Nchi imemshinda ndio maana anajutia Urais

Nchi imemshinda ndio maana anajutia Urais

Joined
Mar 5, 2016
Posts
39
Reaction score
62
Anatumia nguvu kubwa sana kupambana na mambo madogo. Badala ya kutatua matatizo yetu na yeye amekuwa anatulalamikia sijui wananchi tufanyeje. Mara kadhaa kauli zake zimekuwa nizakujutia Urais.Alifikiri Urais ni kazi ndogo? Na anavyojifanya kubana hivi yaani kila kitu anabana tu atachoka sana.

Tatizo lake kubwa ni kuendesha nchi kwa utashi wake zaidi bila kufuata kanuni na taratibu za nchi pia kutokutaka kushaurika. Nchi huwezi kuiendesha kwa utashi wako tu halafu mambo yakaenda vizuri. Sio siri wananchi wengi kwa sasa wanamchukia Rais wetu kutokana na aina ya uongozi wake.

Hivi sasa Watumishi wa serikali ndio hawataki hata kumsikia, vijana waliohitimu vyuoni ndio wanamchukia balaa. Rais asidanganywe na takwimu fake zilizotolewa na Taasisi ya Twaweza eti anakubalika kwa asilimia 96. Watanzania wengi sasa hivi hawampendi Raisi kwa sababu hali ya maisha imezidi kuwa ngumu.

Nchi imeshamshinda kabsa, badala ya kuwasaidia maendeleo watanzania amegeuka kuwa kikwazo cha maendeleo kwa wananchi wanyonge.
 
Magufuli akiona wanamzingua ahamie ACTwazalendo tu.
 
Vuta subira yeye ni rais wa wanyonge hivyo mambo yatakaa vizuri tuko kwenye kipindi anachokiita "transition period" cha kuwafanya watu waliokuwa wanaishi kama malaika waishi kama shetani and vice versa is true.
Tumpe muda utaongea zaidi
 
Urais ni kazi inayotaka hekima Sana, yeye anaendesha nchi Kwa chuki, ana chuki kubwa sana na wapinzani.
Halafu eti kila Siku anasema tumwombee,Mungu hawezi kusikia Maombi yetu Kwa Sababu yeye hayuko sawa Kimatendo ,hatendi sawa na Mungu anavyotaka.
Ametudhulumu wafanyakazi mafao yetu, halafu anasema tujiajiri, tutajiari na nini? wakati mitaji yetu wanaishikilia?
Maisha yamekuwa magumu bila Sababu.
Hiyo TWAWEZA ni taasisi ya ccm, ndo wanamdanganya rais kuwa anapendwa wakati anachukiwa haijawahi kutokea.
 
Mmebanwa na bado mtalia lia sana ngosha ataendelea kuwakamua damu wadanganyika
 
Urais ni kazi inayotaka hekima Sana, yeye anaendesha nchi Kwa chuki, ana chuki kubwa sana na wapinzani.
Halafu eti kila Siku anasema tumwombee,Mungu hawezi kusikia Maombi yetu Kwa Sababu yeye hayuko sawa Kimatendo ,hatendi sawa na Mungu anavyotaka.
Ametudhulumu wafanyakazi mafao yetu, halafu anasema tujiajiri, tutajiari na nini? wakati mitaji yetu wanaishikilia?
Maisha yamekuwa magumu bila Sababu.
Hiyo TWAWEZA ni taasisi ya ccm, ndo wanamdanganya rais kuwa anapendwa wakati anachukiwa haijawahi kutokea.

Mungu husaidia mwenye haki. Twaweza ni chama cha siasa
 
yaani naishiwa hata maneno, tukabwa, hatuna pa kupumulia, ukikutwa tu hapo hapo huna kazi jaman , kweli ndio, mikataba ya kazi hiyo, asante raisi,
 
Utafiti wa twaweza ni sawa na kujitekenya alafu ukacheka mwenyewe, waligawa simu kwa watu alafu hao hao ndio wanawafanyia utafiti huku January na mwigulu wakiwa pembeni unategemea majibu yatakuaje?
 
Twaweza pamoja na kuitaja ni taasisi ya utafiti ya ccm ila imetoa ripoti yake, ningependa kuona utafiti wa taasisi nyingine itoe report tujue kipi ni kipi ila kusema maisha magumu kwa kila mwananchi bila utafiti binafsi sielewi! watu wanajenga tena majumba ya kifahari kwa pesa zipi ikiwa unasema hali ni tete kwa kila mwananchi?
Kiukweli niseme, binafsi nimeanza kujitegemea kimaisha mwaka 2003 na katika kipindi chote cha JK nilishindwa hata kujenga kibanda ila kwa kipindi hiki hata mwaka haujaisha mambo yangu yameanza kwenda vizuri na hata kibanda nimejenga pasipo presha kabisa!
Sema una hali ngumu usiwajumuishe wananchi wote! Jpm pamoja na mapungufu yake kama mwanadamu anaweza kuthubutu kutenda analoliamini pasipo uoga! Kauli za kukata tamaa ni za mzaha tu ila aina ya akina Jpm ndiyo hubadilisha katiba itawale zaidi ya mihula pangwa awali!
 
Hao wanaojenga maghorofa na wewe na ka kibanda kako, ni asilimia ngapi ktk idadi ya watanzania mil 40 wenye akili timamu?

Utafiti wa taasisi yoyote ile unaoikosoa serikali ya JPM ni lazima uitwe uchochezi na hiyo taasisi itafungiwa pia .
Hujiulizi hivi kampuni ya Benchmark production ilikuwa na kipato gani hadi idaiwe kodi ya bil 6 Kwa miaka 7 ?ina maana kila mwaka ilitakiwa ilipe kodi zaidi ya mil 800 ?hata migodi ya dhahabu hailipi kodi ya hivyo.
Chuki ya wazi ipo wote walio kinyume na serikali hii.
Mungu yupo, wakati si milele.
 
nyie wacheni bana ngosha apige mzigo.Rais ni yeye,mawazo yake tuu ndio sahihi.km mliweza kumuamini nakumchagua kuwa rais kwanini sasa hamuamini anayoyatenda...
Na ndio nyie nyie mliomkashifu sn jakaya,leo mnamkashifu magu.tuwaelewe vp ss.
ngoshapiga mzigoooo.maisha mazuri yawe ni majaaliwa sio kwa wizi waloouzoeaaaaaa pumbafu hawa.
yani wanataka bandari iwe huru no kodi km kanisani.....
 
Back
Top Bottom