Nchi mpya zinazotarajiwa Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi mpya zinazotarajiwa Afrika

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Kituko, Aug 6, 2011.

 1. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Baada ya Sudan ya Kusini kujitenga kutoka main Sudan na kuongeza idadi za nchi katika bara la Afrika na duniani kwa ujumla, inaonekana inaweza kuwa chachu kwa baadhi ya majimbo ama nchi kumegeka,
  inaweza kuongeza nguvu kwa nchi zilizokuwa kwenye maelekeo huo na pia inawweza kuwa chachu kwa nchi/majimbo mapya, baadhi ya majimbo na nchi hizo ni kama ifuatavyo
  1)TAnzania
  Kwa hali ya kisiasa na nchi kukosa mwelekeo wa kujua ni kipi cha kushika kwanza, kuna uwezekano mkubwa wa Zanzibar kutoka kwenye muungano,
  Japokuwa muungano ulikuwa na kelele na kutokubaliana kwa baadhi ya Mambo lakini kulikuwa na uongozi Imara na CCM ilikuwa Bora, lakini kwa mwenendo wa CCM kwa sasa na nchi kukosa Kiranja wa kuweza kukemea mambo mazito ya Kifisadi ni wazi Zanzibar inaweza kuwa na sauti na haki ya kujioa kwenye muungano na kutengeneza nchi mpya katika Africa na Dunia kwa ujumla,
  Nchi mpya zinaweza kuwa kama hivi
  a) Tanganyika,
  b) Jamuhuri ya Zanzibar (Pemba na Unguja)
  c) Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Unguja
  d) Jamuhuri ya Watu wa Pemba
  e) Jamhuri ya watu wa Unguja

  2) DRC
  Ni miongoni mwa Nchi kubwa kabisa Barani Afrika na duniani
  Tatizo kubwa la DRC ni Majimbo yaliyogawanjwa kwa minajili ya ukabila, Congo DR pana ukabila mkali kabisa, Baadhi ya Province za Congo zimeendelea sana na sababu zinazotoka kwenye province ambazo ziko nyuma kimaendeleo ni kuwa hizo zimeendelea kutokana na viongozi waliokuwa madarakani wametoka kwenye hizo province
  Lakini ni kweli ukifika Province ya Katanga yenye Lubumbashi, Kolwezi, Likasi, Kalemie ni tofauti sana na Province ya Sud (South) Kivu yenye Uvira, Baraka, Fizi nk au province ya Nod (North) Kivu yenye Bukavu, Kamanyola nk
  WAtu wa Katanga wameshaweka wazi kuwa Kabila kama hakupita kwenye uchaguzi wa mwaka huu basi Katanga Province itakuwa nchi, same time na watu wa province zingine nao wanataka wape independent, kwa minajili hiyo kuna uwezekano wa kuwa na zaidi ya nchi tano kutoka DRC (Time will tell)

  3) Morocco
  Polisario wamepigana kwa miaka mingi mno kutaka kutoka Morocco na kuwa na nchi yao ya Sahara Magharibi, haya mapinduzi ya nchi za kiarabu na kupatikana kwa uhuru wa Sudan ya kusini ambao walikuwa almost wanafanana kwenye kutafuta uhuru wao,inawatia Chachu kubwa kwa watu wa sahara Magaharibi, kuongeza nguvu zao za kudai Nchi "yao"

  4) Somalia na SomaliLand nchi inayojiendesha yenyewe lakini bado haijajitangazia uhuru wake,

  5) Baada ile issue ya Biafra Nigeria inaonekana kana kwamba bado wapo Pamoja, lakini muendelezo wa siasa za Kidini na Kikabila zinaonyesha wazi uwezekano wa nchi kumegeka

  mitizamo yenu ni ipi wana JF
   
 2. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145

  Si ajabu hayo kutokea kwa kuwa mara nyingi raia wa kawaida anapotafuta haki yake asione utengeneza kundi kubwa la wakosa haki hivyo ujiunga pamoja na kutengeneza kundi kubwa la wasaka haki kwa gharama yoyote.Ni hapo matamanio ya kuona kuwa kumbe mengi makubwa kwa umoja wao yanaweza kupatikana.Lakini pasipo kuzingatia hali halisi.

  Ni kweli Mubarak alistahiki kuondoka lakini,pia matamanio ya Wananchi yalikuw makubwa kulko uhalisa wa Taifa kwa ujumla.Ila kwa kuwa wao kama Wananchi hawastahiki lawama anayestahiki lawama hi yule aliyewafikisha hapo.

  Taifa likikokosa dhamila ya kutenda haki dhuruma utawala na kuunda watawala walevi wa madaraka na wachoyo wa nafsi.Na hivyo kupelekea kuzaa jamii yenye unafsi [Selfish] dhidi ya wanajamii ambayo pia uzaa umoja kwa njia ya kufaidika kila mmoja kwa dhamila yake.

  Sia ajabu lolote laweza kutoke,pengine Mungu upenda yatokee kwa kuwa Viongozi wanakuwa na miyo migumu.Tena uzuri wa siku hizi sioo kama zamani mambo yalikuwa yakialibika viongozi wengi walikuwa wakitimka wao na familia zao.lakini sku hizi dunia inawasaka popote kuja kujibu tuhuma hata kama uko kitandani kama Mubarak.
   
 3. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Zenj wajikate, wasituzingue wabara kwa kelele zao za taarabu. Waishie kuimba nyimbo zao huko za bata na samaki. Ngoja nitafute binti nioe kabla ya Ramadhani.
   
 4. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  acha ubaguzi ni dhambi kubwa hiyo
   
 5. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2011
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,984
  Likes Received: 1,556
  Trophy Points: 280
  zenj kwani hakuwa nchi hapo zamani ??? Jee kiti chao katika UN walikiondoa wenyewe au kiliondolewa???

  Kuwa na Jamhuri ya Pemba au Unguja nafikiri hizi ndio dhamira za kanisa itokee hivyo lakini kwa fikra zangu haiwezekani kwani wazenj wameamka na wanamuelewa adui yao
   
 6. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,071
  Likes Received: 1,107
  Trophy Points: 280
  Gavana bwana yaani wewe huwa hauna hoja isipokuwa udini tuu, hapa tunaongelea siasa bwana hayo mengine yafanyie kule mnakotukanana.
   
 7. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tanzagiza
   
 8. a

  adobe JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Jamhuri ya tz kaskazini na magharibi(kilmanjaro,arusha musoma, shy,mwanza na bukoba) kujitenga na wakwere wanaokula jasho letu
   
 9. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  HIyo ya DRC ina ukweli na giza kidogo. Kwanza hakuna ukabila mkali, zaidi ya Ituri ambako kulikua na vita la ukabila. Kungine kupo sawa (nilifanya social study huko).
  Pia Fizi, Uvira, Baraka, Bukavu vyote pipo south Kivu. Nord Kivu ni Goma Beni, Butembo etc na Maniema ni Kindu.
  South Kivu na katanga kweli kuna discrepancy ya development level sababu mining ilianza Katanga enzi za ukoloni ila tofauti hiyo inaenda ikifutika sababu mining imeanza South Kivu pia (mostly gold, tin, cassiterite coltan etc).
  Balcanisation (nchi kujigawa kama sudan) ni threat ipo kwenye nchi nyingi za Africa ila sio kitu rahisi kutekeleza sababu ya strong nationalist feelings. Leo ukiambiwa we sio mtanzania, ni mtanganyika, utasita sana kabla ya kukubali. Unless uoneshwe clearly mafaa ya balcanisation.
  DRC imeamua kwenda pole pole toward federalism. Kwa leo kija jimbo lina governor, provincial assembly chaired by a speaker, a budget etc
  Binafsi nadhani ni more sustainable solution.
   
 10. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Habari RR,

  Kabla sijaanza ningeomba nikusahihishe kuwa hakuna Mining kubwa ianyofanya kazi Upende wa East Congo, uchimbaji uliopo ni wa wachoji tu, japo mining iko karibu kuanza maeneo ya Twangiza

  Sijuhi unazungumzia ukabila upi ambao hujauona DRC, Kivu ilikuwani province moja tu yenye Sud, Nod Kivu na Maniema (Manyema) na iligawanyika na kuwa Province Tatu na kila Province ikiwa na na dominant tribe (ndio maana nasema Province ziligawanywa kwa misingi ya kikabila).

  South Kivu ina makabila makubwa mawili japo kuna mengine madogomadogo, kuanzia Makobora, Baraka, Fizi, Lubondja, Misisi Mpaka Lubichako huko kote wapo Wabembe ambao ndio baba wa Vita na Upande wa Kuanzia Uvira, Bukavu Mpaka Nord Kivu wapo wa-Bashi ambao hawaelewani vizuri na Wabembe. makabila mengine ni kama Waferero,Wavira,Warega, Wabwali nk

  Lakini Tatizo kubwa hapa lipo kwa Raisi Kabila na Kabila la Wanyamulenge(Watusti) ambao wapo kwa wingi Minembwe, Wabembe (Mayimayi) hawamkubali kabisa Raisi kabila, kwao kabila ni kama Mtusti na uwepo wa watusti Jeshini na kwenye sector nyingine wanaona ni kana kwamba ni Kabila ndio chanzo, Hivyo uchaguzi wa mwaka huu unatatizo kubwa sana, Iwapo kabila atashinda kuna uwezekano wa watu wa Sud Kivu kutomkubal na kuanzisha vurugu za kujitenga

  Watu wa Katanga chini ya Moise wanaajenda za chinichini za kutaka kujitenga iwapo Kabila Hatapita kwenye uchaguzi wa mwaka huu, na hizo siasa za kujitenga zilianza tangu miaka ya 60, Hofu hiyo imeingia Zaidi baada ya ya Wakasai chini ya Mkongwe wa siasa za DRC Tshekedi kuingia katika kinyanganyiro cha uraisi,
  Wakasai hawana Tofauti na Wabembe katika kumpinga Kabila kuwa sio Mcongoman, na kuna kampeni kali sana kutoka kwa Wakasai walioko Lubumbashi (Katanga) za kusimamia na kuhakikisha Kabilahawi raisi,
  kwa Kabila pia akichaguliwa kuna wasiwasi wa Wakasai kutoka Kasai zote mbili kutaka kujitenga

  Province zingine Bandundu, Kinshasa, Bacongo hazina kelele sana na ziko karibu sana kutokana kuwa zinasema LUgha moja Lingala na KIcongo
   
 11. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Naona una ujuzi wa juu juu tu wa Congo, Naomba nikukosoe kidogo:

  Nikirudi kwenye mada in genera nasema tena: federalism is a more sustainable solution for the COngo na Congo imeanza kuelekea federalism. Hatua ya kwanza ilikua kujaribu kugawa Kivu, it was succesfull. Hatua ya pili ni kmugawa provinces zingine. kila province inakua na executive yake (governor and ministers) na pia legislative (bunge). Mgao huu utaifanya serikali ya jimbo kua karibu zaidi na wanainchi na kuipa nafasi serikali ya federal level ku-focus kwa maswala ya defence na international relation (trade and diplomacy, state representation on international arena etc).
  Hatua ya tatu itakua kuipa kila jimbo a judicial.
   
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Haya mambo yote nadhani yana mkono wa external prssure. Pamoja na matatizo yote DRC kuna vita kama ya mataifa makubwa yanapigana africa. Scramble and partition of & for africa ipo na inaedelea kwa style mpya.

  DRC

  • Ni france, US& UK ( Hawa interest zao huwa ziko paomja) Belgium. So mtawala akijivuta upande wa france zaidi US wanafanya mambo zao. Akionekana anajivuta upande wa france au belgium zaidi US wanafanya mambo zao. Na hivi sasa hao wote wa ulaya China amekuwa threat. So kuna mawili either DRC iendelee kuwa unstable kwa manufaa wa wanyonnyaji wote. Na viongozi wa wa nchi wanakula double dili ili kisiasa waendelee kutawala. Au DRC iwe stable kwa kukubali kugawanywa ili "wakubwa" wagawane viwanja... Kisiasa haya ni maamuzi magumu kwa kiogozi yeyote.......
  • Mfano halisi wa diplomatic war ya france VS (UK and US) ni Rwanda. kagame alionekana ni pro US zaidi. Ndio maana hata majeshi ya France yaliyokuwa rwanda hayakufanya cha maana saaana kuzuia maujai wakati wanaona RPF wanachukua nchi. Na ndio maana france wakafungua kesi ya maafisa wa RFP kuhusu mauaji...... Offcialy Kingereza nacho ni lugha ya rwanda . Sarkozy hafurahii hilo. Haya makoloni waliyapa uhuruwa bendera lakini bado ni yao..........
  Libya - Hawa jamaa hujawataja lakini hizi nchi za uaya zimeshafanikiwa kuwagawa walibya. So it ill be just a matter of time tutasikial ibya inagawanyika. Je kugawayika huko ni kwa faida ya walibya. Wapo watakaosema ndiona zipo hoja lakini hata kama ni wa faida ya walibywa behind the sncene ni kwa faida ya wakuu wa dunia. Hata mrusi kamtosa Libya. Hisia zangu ni kuwa Gadfi alikuwa anazidi uwa china oriented kwa mambo ya silaha.......

  Tanzania- Tanzania tumekarirshwa kudharau na kuwaponda wachina. So far tuko safe kiasi. kama ni kugawanyika tutagawanyika wa sababu zetu wenyewe za internal. Lakini the more tukiwa china oriented usishangae extenal forces( UK,USA) na pressure za kutugawa zikaogezeka. Na kwa sumu ya dini iliyopo tayari mhhh . The so called most peaceful country in africa itakuwa the most bloodiest.... tuombe yasitokee na hawa wansiasa wetu........ kadiri siku zinavyowkeda probability ya haya kutokea inaongezeka.

  Mfano unajua ile rada ya BAE tanzania ingenunua kutoka china kwa kashfa kama ilivyo sasa kuna watu wasingruhusiwa kuingia UK au US. But sababu tulinunua rada kwa rushwa UK basi "wakubwa" wanajua kutuliza mambo


  Uwajibikaji mwema wana jf
   
 13. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,340
  Trophy Points: 280
  Tanzania nayo ukiacha zanzibar kujitenga sisi Wakwere tunataka nchi yetu kwani Wachagga mnatunyanyapaa sana sisi wapenda kiduku
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Warega na Wabembe ni kabila zinazofanana mno ni kama Wasukuma na Wanyamwezi ("cousin") Na ndio wenye SUD Kivu+ makabila mengine madogo, Tatizo kubwa wanalompinga kabila ni Kuwasupport Wanyarwanda (Banyamulenge) na sababu wanayotoa ni kuwa yeye sio Mcongoman, Baadaya Wanyamulenge kuingia congo na Kabila Mkubwa na kisha kuwatosa na kuanza kushirikiana na wahutu kuwaondoa Watusi na ndio kisa cha kumuua, Wanyarwanda (Watusti) walirudi na kujikusanya EastCongo (Nod ,Sud Kivu na MAniema) na wala hawakutoka congo na walianzisha mashambulio mengine mapya dhidi ya serikali ya Kabila mdogo,

  Watu wa UN walikuja na Operation ama Mjumuisho waliouita AMANI LEO, na madhumuni ilikuwa ni kuunganisha majeshi yote ya Wanyarwanda (Watutsi na Wahutu) na Wacongoman na kuwa na jeshi moja tu, Tatizo lililopo ni kuwa Mkuu wa Majeshi wa Province ya Sud Kivu ni Mtusti na wanaoshikiria division za Uvira, Baraka, Fizi zao pia ni watutsi, Hilo wacongo man walilipinga na wanalipinga mno na ndio kisa cha Jean Kutumba (Mayimayi) pamoja na Wahutu (FDRL) kuingia msituni kwa pamoja wakiwashambulia Watusti na pia kumpinga kabila
  Hawamkubali kabila na hata akichukua nchi kutakuwa na Tatizo kubwa tu

  Ni kweli Katanga ni mjumuisho wa Makabila Mengi tofauti tofauti, Lakini wao wanasubiri uchaguzi tu, Kabila anaweza kushinda kwa sababu yupo madarakani lakini watu hawamkubali na hilo ndilo linalowapa watu wa Katanga ile ya kusema kama Kabila akishindwa basi Wao watakuwa na nchi yao

  Nachowafananisha Wakasai na Wabembe sio Uwingi wala Umahili nalichosema ni kuwa Wakasai ni kama wabembe kwa sababu wote hawamkubali kabila na sasa wamepata nguvu kubwa ya kumpinga pale Tsekedi alipotangaza kugombea uraisi pamoja na Kabila, kampeni za Kumpinga na uchochezi ndio zinashika kasi
   
 15. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Republic Of South Tanganyika. (Lindi,Mtwara, Ruvuma) Yaja hiyo! Ngoja muziki wa gesi (Mnazi Bay) na Uranium (Tunduru na Namtumbo) na mafuta pwani ya miji ya Lindi na Mtwara. Patachimbika nasema kama naota leo.
   
 16. K

  Karry JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kwa upande wa tanzania bado hatutagawanyika
   
 17. K

  Karry JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  duh hii inawezekana miaka 5o ijayo kama hakutakuwa na mgawanyo bora wa mapato yatokanyo na bidhaa hizo kunufaisha wakazi wa maeneo hayo
   
 18. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mtazamo sio jimbo hapa zaidi ya maumivu..
   
 19. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,134
  Likes Received: 849
  Trophy Points: 280
  Nillishawahi kuweka thread inayozungumzia hili, niliandika taifa linalofuata baada ya Sudan ya kusini ni Tanzania ya Kusini. Waliniponda watu sana lakini mpaka sasa watu wa kusini wanahoji kwa nini gesi isafirishwe kwa mabomba mpaka Dar au Tanga??? Wao hawastahili maendeleo kama kanda zingine za nchi hii??!!!

  Wana uchungu hao maana mpaka bandari zao zimetelekezwa (Mtwara &Lindi)

  Kilimo ndo usiseme, korosho hamna kitu tena!!!
   
 20. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Mikoa ya Kusini ni bomu linalosubiri kulipuka. Rasilimali kibao zimeanza kuwatoa imani na utu Watawala wetu. Na mazowea ya uporaji na kutojali ni kichocheo cha ndoto ya wanakusini. Gesi toka Songosongo inawanufaisha watu wa mikoa mingine Gesi ya Mnazi Bay ikiunganishwa na ile ya Songosongo kuelekea Mwanza (rejea mipango ya NSSF kujenga bomba Mnazi Bay- Dar-Mwanza) itakuwa uamsho tosha kwa wenyeji wa huko. Tusubiri tuone!
   
Loading...