Nchi inasogea-bajeti ya dawa na vifaa tiba yapanda!!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,534
Hongera JPM na wasiotaka watakubali tu....BOMBARDIER ZITANUNULIWA KWA CASH NA HUDUMA ZA JAMII ZITABORESHWA...!!

Serikali imefanikiwa kuongeza upatikanaji wa dawa(essential medicines) na kufikia asilimia 83 hadi mwezi machi 2017.

Serikali imeongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka bilioni zipatazo thelathini hadi kufikia bilioni zipatazo miambili.

Ongezeko la bajeti hii limelenga kwenye kujenga viwanda vya dawa na vifaa tiba.Hii ni sustainable way of ensuring the availability of medicines and medical equipments.

Nategemea kuanza kuona bidhaa kama IV FLUIDS,WATER FOR INJECTIONS,SYRINGES na POPs zikitoka humu humu nchini kwa bei nafuu.

[HASHTAG]#HapaKazitu[/HASHTAG]
 
Ni bajeti imepanda au wamefanya re allocation ya fedha? wametoa sehemu nyingine na kuzipeleka kwenye dawa....bajeti inapanda kwa kawaida ila sio kwa kiasi kikubwa hivyo, na kumbuka pia makadirio ni tofauti na reality
 
Hela anazotumia ni za kwetu kodi zetu utamsifiaje kutumia hela zetu,afanye projects mpya ambazo tutaingizia hela awe entrepreneur hapo tutamsifia na sio kutukandamiza madeni
 
Upuuzi mtupu.
Karibu kila mwaka kwenye kila wizara budget inapanda lakini Pesa inayokuja kutolewa inapungua, mahitaji yanaongeza na huduma zinazidi kuzorota.

Acha maneno, lete pesa.
 
Katika mazingira ambayo Thamani ya Shilingi ya Tanzania inapoteza thamani, Mfumuko wa bei unazidi kuongezeka na idadi ya watanzania inazidi kuongezeka. Hapo unategemea Budget itakuwaje?
Kwanini budget isipande?
 
Ni bajeti imepanda au wamefanya re allocation ya fedha? wametoa sehemu nyingine na kuzipeleka kwenye dawa....bajeti inapanda kwa kawaida ila sio kwa kiasi kikubwa hivyo, na kumbuka pia makadirio ni tofauti na reality
Rais Trump alipoingia madarakani kitu cha kwanza kukishughulikia ilikuwa ni sera ya afya OBAMACARE hii ikimaanisha afya ni priority katika ustawi wa taifa.

Rais Magufuli alipoingia madarakani alifanya utumbuaji wa kwanza kabisa nchini, katika hospitali ya Muhimbili...hii ikimaanisha kuwa afya ilikuwa ni kero na priority ya Rais kuifanyia kazi.

Reallocation au jina lolote utakaloiita ni hoja zisizo na tija...Bado tunahitaji kuongezea bajeti zaidi kwenye sekta ya afya ili ifike mahali tuachane na "KWA HISANI TA TAIFA FLANI"
 
Upuuzi mtupu.
Karibu kila mwaka kwenye kila wizara budget inapanda lakini Pesa inayokuja kutolewa inapungua, mahitaji yanaongeza na huduma zinazidi kuzorota.

Acha maneno, lete pesa.
Mkuu soma post yangu vizuri utaelewa.
 
Katika mazingira ambayo Thamani ya Shilingi ya Tanzania inapoteza thamani, Mfumuko wa bei unazidi kuongezeka na idadi ya watanzania inazidi kuongezeka. Hapo unategemea Budget itakuwaje?
Kwanini budget isipande?
From 30 to 200 b...huo mfumuko ni wa zimbabwe au?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Tanzania siku hizi ujinga ni profession na qualification .... waweza kuwa mkuu wa mkoa au Wilaya
 
Unaeza ukawa na bajet ya milioni mia alafu ukaitekeleza kwa asilimia mia na mwingine akawa na bajeti ya milioni mia mbili alafu akaitekeleza kwa asilimia 25! Swala hapo ni utekelezaji sio mipango...
 
Unaeza ukawa na bajet ya milioni mia alafu ukaitekeleza kwa asilimia mia na mwingine akawa na bajeti ya milioni mia mbili alafu akaitekeleza kwa asilimia 25! Swala hapo ni utekelezaji sio mipango...
ili ufike unahitaji hatua ya kwanza....hatua ya kwanza ni bajeti...ambayo kwa miaka mingi haikugusa eneo nyeti la kuondoa upungufu wa dawa.
 
From 30 to 200 b...huo mfumuko ni wa zimbabwe au?

Zamani nilikuwa nikisia bajeti ya kiasi fulani nilidhani hiyo hela inapelekwa kweli, kumbe ni figure watu wanaweka tu na wanaweza wasizipeleke na wala hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa. Inanikumbusha wakati tunawatongoza visichana vidogovidogo tunaviahidi mambo kibao ili tuvile uroda, lakini kikishakupa wala hakuna chochote cha maana unakipa kwani uwezo wa kutimiza hizo ahadi huna. Ndio hayohayo unataka tusifie hiyo bajeti ya 200b lakini kiuhalisia hela inayopelekwa huko haizidi hata 25b. Nenda mkawasomee watu wa vijijini hiyo bajeti ya 200b lakini hawaoni chochote cha maana kwenye huduma za afya bali shida ya matibabu iko palepale.
 
Bado nitaendelea kuwa kutoamini hizo percent zilizosemwa kisiasa,mwezi uliopita jirani yng mke wake alienda kujifungua hosptali ya umm(ngazi ya mkoa),walimwambia alete gloves pair za kutosha,bomba la sindano idadi ya kutosha.Kisa hosptali haina vifaa.So wanasiasa wanapokuwa wanapayuka wawe wanachunguza kujua reality ya wananchi wake kabla ya kupayuka!!
 
Aisee hizi akili Mungu tu asaidie hivi umejiuliza mpaka tarehe 30 April bajet iliyipita ilikuwa imetekelezwa kwa asilimia ngapi kwenye hiyo wizara?
 
Hongera JPM na wasiotaka watakubali tu....BOMBARDIER ZITANUNULIWA KWA CASH NA HUDUMA ZA JAMII ZITABORESHWA...!!

Serikali imefanikiwa kuongeza upatikanaji wa dawa(essential medicines) na kufikia asilimia 83 hadi mwezi machi 2017.

Serikali imeongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka bilioni zipatazo thelathini hadi kufikia bilioni zipatazo miambili.

Ongezeko la bajeti hii limelenga kwenye kujenga viwanda vya dawa na vifaa tiba.Hii ni sustainable way of ensuring the availability of medicines and medical equipments.

Nategemea kuanza kuona bidhaa kama IV FLUIDS,WATER FOR INJECTIONS,SYRINGES na POPs zikitoka humu humu nchini kwa bei nafuu.

[HASHTAG]#HapaKazitu[/HASHTAG]
Bajeti ya afya ya mwaka uliopita , imetekelezwa kwa asilimia ngapi ? Mipango siyo matumizi mjomba .
 
Bado nitaendelea kuwa kutoamini hizo percent zilizosemwa kisiasa,mwezi uliopita jirani yng mke wake alienda kujifungua hosptali ya umm(ngazi ya mkoa),walimwambia alete gloves pair za kutosha,bomba la sindano idadi ya kutosha.Kisa hosptali haina vifaa.So wanasiasa wanapokuwa wanapayuka wawe wanachunguza kujua reality ya wananchi wake kabla ya kupayuka!!
Hospitali gani mkuu?
 
Tutakutana utelelezaji.....tunaomba fedha zifike tu isijekuwa yaleyale ya 2% ya budget
 
Back
Top Bottom