Umeandika uzi huu ukiwa tayari umekunywa chai iliyotengenezwa kwa nishati ya umeme.
Chai uliyokunywa imekolezwa na sukari ya kilombero
Sukari hiyo imeletwa katika barabara zilizo karabatiwa na srikali ya CCM
Na kama umekula kamhogo , kamefika hapo kwa magari yaliyotumia diesel ambayo haijapanda bei muda sasa
unaandika uzi huu baada ya kuchaji ka samsung kao au kompyuta mpakato ofisini- kwa nishati ile ile
Zaidi ya hapo, pengine huna mipango yoyote ya kipato cha ziada, kana mtadi vile
Walia zaidi kwa kunyoosha mikono kama Matonya ili kipato kiongezwe kwa kutokana na kodi
Mimi niko likizo lakini nina uhakika wewe ukiwa kazini unatumia muda wa mwajiri wako,unamwibia!
Tatizo kubwa zaidi la Watanzania ni kutojua jinsi ya kujikomboa kiuchumi, hivyo macho yote yako kwenye siasa.