mimi nimeishi Uturuki miaka almost 6 nimesoma chuo kinaitwa University of Instanbul. infact kwa Elimu wanajaitahidi sana ila kwa maisha pako very tight. kupata kazi za vibarua kama UK au States ni almost impossible njia rahisi ni uwe mmachinga. nchi ipo so crowded, Istanbul alone ina watu zaidi ya 20 milion. na hii inaifanya ajira kuwa ngumu kidogo. upande wa chakula wapo vzr wana aina nyingi sana za vyakula na wanajua haswa kupika. ubaguzi upo kiasi especially pembezoni mwa miji. kuna mabinti wazuri sana na wanapenda sana wanaume weusi ahida kaka zao wanakuwaga na wivu sana kwenye hili unaweza kupigwa. upande wa maisha yapo expensive kidogo kupangisha aprtment inabidi ujiweze sisi tulikuwa tunaishi wanne nyumba moja ila ofcourse tulikuwa wanafunzi. gharama za simu zipo juu nadhani ndio inaongoza dunia nzima. ukiwa mwanafunzi lakini unapeta kuna ofa kibao za mitandao yote. upande wa transportation kuna ferry boat inayotoka European side kwenda Asian side, kuna mabasi kama haya ya mwendokasi kule wanaita Metrobus, kuna Tram ambayo ni nzuri sana kuna mabasi ya kawaida na Metro ya underground. mavazi ni moja ya eneo ambalo wapo vzr sana wana nguo kali na bei ya chini. Industry hiyo kule nahisi ni one of the best in the World. vivutio vya utalii ni vingi kuna maeneo ambayo yametajwa kwenye Quran na Bible ya zama hizo. In general naiweka katika nchi ambazo unatakiwa utembelee kabla hujafa. Its a really interesting Country. Hope nimetoa information ulizokuwa unazihitaji. kama kuna la ziada utaniuliza.