mashujaa wengi zaidi kuliko wajinga na matapeli kama ambavyo serikali nyingi zimekuwa na viongoi wengi matapeli wsbasiasa wasiyokuwa na maana yoyote ile.
Kuruhusu mamlaka za kigeni kuwa na sauti kwa watu wako ni ujinga! endapo utafanya hivyo unahisi kipi kitatokea?
Basi fahamu ya kuwa kitakachotokea ni watu wako kuendelea kufanywa kuwa watumwa wa fikra na masikini na kuendelea kuwa vijakazi wa mamlaka zingine.
Basi ili watu wa taifa waweze kujikwamua ni lazima kuwe na usirikishwaji wa moja kwa moja wa umma juu ya mambo ya kitaifa kwa maana huo ndiyo muhimili mkuu wa maendeleo ya taifa lolote lile.
Ni lazima ifike hatua taifa liondokane na tatizo la kufanya maamuzi holela
Yaani kusiwepo na kundi flani la watu kuamua jambo flani pasipokuwepo ba ushirikishwaji wa moja kwa moja.
Naweza kumalizia kwa kusema hizi ndizo zinazoweza kusaidia kuondosha hali hii ya utegemezi na kulifanya taifa kusonga mbele.
Ni mimi Selemani Joseph Bundala