Nchi ya Saudi Arabia yapata Mufti

Nchi ya Saudi Arabia yapata Mufti

Yes, descendants,mama wa King Abdullah ni mzungu na alikuwa mkiristo kabla ya kuolewa na King Hussein, ambaye naye mama yake alikuwa na asili ya Ulaya
Uislam hauko kwa ajili ya Waarabu tu, hata Mtume alioa kutoka jamii ya Jews na Coptic Christian ingawa hakuzaa nao watoto

sasa naanza kuulewa kwa nini Islam na muslims wanatumika kudestroy Christianity, elite wanatawala pande zote mbili, duh …
 
Alama kwenye paji la uso inayosababishwa na kusujudu (SIJDA) na alama kwenye unyayo wa mguu wa kushoto inayosababishwa na kukaa kwa kukunja mguu chini wakati wa kusoma tashahhudi (Attahiyyaatu) hutokana na (A) hali ya ngozi ya mtu na (B) hali ya tandiko analosujudu na kukaa juu yake wakati wa kuswali!.
Sio waarabu tu bali hata kwetu waswahili kuna watu wanaswali vipindi vyote na kuongeza na swala za sunna lakini nyuso zao zipo kawaida tu au alama inaweza onekana kwa mbali kutokana na hali ya ngozi zao au matandiko wanayoyatumia wakati wa kuswali.
Hakika mkuu, unasujudu kwenye mkeka mgumu wa ukili, mara tano kwa siku,

Sigda lazima itokee kubwa tu
 
Hivi mtu ili awe mwanachuoni inabidi awe na sifa gani?
1️⃣ Asome sana na kwa muda mrefu kwa wanachuoni wenye kusifika kwa fani mbalimbali za elimu ya uislamu na lugha ya kiarabu, itikadi sahihi , maadili sahihi, sunna sahihi na tabia njema zilizochukuliwa katika mafunzo sahihi ya Mtume Muhammad
صلى الله عليه وآله و سلم.

2️⃣Yeye mwenyewe akiisha soma ayafanyie kazi yale aliyojifunza kwa wanachuoni wa zama zake na wale waliopita kabla yake( asiwe miongoni mwa wale masheikh waovu wanaowaambia watu kwamba fuateni maneno yangu mazuri na msiangalie vitendo vyangu vibaya) kwa hiyo anatakiwa kujipamba na kusifika kwa sifa zote za elimu sahihi ,tabia njema, itikadi sahihi , lugha ya kiarabu na sunna sahihi zilizotolewa katika hadithi sahihi za mtume Muhammad
صلى الله عليه وسلم.
3️⃣Akishasoma yeye pia asomeshe sana wengine elimu sahihi, itikadi sahihi na maadili sahihi na kwa muda mrefu kiasi kwamba wanachuoni wa zama zake na wale watakaokuja baada yake wajiridhishe na wathibitishe kuwa yeye ni mwanachuoni.
4️⃣ Sheikh ambaye
(A) Masheikh zake hawajulikani (haijulikani kasoma wapi!)
(B) Wanafunzi wake hawajulikani!. (haijulikani elimu aliyosoma kaifanyia nini!)
(C) Vitabu vyake havijulikani. .
(D) Itikadi (A'qiyda) yake haijulikani.
(E) Madhehebu yake hayajulikani.
(F) Msimamo, maadili na mienendo yake haijulikani.
(G) Ikiwa chochote kilichotajwa hapo juu kati ya A, B, D, E, na F hakijulikani!

HUYO SIYO MWANACHUONI!
 
Misconception na propaganda za zionists ili waweze kutawala dunia
Hakuna lazima ya mtu kuwa muislam
Quran 2:256: There is no compulsion in religion.”
Qur’ani haiamrishi Waislamu kuharibu au kuondoa Ukristo, bali ni kuamuru kumwabudu Mungu ipasavyo na kuwaalika wengine kwa hekima na mfano mzuri.
 
Cha kushangaza huyo mufti hana sijdah. Sasa njoo kwa niggers nyeusi kiwalani, mbauda, itigi Na nyarugisu nyeusiii tiii lakini ina misijdah miikubwa kwenye paji zao nyeusi.

adriz
Oya huu Uzi haukuhusu Yahudi Galatia wewe kaa pembeni na mambo yasiyokuhusu uache shobo.

Kaa mbali Yahudi wewe
 
Hakuna wee muongo mijitu mieusi inaamini eti ikifa kwenye uislamu inabadilika na kuwa miarabu ndo maana inajisugua paji zao nyeusi hadi na Steel wire na msasa eti ipate misijdah kwenye paji zao nyeusi.

Hovyo kabisa pathetic

adriz Adiosamigo Jagina
Huu sio Uzi wa wavuta bange wenzako wewe Yahudi Galatia punguza ushauri na kulalamika kwenye Mada zisizo kuhusu
 
Jana siku ya jumatano ya tarehe 30 rabiy-l - Akhiyr 1447 (H) sawa na 22 September 2025 (AD) ufalme wa Saudi Arabia umemteua na kumtangaza Sheikh Dr Swaaleh bin Fauzaan bin Abdillaah Al fauzaan kuwa Mufti mkuu wa nchi hiyo akimrithi mufti aliyetangulia Sheikh Abdul Aziyz bin Abdillaah Aal - Al sheikh aliyefariki dunia mwezi ulizopita.

Kabla ya uteuzi huo baada ya kufariki Mufti aliyetangulia mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo mheshimiwa mwanamfalme Muhammad bin Salman maarufu kama MBS alikuwa amependekeza kwa mfalme wa nchi hiyo majina mawili kwa ajili ya kiti cha umufti wa nchi hiyo ambayo ni,
1️⃣Sheikh Dr Swaaleh Al fauzaan na
2️⃣ Sheikh Swaaleh bin Humeid ambaye baadhi ya mitandao ya kijamii kiasi cha wiki tatu zilizopita ilitangaza kwamba ndiye mteule wa kiti cha umufti wa nchi hiyo kabla ya tangazo la jana lililotolewa na mfalme wa nchi hiyo na mtumishi wa misikiti miwili mitukufu mheshimiwa mfalme Salmaan bin Abdil Aziz Aal Saudi lililobainisha kwamba Sheikh Dr Swaaleh Al fauzaan ndiye mufti mpya wa nchi hiyo.

Pamoja na cheo cha umufti ambacho ni cheo kikubwa nchini Saudi Arabia tangazo la mfalme limeeleza kwamba mufti atakuwa na majukumu ya ziada ambayo ni pamoja na kuwa kiongozi mkuu wa baraza la wanachuoni wakubwa wa nchi hiyo na pia kiongozi mkuu wa kamati kuu ya tafiti za kielimu na fatwa ya nchi hiyo akibeba na kusimamia majukumu yote yaliyokuwa chini ya wizara ya masuala ya kiislamu ya nchi hiyo kwa kiarabu
وزارة الشؤون الإسلامية.

SHEIKH AL FAUZAN NI NANI?

Sheikh Dr Swaaleh Al fauzaan ni msomi nguli ,muhitimu na muhadhiri mstaafu wa chuo kikuu cha kiislamu cha Imaam Muhammad bin Saud kitivo cha sharia ya kiislamu na ambaye kwa miaka mingi sana amejulikana sana, kuheshimika sana na kupendwa sana na waislamu wengi duniani hasa wale wa madhehebu ya ahlissunna wal jamaa( masalafi).

Sheikh Dr Swaaleh Al fauzaan pamoja na kuwa muhitimu wa chuo kikuu kilichotajwa hapo juu amepata elimu nyingi kupitia masheikh mbalimbali wa nchi hiyo ikiwa pamoja na :
1️⃣ Mufti wa zamani wa Saudi Arabia Sheikh Abdul Aziz bin Abdillaah bin Baaz .
2️⃣Sheikh Abdul Rahman bin Nasser Al Sa'adiy.
3️⃣Sheikh Abdullaah bin Humeid.
4️⃣Sheikh Muhammad Al Amiyn Al Shinqiytwiy.
5️⃣ Sheikh Abdul Razzaaq A'fiyfiy na wengine kadhaa.

Kati ya wanafunzi waliosoma kwa Sheikh Dr Swaaleh Al fauzaan ni pamoja na Imamu na khatiybu wa msikiti mkuu wa Makka na msomaji mkubwa wa Qur'an maarufu sana duniani Sheikh Abdul Rahman bin Abdil Aziyz Al Sudeysi, Sheikh Muhammad bin Swaaleh Al Munajjid na wengine wengi ikiwa pamoja na sisi wanafunzi wa kitanzania na maeneo mengine duniani tunaosoma vitabu vyake na kufuatilia vipindi vyake vya redio , Tv na pia kupitia mitandao ya kijamii.

Sheikh Dr Swaaleh Al fauzaan ameandika na kusherehesha vitabu vingi sana zaidi ya 50 na kati ya vitabu vyake vingi vilivyoenea katika maduka mengi ya vitabu vya kiislamu duniani ikiwa pamoja na maduka ya vitabu vya kiislamu ya hapa Tanzania ni pamoja na :1️⃣ Aqiydatul Tauhiyd.
2️⃣Al Irshaadu Ilaa Swahiyhil Ii'-tiqaadi.
3️⃣ Al mulakh khaswul -Fiqhiy
4️⃣ Ahkaamul -Atw-i'mati Fy- l -shariya'til - islaamiyyah.
5️⃣ Sharhul -Sunnah cha Imaamu Al - barbahaariy.
6️⃣ Sharhul A'qiydatil- waasitwiyyah cha Ibnu Taymiyyah na vingine vingi , na pia amekuwa akiandika makala nyingi sana ambazo zimekuwa zikiwekwa katika magazeti na majarida ya kiislamu.

Kabla ya uteuzi wa jana sheikh Dr Swaaleh Al fauzaan amewahi kuteuliwa kushika nafasi mbalimbali ikiwa pamoja na:
1️⃣. Mwalimu katika taasisi ya elimu ya Riyaadh.
2️⃣Muhadhiri katika kitivo cha sharia ya kiislamu.
3️⃣Mwalimu katika idara ya elimu ya juu ya wahitimu wa chuo cha misingi ya dini,
4️⃣ Mwalimu mkuu na muhadhiri katika taasisi ya elimu ya juu ya mahakama .
5️⃣Imaamu,khatiybu na mwalimu katika msikiti wa prince Mit-i'b bin Abdil Aziz katika mji wa Al-Malaz.

6️⃣Mjumbe wa kamati ya kudumu wa ya utafiti wa kielimu na fat-wa.
7️⃣
Mjumbe wa baraza la wanachuoni wakubwa nk na pia amekuwa akisomesha masomo mbalimbali kupitia vipindi vya redio na TV na pia akiandika makala katika magazeti na majarida mbalimbali ya kiislamu.

Waislamu wengi duniani hasa wale wa madhehebu ya ahlissunnah wal jamaa (Masalafi) wamepokea kwa furaha sana taarifa ya uteuzi wa sheikh Dr Swaaleh Al fauzaan kuwa mufti mkuu wa nchi ya Saudi Arabia na wanamuomba Allaah mtulufu amsaidie Sheikh Dr Swaaleh Al fauzaan katika utekelezaji wa majukumu aliyopewa.
Habari nzuri kwa Umma .

Cc : Baljurashi
 
1️⃣ Asome sana na kwa muda mrefu kwa wanachuoni wenye kusifika kwa fani mbalimbali za elimu ya uislamu na lugha ya kiarabu, itikadi sahihi , maadili sahihi, sunna sahihi na tabia njema zilizochukuliwa katika mafunzo sahihi ya Mtume Muhammad
صلى الله عليه وآله و سلم.

2️⃣Yeye mwenyewe akiisha soma ayafanyie kazi yale aliyojifunza kwa wanachuoni wa zama zake na wale waliopita kabla yake( asiwe miongoni mwa wale masheikh waovu wanaowaambia watu kwamba fuateni maneno yangu mazuri na msiangalie vitendo vyangu vibaya) kwa hiyo anatakiwa kujipamba na kusifika kwa sifa zote za elimu sahihi ,tabia njema, itikadi sahihi , lugha ya kiarabu na sunna sahihi zilizotolewa katika hadithi sahihi za mtume Muhammad
صلى الله عليه وسلم.
3️⃣Akishasoma yeye pia asomeshe sana wengine elimu sahihi, itikadi sahihi na maadili sahihi na kwa muda mrefu kiasi kwamba wanachuoni wa zama zake na wale watakaokuja baada yake wajiridhishe na wathibitishe kuwa yeye ni mwanachuoni.
4️⃣ Sheikh ambaye
(A) Masheikh zake hawajulikani (haijulikani kasoma wapi!)
(B) Wanafunzi wake hawajulikani!. (haijulikani elimu aliyosoma kaifanyia nini!)
(C) Vitabu vyake havijulikani. .
(D) Itikadi (A'qiyda) yake haijulikani.
(E) Madhehebu yake hayajulikani.
(F) Msimamo, maadili na mienendo yake haijulikani.
(G) Ikiwa chochote kilichotajwa hapo juu kati ya A, B, D, E, na F hakijulikani!

HUYO SIYO MWANACHUONI!
Naomba dalili katika Qurani au sunna kuthibitisha madai yako haya..

Umegusia mas'ala ya kusoma muda mrefu.

Naomba unielezee kwa dalili je kusoma muda mrefu kwa mujibu wa qurani na hadithi iwe ni miaka mingapi al habiib?

Nataka dalili kwa sababu huo ndio utaratibu wa Manhaj salaf kwamba mambo yaende kwa dalili na sio maneno matupu pekeee..
 
إن توضيح الواضحات

من أصعب المشكلات.

وليس يصح في الأذهان شيء

.إذا احتاج النهار إلى الدليل

(كل من عرفناه صاحب علم من المتقدمبن والمتؤخرين

مارأيناه إلا متصفا بالصفات المذكورة في إجابتنا. وأرشدك إلى كتاب إن شئت، كتاب سماحة الشيخ الفوزان المسمى
"الاجوبة المفيدة عن الأسئلة المناهج الجديدة

.سوف تستفيد بكثير إذا كنت طالب علم
اما إذا كنت طالب جدل،
فلست انا من اهل الجدل.
 
Allah Amhifadhi na Amchunge Shaykh Dr. Saleh al-Fawzaan na Amuwafiqishe na Amsaidie katika majukumu yake mapya mazito aliyopewa na Ampe umri mrefu zaidi katika Sunnah na Amjaalie awe na manufaa kwa Uislam na Waislam Saudi Arabia na Duniani kote.

Allah Amsamehe na Amrehemu na Amuingize Peponi na Amuepushe na Moto na Amuepushe na Adhabu ya kaburi Mufti mkuu aliyetangulia Shaykh Abdul-'Azeez Ibn 'Abdullah Aal ash-Shaykh.

Allah Awarehemu Wanachuoni wetu wote waliotangulia na Awahifadhi walio hai.
 
اللهم آمين
 
Mkiambiwa hii midini ni man made mnakataa, sasa ona binadamu anayeteua msimamizi wa “ kitabu kitakatifu” ni muhuni tuu tena muuaji billionaire, za kupewa changanya na zako
 
Back
Top Bottom