Nchi imemshinda ndio maana anajutia Urais

Nchi imemshinda ndio maana anajutia Urais

Mi sitarajii kuboresha sekta ya elimu ni kazi ya mwaka mmoja. Serikali inafanya kazi kwa mipango. Kama umesoma mpango wa miaka itano ya maendeleo ungesema may be mipango hiyo haitaweza kuboresha elimu ama sekta zinginezo.

Hapa ni kama unatuongopea kwa hoja dhaifu, huo mpango wa miaka mitano nilianza kuuonga mwaka 2014 kama sikosei, mpaka sasa ni karibia miaka 3 na ushee, lakini madawati ni hayo watu wamechangishwa. Hebu tuambie uboreshaji upi unausema ndugu yangu. Fafanua kwa hoja zinazoweza kutuingia akilini ni kwa kiwango gani uboreshaji wa elimu mpaka sasa umefanyika.
 
Du kweli kiongozi hujielewi kweli mpango wa mika mitano umepitishwa na Bunge lako. Hivi kweli tunasoma na kujua mipango ya serikali hii. Mbona hujielewi kaka. Miaka mitatu iliyopita du. No research no right to speak kaka. Jitahidi kufuatialia kidogo utakuwa unaelewa na kuleta hoja za msingi.
 
Urais ni kazi inayotaka hekima Sana, yeye anaendesha nchi Kwa chuki, ana chuki kubwa sana na wapinzani.
Halafu eti kila Siku anasema tumwombee,Mungu hawezi kusikia Maombi yetu Kwa Sababu yeye hayuko sawa Kimatendo ,hatendi sawa na Mungu anavyotaka.
Ametudhulumu wafanyakazi mafao yetu, halafu anasema tujiajiri, tutajiari na nini? wakati mitaji yetu wanaishikilia?
Maisha yamekuwa magumu bila Sababu.
Hiyo TWAWEZA ni taasisi ya ccm, ndo wanamdanganya rais kuwa anapendwa wakati anachukiwa haijawahi kutokea.
Mbona twaweza ya Rakesh Rajan ilikuwa safi, lakini hii nani anaongoza ?
 
Mda JPM aliokaa madarakani km umempa 35℅ukilinganisha na mda aliokaa mtangulizi wake nambaye umempa 30℅ basi tegemea mambo mazuri siku za usoni,mtu aliyefanya kazi miaka 10 na akapata 30℅ kwa mujibu wa vipimo vyako utamlinganishaje na mtu aliyefanya kazi kwa mwaka 1 tu na umempa 35℅?

Kwa taarifa yako JK hapo mwanzo alifikia 55%, ila akaishia na hiyo 30%. Huyu kaanza na hiyo 35% tutarajie kupanda au kushuka. Ila huenda akashuka kwani moja nililojifunza kutoka kwake anadhani yuko sahihi na yoyote anayempinga anataka urais wake. Kibaya zaidi hao washauri wake wanamuogopa ile mbaya, na kwa sababu hiyo inabidi yeye mwenyewe aje huku mitandaoni mlikoweka sheria za mitandaoni kuja kuuona taswira halisi ya utawala wake, na kwa kuwa hataki kukosolewa kwa kudhani yuko sahihi ndio anaomba malaika waje wafunge mitandao!!!

Nikuambie kitu ndugu, dhamira njema anayoisema haijawahi kuwa ndio ukweli wa kufanya wananchi wapate maisha bora. Mimi sijui umri wako, lakini hakuna ubishi kwamba hakuna rais aliyewahi kuipenda Tanzania kama Mwl. Nyerere, lakini pamoja na kuipenda na nia njema yake ndio hapo wananchi tulivaa mpaka nguo za viraka, na sehemu kubwa kabla ya yeye kutoka madarakani viwanda vingi vilikuwa hoi bin taabani. Hii yote ilichangiwa na yeye kujiona yuko sahihi na wale washauri wake wote walikuwa hawathubutu kumshauri. Kosa lile lile la Nyerere naona linakuja kujitokeza na sasa. Hapa ni muda utaamua.
 
Urais ni kazi inayotaka hekima Sana, yeye anaendesha nchi Kwa chuki, ana chuki kubwa sana na wapinzani.
Halafu eti kila Siku anasema tumwombee,Mungu hawezi kusikia Maombi yetu Kwa Sababu yeye hayuko sawa Kimatendo ,hatendi sawa na Mungu anavyotaka.
Ametudhulumu wafanyakazi mafao yetu, halafu anasema tujiajiri, tutajiari na nini? wakati mitaji yetu wanaishikilia?
Maisha yamekuwa magumu bila Sababu.
Hiyo TWAWEZA ni taasisi ya ccm, ndo wanamdanganya rais kuwa anapendwa wakati anachukiwa haijawahi kutokea.
Mbona twaweza ya Rakesh Rajan ilikuwa safi, lakini hii nani anaongoza ?
Wajinga mpo wengi Sana, hao wanaojenga maghorofa na wewe na ka kibanda kako, ni asilimia ngapi ktk idadi ya watanzania mil 40 wenye akili timamu?
Hivi Kwa nini watu hatufikirii kutumia kichwa?
Utafiti wa taasisi yoyote ile unaoikosoa serikali ya JPM ni lazima uitwe uchochezi na hiyo taasisi itafungiwa pia .
Hujiulizi hivi kampuni ya Benchmark production ilikuwa na kipato gani hadi idaiwe kodi ya bil 6 Kwa miaka 7 ?ina maana kila mwaka ilitakiwa ilipe kodi zaidi ya mil 800 ?hata migodi ya dhahabu hailipi kodi ya hivyo.
Chuki ya wazi ipo wote walio kinyume na serikali hii.
Mungu yupo, wakati si milele.
daah umenikumbusha mkuu, wakati wa BSS ceaser alisema hapa kazi tu, daah Madam akammaind saana, nafikiri hapo ndio palipomponza madam, lakini madam alikuwa sahihi kuwa neutral
 
Du kweli kiongozi hujielewi kweli mpango wa mika mitano umepitishwa na Bunge lako. Hivi kweli tunasoma na kujua mipango ya serikali hii. Mbona hujielewi kaka. Miaka mitatu iliyopita du. No research no right to speak kaka. Jitahidi kufuatialia kidogo utakuwa unaelewa na kuleta hoja za msingi.

Wewe hujui usemalo, hilo uliloliona juzi ni kama kuongezea rangi tu kwenye huo mpango. Kwa mara ya kwanza hili jambo lililetwa bungeni wakati Wassira akiwa waziri katika ofisi ya rais, akasoma mpango wa miaka mitano wa taifa. Ndio wakaja na blabla za neno BRN na ikaundwa na kamati ya BRN sijui kikosi kazi na hadithi za namna hiyo. Hapo ndio tukaona wanafunzi wakifaulu hata wasiojua kusoma na kuandika. Ama wakati huo ulikuwa hujaanza kufuatilia siasa ndugu yangu? Wewe kaa hapo ukiwa umemezeshwa mistari ushindwe kuhoji na ujitoe mpaka kumbukumbu.
 
Kiongozi jitahidi kufanya kazi za maana hela haziji kilaini kama ulivyozoea. Sisi tunaofanya private sekta tumezoea kuishi kwa mshahara. Hizi disposable income mlizozoea kuzipata burebure ziende kujenga shughuli za jamii kama barabara, gharama za shule, madawa na mengine. Tusipende kulalamika ifikie wakati tujiongeze.
Kuna watu wachache walikua hawagusi mishahara yao kwakua waliishi kupata posho mbali kwa kipindi kirefu hao ndiyo wengi wao wanatokwa sana mapovu awamu hii.Mnyoosho wa JPM umewafikia.
 
Hii ni Orodha ya Watu na taasisi zinalalamika kuwa hali ya Maisha yao ya kila siku imezidi kuwa Ngumu na haina matumaini tena.

1/Watumishi wa Serikali.
2/Wafanyabiashara.
3/Wanasiasa.
4/Wasanii.
5/Wafanyakazi wa sekta binafsi.
6/NGO's
7/Watalii.
8/Wanafunzi.
9/Wasafirishaji.
10/Wakulima.
11/Wabunge.
12/Taasisi zote za Serikali (Ikulu, Wizara, Manispaa, Halmashauri, Shule, Vyuo, Mashirika ya Umma nk.)

Kote huko ni Kilio tena kilio kikubwa. Na kote huko wanasema kuwa chanzo kikubwa ni 'mtukufu' mara nyingi amekuwa akifanya maamuzi yake binafsi, tena yasiyozingatia TARATIBU, HEKIMA na UTU.
Fafanua kwa kila kundi,vinginevyo huo utakua umbea tu.
 
URT=United Republic of Tanzania
Thanks that's good,unajua watu wanaogopa sana kuwa wazi na ndo shida ya tz.hatuko open ktk mambo mengi na ndo maana tunaoneka wema kumbe,siyo.nchi inatafunwa tu ndo kazi kubwa ambayo Mh Rais anapambana nayo.
Wanalipa kodi kumbe hawalipi.
JPM kumbe ni John Pombe Magufuli
 
Kaka k
Wewe hujui usemalo, hilo uliloliona juzi ni kama kuongezea rangi tu kwenye huo mpango. Kwa mara ya kwanza hili jambo lililetwa bungeni wakati Wassira akiwa waziri katika ofisi ya rais, akasoma mpango wa miaka mitano wa taifa. Ndio wakaja na blabla za neno BRN na ikaundwa na kamati ya BRN sijui kikosi kazi na hadithi za namna hiyo. Hapo ndio tukaona wanafunzi wakifaulu hata wasiojua kusoma na kuandika. Ama wakati huo ulikuwa hujaanza kufuatilia siasa ndugu yangu? Wewe kaa hapo ukiwa umemezeshwa mistari ushindwe kuhoji na ujitoe mpaka kumbukumbu.
ila serikali inapoingia madarakani lazima iandae mipango ya maendeleo na kuiwasilisha Bungeni. Hivi unazungumzia serikali ya Dr. Kikwete ama ya Dr. Magufuli. Usichanganye mada hapa iliujielewe vizuri. Mpango wa maendeleo unawasilishwa bungeni kila baada ya Serikali kuwa madarakani na ni hitaji la kikatiba.
 
Huo muono wako umegubikwa mihemko haiwezekani JPM awe hana kipaji cha uongozi km unavyodhania,kumbuka kua mamlaka zote hutoka kwa Mungu,na JPM tumepewa na Mungu kwa hiyo km yote aliyoyafanya hayakufurahishi utakua una bahati mbaya,kumbuka hata Mungu naye si yote anayoyafanya yanamfurahisha kila mmoja.
nashukuru mkuu.
 
Kaka k

ila serikali inapoingia madarakani lazima iandae mipango ya maendeleo na kuiwasilisha Bungeni. Hivi unazungumzia serikali ya Dr. Kikwete ama ya Dr. Magufuli. Usichanganye mada hapa iliujielewe vizuri. Mpango wa maendeleo unawasilishwa bungeni kila baada ya Serikali kuwa madarakani na ni hitaji la kikatiba.

Kwa ujinga huo ndio maana tunaishia kujichanganya kama taifa. Kumbuka serekali hii ni ya chama kilekile na wala sio ya chama kingine. Kulikuwa kuna haja gani ya serekali iliyopita kupitisha mipango ya miaka 5-10 ya maendeleo mwaka 2014 wakati ilikuwa inajua kabisa mwaka 2015 inafikia mwisho, na serekali inayokuja itapaswa kuweka mezani mpango wake wa maendeleo? Tukiambiwa sisi ni wajinga utakataa kwa dharau hiyo? Sasa mnapotuona tunapiga kelele kwamba chama hiki cha ccm kimeshindwa kuongoza nchi mnakasirika nini? Mkiambiwa mnaiga mambo bila kuwa na mkakati halisi mnapinga nini, awamu iliyopita viongozi wa toka chama hichohicho kilicho madarakani rais aliyepo madarakani akiwa waziri, mlipinga elimu bure haiwezekani, leo hii ni nini mnafanya? Yaani watanzania kuwa wajinga ndio mmeamua kufanya mipango ya maendeleo kwa maigizo?
 
Tushajifunza hasa sisi walimu tulioko kitaa,katunyoosha!..hakuna imani nae tena.haya mateso tunayopitia na muda wetu hajali.anajali ndege tu
 
Kwa ujinga huo ndio maana tunaishia kujichanganya kama taifa. Kumbuka serekali hii ni ya chama kilekile na wala sio ya chama kingine. Kulikuwa kuna haja gani ya serekali iliyopita kupitisha mipango ya miaka 5-10 ya maendeleo mwaka 2014 wakati ilikuwa inajua kabisa mwaka 2015 inafikia mwisho, na serekali inayokuja itapaswa kuweka mezani mpango wake wa maendeleo? Tukiambiwa sisi ni wajinga utakataa kwa dharau hiyo? Sasa mnapotuona tunapiga kelele kwamba chama hiki cha ccm kimeshindwa kuongoza nchi mnakasirika nini? Mkiambiwa mnaiga mambo bila kuwa na mkakati halisi mnapinga nini, awamu iliyopita viongozi wa toka chama hichohicho kilicho madarakani rais aliyepo madarakani akiwa waziri, mlipinga elimu bure haiwezekani, leo hii ni nini mnafanya? Yaani watanzania kuwa wajinga ndio mmeamua kufanya mipango ya maendeleo kwa maigizo?
Hapa kaka unachanganya madesa. Kuna National Vision 2025, kuna one year development plan, kuna five year development plan. Serikali ya Dr. Kikwete ilikuwa na mipango yake ya miaka mitano mitano iliyotokana na sera ya chama chake kwa kipindi husika. Pia serikali hii imeingia madarakani kwa sera ya chama cha rais hivyo kuitekeleza lazima kuwe na mpango wa miaka mitano utakaopima mafanikio ya hiyo sera. Pia hata chadema wangeshinda wangefanya hivyo ila wasingeweza kubadili national vision 2025. Kila mpango unaotengenezwa lazima ulenge kufikia hiyo dira kaka.
 
Back
Top Bottom