Nchi tajiri zagoma kusaidia nchi masikini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi tajiri zagoma kusaidia nchi masikini

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Henry Kilewo, May 13, 2011.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kutopewa uzito na nchi tajiri kikao cha Istanbul cha kuzisaidia nchi zenye ustawi mdogo
  Kikao cha nne cha Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuzisaidia nchi zenye ustawi mdogo duniani kimefanyika mjini Istanbul Uturuki bila ya kupewa uzito unaostahiki na viongozi wa nchi tajiri na zilizoendelea. Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan amesema viongozi na maafisa wa ngazi za juu wa nchi tajiri na zilizoendelea hawakuonyesha hamu kubwa ya kuhudhuria kikao hicho wakati ambapo hakuna mwenye haki ya kujifanya kuwa hana jukumu wala dhima yoyote kuhusiana na mwanadamu ambaye hutumia dola 1.25 tu kwa siku ili kuweza kuendelea na maisha yake ya dhiki na hilaki. Waziri Mkuu wa Uturuki ameongeza kuwa leo masuala na matatizo ya dunia yamevuka mipaka, nchi, jiografia ya kisiasa na watu wa mataifa. Erdogan amesema matatizo ya hifadhi ya mazingira, hali mbaya ya ikolojia na hali ya hewa, ugaidi na uhajiri yanazitishia nchi zote, na kwamba nchi ambazo zinayapuuza matatizo hayo zinawafanyia dhulma wananchi wao wenyewe na jamii ya kimataifa pia. Waziri Mkuu wa Uturuki amesisitiza kuwa vita vya kupambana na njaa na umasikini si jukumu la mtu binafsi bali linaihusu jamii nzima ya kimataifa.
  Kikao cha nchi zenye ustawi mdogo kimebuniwa na Umoja wa Mataifa; na hufanyika mara moja kila baada ya miaka kumi ili kufikiria njia mpya za kuzisaidia nchi masikini duniani. Imepangwa kuwa hati ya mkakati mpya wa kukabiliana na umasikini katika nchi zenye ustawi mdogo ipasishwe katika kikao cha Istanbul. Kikao cha nne cha nchi zenye ustawi mdogo kimefanyika katika hali ambayo takwimu zinaonyesha kuwa hali ya nchi hizo hivi sasa ni mbaya zaidi kulinganisha na miaka kumi iliyopita. Katika ripoti uliyotoa sambamba na kuanza kwa mkutano wa Istanbul, Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya kuongezeka idadi ya nchi masikini. Kwa mujibu wa ripoti hiyo hadi ifikapo mwaka 2050 idadi ya watu katika nchi masikini zaidi duniani itafikia bilioni moja na milioni 700. Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imefafanua kwamba kuongezeka kwa idadi ya watu katika nchi masikini kutaongeza matatizo zaidi katika utoaji huduma za msingi zikiwemo za afya na elimu. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa asilimia 60 ya watu katika nchi hizo wana umri chini ya miaka 25, ambao kama watapatiwa fursa mwafaka, watu hao wa rika la vijana wanaweza kuwa injini ya kuongeza kasi ya ukuaji uchumi; vinginevyo watakabiliwa na ufukara wa kupindukia. Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa nchi 48 ambazo zina idadi ya watu bilioni moja ziko kwenye orodha ya nchi masikini zaidi duniani. Thelathini na tatu kati ya hizo ziko katika bara la Afrika, 14 ni za bara la Asia na nchi ya 48 ni Haiti iliyoko katika bara la Amerika. Hii ni katika hali ambayo miaka 40 nyuma nchi 25 tu zilikuwa kwenye orodha ya mataifa masikini duniani. Idadi ya nchi masikini imeongezeka maradufu katika muda wa miongo minne iliyopita wakati ambapo kiwango cha uzalishaji wa utajiri na mazao ya kilimo kimeongezeka mara kadhaa. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa kuna ufa mkubwa wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi tajiri za Kaskazini na zile masikini za Kusini. Na hii ni katika hali ambayo katika vikao mbalimbali vilivyofanyika katika miongo kadhaa iliyopita nchi tajiri na hasa zile za kikoloni zimekuwa zikitoa ahadi ya kuzisaidia nchi masikini na kupunguza idadi ya watu masikini. Lakini kumbukumbu zinaonesha kuwa ahadi hizo zilikuwa ni za makaratasini tu, na kama kuna msaada ambao umetolewa, basi ni kwa malengo ya kujipatia faida na maslahi ya muda mrefu katika nchi masikini. Tunachoweza kusema ni kwamba kutokana na hatua ya nchi tajiri na zilizoendelea ya kutokipa uzito unaostahiki kikao cha Istanbul hatuwezi kuwa na matumaini makubwa kuwa malengo yaliyomo kwenye hati ya kikao hicho kuhusiana na kuboresha hali ya maisha katika nchi masikini yataweza kufikiwa.../
   
 2. n

  never JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ni bora hayo mataifa kuamua kuzitosa hizo nchi iliziweze kuumiza vichwa na kujitegemea kuliko kuendelea kuwa mataifa tegemezi
   
 3. O

  Oikos Senior Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mataifa yenye viongozi wanaoeleweka kuwa ni waadilifu hawatanyimwa misaada. Hawa wa kwetu, sijui kama tutapona.....
   
 4. n

  never JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ni bora uendelee kunyimwa ili hawa mafisadi waumbuke na mitumbo yao na matabasamu yao yanywee na kufifia then waonje joto ya jiwe
   
 5. M

  Mmongolilomo Senior Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kati ya vigezo walivyopewa na wafadhili hata nusu hawakuweza kufikia. Hii hatari
   
 6. Habdavi

  Habdavi JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  So far kwangu mimi that is good news. Tutaendelea kubebwa mpaka lini
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Miaka yote hamsini pesa zote walizoleta hazijaonyesha matunda, bali kudidimiza zaidi.
  Mtoto ukimlea kwa kumpa bajeti ya kutunia hatajishughulisha kubuni mbinu za kujitegemea. Tumeshuhudia watoto wa maskini wanahimili vishindo kuliko watoto wa matajiri waliozoea kusafishiwa hata vyombo wanavyolia chakula.:kev:
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Wenyewe wako taabani, unasikia wanavyopeana bail outs.....lakini ukweli pia sio kuwa wanatusaidia,wanatuzidishia utegemezi huku wakituibia maliasili zetu.

  Kama viongozi wetu wangelitambua hili basi wangefata mfano wa Gaddafi kwa yale mazuri yake aliyowafanyia walibya na kupinga ubeberu wa hizi nchi zinazoitwa tajiri,ingawaje ni utajiri walioupata na wanaoendelea kuupata kwa kuziibia na kuzifanyia ujanja nchi "masikini".

  Nchi zetu si masikini ila zimekosa viongozi tu.
   
 9. A

  Ame JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Mataifa mavivu ( a.k.a nchi zinazoendelea) zimezidi kuwa na rent seeking behaviour. Hazitaki kujifikirisha ili waweze kujitegemea na viongozi wao wamebakia kuwa wakinga bakuli ili wastarehe na familia zao huku population zao kubwa zikiishi kwa mlo mmoja kwa siku. Nina wapongeza sana hayo mataifa acha tupate utamu wa maisha kwa kukosa misaada ili akili zetu zichangamke kujitengenezea uchumi unaojitegemea.
   
 10. s

  seniorita JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sidhani hata inafaa kuita misaada maana huko zinakoishia hizo fedha si kwa watu wanaohitaji msaada kwa hiyo wakikataa hao wakubwa wa dunia, impact yake kwa common perso ni ndogo sana
   
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hamna haja,.
  hasa kama hela wanazotoa
  zinaenda kwenye matumbo ya mafisadi,...
  siku zote nawaona wajinga kweli hao wanao jipendekeza kutoa misaada Tanganyika
   
 12. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #12
  May 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mataifa hayo tajiri yanastahili pongezi kwakuwa yamesababisha sasa mataifa masikini kukaa na kufikiri juu ya kujijenga na kuendeleza wananchi kwakuwa yalikuwa yameyapumbaza mataifa masikini na kuacha kubuni juu ya utumiaji wa rasilimali zake kwa maslahi ya wananchi wake,

  hii ni nzuri sana kwa wale wenye uelewa wa kutaka maendeleo kuliko ya wale watakao kaa na kuhoji na kunung`unika juu ya kutoswa safi sana, jikomboeni wenyewe!!!!!!!!!!
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Lakini mmeona alternative inayokuja nayo mi-great thinker yetu katika uongozi -- kukopa toka benki binafsi ili kuendeleza kutanua kwenye mashangingi na kulipana posho za ajabu kwenye semina "endekezi" !!
   
 14. n

  never JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kamanda KILEWO nikupongeza kwauchambuzi huwo na habari hii uliyoishusha, ni kweli kila taifa linawajibu wa kuwajibika katika kujikomboa ila mataifa yetu haya hususa hili letu la tanzania limeshindwa kujikwamua kwakukosa viongozi wenye uchungu na taifa hili, kukosekana kwa misaada itasababisha kuwaamsha waliyo lala na kuweza kukaa kwenye mstari

  ila katika harakati hizi inatubidi tufunge mkanda kweli kweli katika kukomboa mataifa haya kwani yako mbali sana kifkra yameendelea kuwa na mawazo mgando juu ya ustawi wa wananchi wake.
   
 15. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  tukatae hata wakitulazimisha afu tuwachenjie kwenye mikataba walioingia nasi afu tuone...
   
 16. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #16
  May 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  tusikubali kuendelea kuwa watumwa kwasababu ya misaada ya hapa na pale na kufurahia safari za ulaya na kupewa ofa ya kupeleka watoto wetu majuu ili wakapate elimu, tukomae humu humu bongo ipo siku tutalikomboa taifa letu na kurudi kwenye mstari unaotakiwa na kuheshimika duniani kote bila wasi wasi wala woga i hope tutafika huko god be blessing us
   
 17. Dadii

  Dadii Senior Member

  #17
  May 15, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ule si msaaada ni mkupo, na kwa kawaida kitu kikishakuwa cha mkopo kinakuwa na impact yake, huwezi kurudishi kama ulivyochukuwa lazima na riba juu.
  Mikopo yenyewe ingekuwa inatunufaisha tungehuzunika sana ila inaenda kwenye matumbo ya mafisadi pouwa tu kuikosa kwasababu nchi hii inandeshwa kwa fedha yaka yenyewe na mikopo ni miradi ya mafisadi amabyao inakuja kukumuimiiza mwananchi wa kawaida thus why JK kila siku kwenye kuomba misaada. wakati mzee mkapa alikuwa analipa madeni ya misaada jaopa nae mwishoni alituchakachua.

  Kama mie ndo Rais kuitwa mbele ya hadhara masikini ni aibu kwa nchi kama Tanzania then nasafiri kwa gharama za wadanganyika kwa ajiri ya vikao vya masikini poor Tanganyika nchi ya mari nyingi watu wengi wa Ulaya wanailili sana.

  Viwanda vyetu tumeuza tutapeleka wapi vijana wetu wanomaliza vyuo kunzia veta mpaka university, kilimo tunakipa siasa toka uhuru jembe la mikono hatuwezi kudharisha mazao yenye tija mwisho wake ni umasikini huku tukiwa na sela mbovu kwa vijana amboa ndio nguvu ya sasa ya kusukuma gurudumu la maendeleo sisi tunawaita Vijana Taifa la kesho.

  So Tanzania kwa vijana sio isssue, kwa serikali yetu ya Magamba mpaka ukizeeka ndio utmike sababu ndio muda wako na sio wa ujana. Tanzania haipo wala haifuati sera za ujamaa na kujitegemea wala siasa za mrengo wa kti,kushoto wala kulia wala ubepari ni nchi inanyonywa na nchi Tajiri kwa sera zake mbovu za uwekezaji na ubinafsishaji na mikataba mibovu ya viongozi wetu wa leo wakina Mangungulo wa Msovelo wale wazee walikuwa hawajui kusoma wala kuandika zaidi ya kuweka dole gumba, sisi ni sera za ufisadi na 10% kila makatba.

  Viongozi wetu ni ombaomba kama kina matonya ispokuwa wao wanomba kwa kutumia kidhungu na miradi uchwara katika makaratasi huku wamevaasuti. Sasa jamaa wamekata mrija.

  Rudini kwenye mstari kina jk na wenzio vunja mikataba uchwala inayoumiza nchi na wananchi kwa ujumla tuna wasomi wenye tija nchi tufanye reserch kwa wenzetu walioendelea juu ya issues za mikataba kwenye madini na kila sehemu, adabisha watu wenye rushwa, fukuza mtu semina elekezi jk ni uchakachuji wa fedha za walala hoi wakati kila mujiriwa huwa ana job descriptions.

  Tumechoka, tumechoka tena tumechoka sana, tumetoka safari ya mbali toka uhuru hapa tulipo tumevimaba yote mapaja na kutetemeka mwili watoto wetu wanakuja CDM kututaka hari..........

  Haya sintonyamaza mpaka pumzi yangu ya mwisho au mpaka niione Tanzania yangu tukila sahani moja keki ya taifa sisi mafukara na nyie watawala uchwala. ole wenu ole wenu ipo siku mtakuja kulia na kusaga meno viongozi mbumbu msiojali taifa hli,, tutakuja kuwatafuta kokote mliko mturudishie chetu milchochukua kwa muda mrefu siku siku si nyingi wazliwa wa kwnza wa Tanzania watakopo pigo hodi ikulu usiseme ho mi sikuja kama unakuja oho sijajiandaa, tengeneza njia zako uondoke kwa amani kuliko unayoyafanya magamba.
   
Loading...