Mkuu, hata kama hiyo pesa ya barabara ya Chalinze inatoka wapi, kwani anayenufaika ni nani si ni watanzania sisi jamani..!!
Stahiki za watumishi si zinalipwa kwa awamu baada kuhakiki kama ni AUTHENTIC. yaani wewe ulitaka pesa ilipwe tuu kiholela wakati hizi ni zama za wafanyakazi hewa.? yaani turudie makosa yale yale sio.?
Hiyo hali ya uchumi unayozungumza wewe ni ipi, wakati Waziri Mpango keshasema hali ya uchumi ni nzuri, au na wewe una wizara yako.? basi tuwekee hapa takwimu ya hali ya uchumi kwa mujibu wa ofisi yako.
Baa la njaa hilo ni janga la asili, au na lenyewe limesababishwa na serikali.?
Kukopa ni jambo la kawaida, unless hujui uchumi wa dunia unaendeshwa vipi. na ukiona tunakopa, ujue kama nchi bado tuna sifa ya kukopesheka.
Cha kuzingatia hapa ni kwamba, sisi ndio tunachagua nani atukopeshe, maana kuna wengine wapo tayari kutukopesha hata leo, ila hatutaki kwa sababu mikopo yao ina masharti magumu. mbona hivi ni vitu simpo kabisa na havihitaji kula ugali mgumu kuvielewa jamani, mnatumia nguvu nyingi mno kuilewa serikali ya JPM ndio maana mnalalamika kila siku, just be simpo dear brothers.