A
Dar kukosa Maji ni sawa na baba mwenye NYUMBA ununue Kuku jogoo aliyekomaa na wakati wa kula wakupe miguu ya jogoo
Ikiwa DSM inashikilia uchumi wa nchi kwa 80% je hatuwezi kuona Aibu kuwakosesha Maji
We don't need to find excuse on this
Aisee we jamaa umeongea point sana, kila siku huwa nawaza kwanini DSM hairejeshewi kama inavyoingiza??, yan huwa inafikirisha sana sehemu inayo changia pato la taifa kwa zaidi ya 18% lakini ndo sehem ambayo wanachi wake wanazidi kuteseka, kuanzia miundombinu ya usafiri na barabara na maji. Ki ukweli mapato yanayotokana na dar kuyatumia hayo hayo kuboresha miundominu na mikoa mengine halaf wananchi wanaotafuta hayo mapato wanateseka ni kitu cha kifedhuli sana.
Sasa hivi DSM imeelemewa, utitiri wa private sectors na fursa nyingine za biashara unaendelea ndani ya jiji na kila kijana anayetamani kufanikiwa anataman aje dar, population na huduma za kijamii ni irrelevant. Watu wanateseka makazi na huduma za usafiri sababu wamekua centered kwenye eneo finyu sana.
Haya mapato yanayogawanywa kwanini yasitumike kuboresha miundominu ili wanaozidi kuja kutafuta wasipate unnecessary obstacles? Kwaninj ule mpango wa kumega sehem ya pwani kuwa DSM Usiendleee kwa kulazimisha baadhi ya makampuni makubwa yahamie huko (ila yapewe specific period) na serikali igawe ardhi kwa njia ya kuuza kwa bei nafuu ili watu waanzishe makazi?
Kujenga barabara za mwendokasi si kutatua changamoto ya foleni…kwanza njia panda zote ziwekewe interchange, hii miradi ya mwendokasi isijengwe kwa kusua sua kama ilivyo sasa, lakini pia kariakoo ifike mahala sasa itafutiwe mbadala kuwekwe mpango wa kugawanya hawa wafanyabiashara na kutafuta sehem nyingne sio lazima milele kariakoo iwe sehem kuu ya biashara sio msaafu au biblia ile maana imekua kirusi sasa…
yani uchangie pato 18% + halafu wewe uhangaike barabarani, mara maji, umeme, msongamano wa watu, makazi kupandishwa bei zisizo na uhalisia aisee, serikali iangalie sana hawa wananchi wa DSM ni watu wasio na furaha kabisa (wengi wao sio wote)
Najua serikali ilianza kwa wao kuhama na kuhamisha serikali rasmi dodoma, basi waangalie hili la kuiongeza Dar kwenye sehem ndogo ya pwani, na kulazimisha baadhi ya huduma na vitu vingine pia vihame kwa awamu.